Saturday, June 22, 2019

Vikao vya Kamati Kuu CCM kufanyika Dar

Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kinatarajia kufanya vikao vyake Kamati Kuu pamoja na Halmashauri kuu (NEC) wiki ijayo Dar es Salaam.

Wakati kikao cha kamati kuu vitafanyika Juni 26, 2019 kikao cha NEC kitafanyika Juni 27,2019 na kitakuwa cha kawaida kwa mujibu wa kalenda ya chama na Katiba ya CCM ibara ya 101(2).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ilisema kikao cha Kamati kuu kikitanguliwa na vikao vya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika Juni 24,2019 na kufuatiwa na semina ya makatibu wa mikoa Juni 25, 2019.

Polepole alisema semina hiyo itaendeshwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Philip Mangula pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati kuu ya Taifa.

Wajumbe wa vikao hivyo pia watapata fursa ya kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya CCM ya awamu ya Tano iliyo katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...