Friday, September 27, 2019
Bashe Asema kuna upotevu wa zaidi ya Bilioni 120 kwenye vyama vya ushirika
Naibu Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), wamebaini kuwepo kwa upotevu wa jumla ya shilingi Bilioni 123 kwenye vyama vya ushirika.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa bodi ya pamba nchini kinachofanyikia kwenye ukumbi wa benki kuu (BOT) jijini Mwanza ambapo ameeleza kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua kali.
"Hapa nina kabrasha, nitawapatia wakuu wa mikoa wote na nitamkabidhi kiongozi wa tume, kwa ripoti ya COASCO ushirika kumetokea jumla ya upotevu wa sh. Bilioni 123, na nisema hapa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika wote," amesema.
"Hizi ni pesa za wakulima, wote waliohusika katika huu upotevu watachukuliwa hatua kali na wakuu wa mikoa tutawapa majina ya Amcos gani wanahusika na mnatakiwa kuchukua hatua," amesema Bashe.
Aidha ameongeza kuwa ushirika uliopo kwa sasa unahitaji mabadiliko makubwa kwani hauwezi kutatua matatizo ya kilimo hasa kwenye zao la pamba, ambapo mfumo unatakiwa kubadilishwa kutoka ushirika wa kuhudumia wakulima na kuwa ushirika wa kibiashara.
DC MWAIMU AWATANGAZIA KIAMA WANAOJUMU MIRADI YA MAENDELEO KYERWA
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mh. Rashid Mwaimu
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Mhe. Rashid Mwaimu
amesema atapambana vikali usiku na mchana ili kuhakikisha anakomesha watu wanaotaka kuhujumu miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi itolewayo na serikali akibainisha kuwa yupo tayari kukesha katika maeneo yote ya miradi ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.
Mkuu huyo wa wilaya hiyo Rashid Mwaimu ametoa kauli hiyo Septemba 27.2019 ofisini kwake wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo wilayani hapo.
Mhe.Rashid amesema atahakikisha analinda na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoletwa na serikali wilayani humo huku akiahidi kuwashughulikilia wale wanaokutaka kufanya vitendo vya kuihujumu serikali.
Amesema kutokana na jitihada, nguvu na busara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika utekelezaji wa miradi ya ki maendeleo yeye kama mkuu wa wilaya hatomfumbia macho mtu yeyote anayepanga kuhujumu miradi hiyo.
"Nawaahidi miradi yote inayoletwa na serikali kwa ajili ya wilaya ya Kyerwa nitaisimamia na kuilinda kwa nguvu zote, nitahakikisha adui yeyote haisogelei miradi hiyo ,miradi ni mali ya wananchi ole wenu mliozoea kuitafuna muda umekwisha, nitacheza na nyie usiku kucha", alisema Mwaimu.
Hata hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kuwahimiza kutomchagua kiongozi mbishi, badala yake wachague kiongozi ambaye ni mzalendo na muadilifu atakayewaletea maendeleo.
Katika suala la ulinzi na usalama, amesema katika wilaya yake ulinzi na usalama ni wa kutosha hivyo amewataka wananchi kuripoti katika vyombo husika mara moja vinapojitokeza vitendo vya uvunjifu wa amani kwa baadhi ya watu wasiowaadilifu hasa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
KITABU CHA KUSAIDIA WANAWAKE WANAOWANIA NAFASI ZA UONGOZI CHAZINDULIWA KWENYE TAMASHA LA JINSIA 2019
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukifanyika leo Alhamis Septemba 26,2019 kwenye usiku wa Mwanamke wa Kiafrika wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam. Lengo la kitabu hicho ni kutoa taarifa muhimu kuhusu mashirika yanayosaidia jitihada za wanawake kuwania nafasi za uongozi kwa ngazi zote na kwa wanawake wa vyama vyote vya siasa. Kitabu hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Women Fund Tanzania kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya na Seidel Foundation. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Wanawake wakifurahia wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change'.
Wanawake wakifurahia wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change'.
Wednesday, September 25, 2019
VIDEO: Kocha Simba atamba kuishangaza Kagera Sugar
Kocha mkuu wa timu ya Simba, Patric Ausemsi ametamba kuondoka na pointi tatu muhimu katika uwanja wa Kaitaba katika mchezo ligi kuu ya Tanzania bara dhidi Kagera Sugar huku wachezaji wake wanne tegemeo wakiukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE
Source
ASKOFU MKUU YUDA THADEUS RUWA'ICHI ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI MOI LEO.....AMSHUKURU RAIS MAGUFULI NA TAASISI YA MIFUPA YA MUHIMBILI
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiongea kwa furaha na wanahabari mara baada ya kuruhusiwa kuondoka Taasisi ya Mifupa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa.
Wengine ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia).
