Wednesday, July 10, 2019

Hospital mpya ya rufaa Njombe yaanza kutoa huduma




Na Amiri kilagalila-Njombe

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amefungua zoezi la utoaji wa huduma ya afya katika hospital mpya ya rufaa ya mkoa wa Njombe iliyofunguliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alipokuwa na ziara ya siku tatu kuanzia april 9 mwaka huu mkoani humo.

Akizungumza na wananchi kabla ya kukabidhi hospital hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka amesema kuwa awali mkoa wa Njombe ulikuwa ukitumia hospital ya kibena iliyochini ya halmashauri ya mji wa Njombe kuwa hospital teule ya mkoa.

Ili kuendelea kuboresha na kusogeza karibu huduma za afya mkoani humo waziri Ummy amesema kuwa hospital ya kibena haitoweza kuondolewa kifaa chochote huku akitoa wito kwa halmashauri ya mji wa Njombe kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa katika hospital hiyo.

"Hamkufanya makosa halmashauri kutukabidhi hospital ile ya kibena ninyi wenyewe ni mashahidi baada ya kuwa imeteuliwa hospital teule ya mkoa,hali ya utoaji huduma ilibadirika,sasa niseme pale katika hospital hatutaondoa.

chochote,na mimi ni matumaini yangu kwamba halmashauri mtaendelea kuboresha ili ipatikane huduma bora".

Katika hatua nyingine waziri Ummy amemkabidhi site mkandarasi  ili kuanza ujenzi wa majengo 7 ya kisasa katika ujenzi wa hatua ya pili na kumpa mkandarasi miezi 8 mpaka 10 na kumpongeza Rais kwa kutoa bilioni 7.65 kwa ajili ya ujenzi huo.

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka mara baada ya kuishukuru serikali kwa kuzindua huduma katika hospital hiyo,ameagiza halmashauri kuweka utaratibu mzuri wa usafiri ili wananchi waweze kupata huduma kufika katika hospital hiyo.

Mganga mfawidhi wa iliyokuwa hospital ya rufaa ya mkoa wa Njombe kibena Dkt.Winferd Kiambile,amesema miongoni mwa huduma zitakazotolewa katika hospital mpya ni pamoja na kliniki za kibingwa.

"Mh waziri nikuhakikishie kwamba watoa huduma tupo tayari kutoa huduma katika hospital hii,huduma zitakazotolewa ni  huduma za OP zote vile vile kuna kliniki za kibingwa,na huduma nyingine nyingi"

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo wamesema kuwa kuanza kutumika kwa hospital hiyo kutawapunguzia gharama kwa kuwa awali walikuwa wakifuata huduma kubwa za rufaa katika mikoa jirani ikiwemo Mbeya na Iringa.

Hospital ya rufaa ya mkoa wa Njombe kwa wagonjwa wa nje, awamu ya kwanza ya ujenzi umegharimu bilioni 3.2
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...