Malkia wa Muziki wa Afrika, Mama Yvonne Chaka Chaka tayari yupo visiwani hapa kwenye tamasha la 22 la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF) ambapo atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo makongamano na Wanawake pamoja na wadau wengine wakiwemo wasanii wa filamu na muziki.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa ZIFF, Isihaka Mlawa amebainisha kuwa, Mama Yvonne ni miongoni mwa wageni maalum kwa mwaka huu ambapo pia atafanya shughuli za kijamii ikiwemo makongamano na warsha ya Wanawake, wasanii wa filamu na wale wa muziki shughuli zilizoandaliwa na ZIFF 2019.
"Mama Yvonne Chaka Chaka amefika jana Zanzibar na leo ataendelea na programu maalum ikiwemo kukutana na Wanafunzi wanaopata mafunzo ya filamu lakini pia atakutana na Wasanii wa muziki kutoka Chuo cha Muziki cha Dhow Country Music Academy." Alieleza Isihaka.
Aidha, Isihaka Mlawa ameongeza kuwa, wanatarajia Mama Yvonne Chaka Chaka na mwanamuziki aliyeimba wimbo wa Zanzibar miaka 40 iliyopita, Sipho Mabuse kufanya tukio maalum la muziki kidogo kwenye shughuli za tamasha hilo linaloendelea visiwani hapa na kutarajiwa kufikia tamati Julai 14, mwaka huu.
Mama Yvonne Chaka Chaka na Sipho Mabuse wapo visiwani hapa kama wageni maalum waalikwa wa tamasha hilo kwa mwaka huu ambapo wamekuwa kioo na kielelezo kutokana na nyimbo zao mbalimbali zilizotamba Bara la Afrika pamoja na umaarufu wao katika jamii inayowazunguka.
Msanii Mama Yvonne Chaka Chaka (Jina la kuzaliwa Yvonne Machaka ambapo alizaliwa mnamo mwaka 1965 ni mwimbaji kutoka Afrika ya Kusini.
Kuitwa kwake Malkia wa Afrika ni kutokana na kuwa mstari wa mbele katika muziki maarufu wa Afrika Kusini kwa miaka 20.
Nyimbo kama "I'm burning Up", "I'm in Love with a DJ", "I Cry for Freedom", "Makoti", "Motherland" na "Umqombothi" ("Pombe ya Afrika") zimeweza kumuweka kwenye ramani ya Afrika na kuwa maarufu zaidi.
Msanii huyo alizaliwa Dobsonville huko Soweto na alikuja kuwa mototo wa kwanza wa Kiafrika kuonekana kwenye televisheni Afrika Kusini. Mwaka 1981 "Sugar Shack", kipindi cha wenye talanta, kilimjulisha kwa umma wa Afrika Kusini.
Katika harakati za muziki, Chaka Chaka alianza kuimba akiwa na miaka 19 mwaka 1985 wakati Phil Hollis wa Dephon Records alimgundua mjini Johannesburg- Muda mfupi baada ya albamu yake "I'm in Love With a DJ", kuuzwa nakala 35,000.
Pia katika nyimbo zake zilizowahi kushinda tuzo mbalimbali ni kama "Burning Up", "Sangoma", "Who's The Boss", "Motherland", "Be Proud to be African", "Thank You Mr DJ", "Back on my Feet ", " Rhythm of Life "," Who's got the Power "," Bombani (Tiko Rahini), "Power of Afrika", "Yvonne and Friends" na "Kwenzenjani".
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
NA REBECA DUWE TANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Burian amewataka wananchi wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya ndoa na ardhi ...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