Mhashama Askofu Mkuu Ruwa'ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu
Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MOI) pamoja na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia) baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali leo Jumatano Septemmba 25, 2019.
Mhashama Askofu Mkuu Ruwa'ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu.
Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.
PICHA NA ISSA MICHUZI
Source
Tuesday, September 24, 2019
Picha : TAMASHA LA 14 LA JINSIA LAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM..ANGALIA MATUKIO YOTE YALIYOJIRI HAPA
Balozi Getrude Mongella ambaye ni Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) na Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa wanawake duniani uliofanyika mwaka 1995 Beijing China amefungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 leo Jumanne Septemba 24,2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa kufungua Tamasha hilo litakalodumu kwa muda wa siku nne (Septemba 24 hadi 27,2019),Balozi Mongella maarufu 'Mama Beijing' amesema ili kujenga Tanzania ya Viwanda ni lazima wanawake na wanaume washiriki.
Balozi Mongella pia amehamasisha umuhimu wa wanawake kushirikishwa katika utengezaji wa Ilani za uchaguzi za vyama vya siasa ili kuhakikisha masuala ya wanawake yanaingizwa kufikia usawa wa kijinsia.
"Huu msemo wa Wanawake wakiwezeshwa wanaweza mimi nasema hii ni dhambi...hatupaswi kuwa omba omba...Sisi wanawake tunaweza tunachotaka ni vikwazo vinavyotukwamisha viondolewe njiani,tunataka wanawake washiriki kwenye utengenezaji wa ilani za uchaguzi ili Rais atakayegombea apewe na kubeba ajenda zinazohusu wanawake",alisema Balozi Mongella.
"Tuone masuala yanayotuhusu wanawake ni sehemu ya ajenda na uchaguzi utakapopita iwe rahisi kwa tutakayemchagua kuwa Rais kumuomba akimbizane na ajenda za wanawake na asipofanya hivyo atakuwa hajatekeleza Ilani",aliongeza Mama Mongella.
Hata hivyo aliipongeza serikali kwa kutekeleza ajenda za Mkutano wa Beijing mfano Sera ya elimu bure hali inayosababisha ongezeko la watoto wa kike kwenda shule na imeondoa kikwazo cha watoto kukosa elimu.
Aidha Balozi Mongella aliwataka wanasiasa kuepuka Rushwa huku akieleza kuwa Wanasiasa wanaohonga 'rushwa' ili wapate uongozi wanabaka siasa.
Naye Mgeni Maalumu kutoka serikalini,Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alisema Ukatili wa Kijinsia ni janga jipya linaloitia doa nchi ya Tanzania hivyo kuwaomba wadau wote kuungana kutokomeza hali hiyo.
"Hatuwezi kufikia usawa wa kijinsia katika taifa kama tunaendelea kuwa na matukio ya ukatili ya kijinsia ambayo nyuma yake yana sura ya mila,desturi,umaskini na ukosefu wa elimu.Naomba tuvunje ukimya na tuepuke kumaliza kesi zinazohusu masuala ya ukatili kwa kuyamaliza kienyeje",alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019.
Akielezea kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia 2019,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi alisema linahudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake kutoka ndani na nje ya Tanzania likiongozwa na mada kuu 'Wanaharakati wa jinsia mbioni kubadili dunia'.
"Tamasha hili lina umuhimu wa kipekee kwani tunaendelea kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya TGNP tangu ianzishwe mwaka 1993 na kidunia tumeanza kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio na Mpangokazi wa Beijing ambapo kilele chake ni mwaka 2020",alisema Liundi.
ANGALIA HAPA CHINI PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI
Balozi Getrude Mongella akifungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019.
Balozi Getrude Mongella akisalimiana na Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kufungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019.
Awali Balozi Getrude Mongella (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro wakifurahia jambo wakati akiwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao kwa ajili ya kufungua Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Meza kuu wakiwa wamesimama baada ya Balozi Getrude Mongella kuwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 wakiendelea na burudani wakati Balozi Getrude Mongella akiwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao kwa ajili ya kufungua tamasha hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
MC wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 ambaye ni Mwanachama wa TGNP Mtandao Ulu Mallya akitoa maelekezo mbalimbali wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wa tamasha.
Sehemu ya wageni waalikwa wakati wa tamasha hilo.
Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania,Anne Makinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Waziri Mkuu Mstaafu Tanzania,Joseph Sinde Warioba akizungumza wakati wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Washiriki wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019 wakicheza muziki.
Washiriki wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019 wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo.

Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019 likiendelea.

