Thursday, July 4, 2019
Bei za bidhaa mbalimbali zimeshuka visiwani Zanzibar
Na Thabit HamidumZanzibar,
MKUU Wa Kitengo cha bei Khamis Abdulrahman Msham amesema hali ya mfumo wa bei za bidhaa umepungua kutoka asilimia 3.1 hadi kufikia 2.7 kwa mwaka uloishia June 2019 kwa bidhaa mbalimbali zinazotumiwa na wananchi tofauti visiwani Zanzibar.
Hayo ameyasema leo huko katika Ukumbi ya Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mkoa wa Mjini Unguja wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa kuripoti taarifa za bei kuhusu kushuka kwa bidhaa ikiwemo chakula.
Alisema mfumuko wa bei za bidhaa umepungua ikiwemo chakula kama vile mchele wa mapembe, mchele wa basmati, ndizi na samaki na pia mafuta ya taa.
Aliongeza kusema hali ya uchumi inaimarika vizuri ukilinganisha na nchi nyengine za Afrika Mashariki kwa jinsi kasi ya kupanda imepungua kutokana na uzalishaji uliyo mzuri.
Nae Meneja wa Idara ya Uchumi Tanzania Bank of Tanzania BOT Moto Ng'winganele Lugobi alisema hali ya mfumuko wa bei kwa sasa ni mzuri kutokana na uzalishaji wa mavuno uko vizuri na kuwataka wananchi kuzalisha mavuno kwa wingi.
Kwa upande wa Mhadhiri wa Uchumi kutoka chuo kikuu cha Taifa SUZA Suleiman Msaraka Pinja alisema Serikali ikianza bajeti huweka malengo yake hivyo lengo la mfumko wa bei usizidi ili wananchi waweze kumudu bei za bidhaa.
Hivyo lengo limetimia mfumo wa bei umeshuka na kuwataka wananchi waendelee kuzalisha chakula kwa utaalamu zaidi kwani wakifanya hivyo mfumko wa bei hautokuwa mkubwa.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 29, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...