Mwakilishi wa balozi wa Ireland nchini akizunguza kwenye tamasha la 14 la jinsia 2019
Mwakilishi Mkazi Un Women nchini Tanzania akizunguza kwenye tamasha la 14 la jinsia 2019
Utoaji Tuzo maalum kwa viongozi wa serikali ambao wamechangia mabadiliko ya kisera kuwezesha masuala ya kijinsia kufanikiwa ikiwemo utekelezaji wa maazimio ya Beijing mwaka 1995.Kushoto ni Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao,Deogratius Temba akishikana mkono na Balozi Getrude Mongella baada ya kupokea cheti kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Benjamin Mkapa ambaye wakati wa uongozi wake aliweka mazingira wezeshi kupokea na kusaidia utekelezaji wa maazimio ya Beijing 1996.
Balozi Getrude Mongella akikabidhi tuzo kwa Mhe. Joseph Sinde Warioba ambaye ametunukiwa tuzo ya heshima kwa sababu kwa muda mrefu amekuwa mstari wa mbele kusimamia ajenda ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia kila mahali anapokuwa.
Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro akimkabidhi Balozi Getrude Mongella tuzo ya heshima kwa kumtambua kuwa mwanamke shupavu anayesimamia haki za wanawake na usawa wa kijinsia bila kutetereka.
Bhoke Wankyo Nyerere akipokea Tuzo ya Heshima iliyotolewa kwa hayati Baba wa taifa kama sehemu ya kuendeleza kuuenzi mchango wake katika kutetea,kulinda na kupigania haki za watu wote zikiwemo za wanawake na usawa wa kijinsia.
Tuzo ya heshima kwa Hayati marehemu Sophia Kawawa ikitolewa ikiwa ni tuzo ya heshima kuuenzi mchango wake katika kupigania haki za wanawake hasa waajiriwa.
Agripina Mosha akipokea kwa niaba ya Dr. Inj. Strato Mosha tuzo ya heshima kwake kwa kujitoa tangu awali kabisa wakati shirika la TGNP linaanza.
Mwakilishi wa Prof. Simon Mbilinyi akipokea tuzo ya heshima kwa kujitoa kwake kwa rasilimali na wakati mwingine ushauri
Utoaji tuzo kwa watu binafsi ambao walitumia rasilimali zao,muda,ushauri,kuwezesha TGNP Mtandao kusimama na kufika hapo ilipo sasa.
Dkt. Hellen Kijo Bisimb akionesha tuzo ya heshima aliyopewa kutokana na kuendeleza agenda ya ukombozi wanawake kimapinduzi ndani ya shirika la LHRC.
Vicky Tetema kutoka Under the Same Sun akipokea tuzo kutokana na kuendeleza agenda ya ukombozi wanawake kimapinduzi ndani ya shirika hilo.
Mary Lusindi akipokea tuzo kutokana na kuendeleza agenda ya ukombozi wanawake kimapinduzi ndani ya TGNP.
Usu Mallya akioesha tuzo ya heshima aliyopewa kutokana na kuendeleza agenda ya ukombozi wanawake kimapinduzi ndani ya TGNP
Usu Mallya akipiga picha na Mkurugenzi wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi baada ya kupewa tuzo ya heshima.
Perpetua Magoka akipokea tuzo ya heshima kwa niaba ya WLC
Utoaji tuzo ukiendelea
Mwakilishi wa halmashauri ya Kishapu akipokea tuzo kutokana na halmashauri hiyo kutenga fedha kwenye bajeti zake mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mrengo wa kijinsia baada ya kujengewa uwezo na TGNP Mtandao.Halmashauri hiyo pia imetenga bajeti kuwezesha wasishana waliopo shuleni kupata taulo za kike bure wanapozihitaji.
Mwakilishi wa halmashauri ya Kisarawe akipokea tuzo kutokana na halmashauri hiyo kutenga fedha kwenye bajeti zake mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mrengo wa kijinsia baada ya kujengewa uwezo na TGNP Mtandao.Halmashauri hiyo pia imetenga bajeti kuwezesha wasishana waliopo shuleni kupata taulo za kike bure wanapozihitaji.
Mwakilishi wa halmashauri ya Morogoro akipokea tuzo kutokana na halmashauri hiyo kutenga fedha kwenye bajeti zake mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mrengo wa kijinsia baada ya kujengewa uwezo na TGNP Mtandao.Halmashauri hiyo pia imetenga bajeti kuwezesha wasishana waliopo shuleni kupata taulo za kike bure wanapozihitaji.
Mwakilishi wa UN Women nchini Tanzania akipokea tuzo ya heshima
Mwakilishi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg akipokea tuzo ya heshima
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao akipokea tuzo ya heshima kwa kupigania masuala yanayohusu wanawake.
Wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakipiga picha ya pamoja baada ya mkurugenzi wa TGNP Mtandao kupokea tuzo.
Wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakipiga picha ya pamoja baada ya mkurugenzi wa TGNP Mtandao kupokea tuzo.
Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe kufungua maonesho kwenye Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019.
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...