Monday, June 24, 2019
Maswali muhimu ya kujiuliza kabla ya kuanza kufanya biashara
Watu wengi wanaoingia kwenye biashara huwa wanakuwa na matumaini makubwa sana ya kufanikiwa kupitia biashara hiyo. Matumaini haya huwa yanatokana na kuona wengine wanafanya biashara ile wakiwa wanafanikiwa. Mara nyingine matumaini haya hutokana na kuona kuna watu wanaohitaji kile unachopanga kutoa.
Mara nyingi watu wanapoingia kwenye biashara hujikuta wakiona matumaini yale hayawezekani tena. Hii inatokana na kukutana na uhalisia wa kibiashara tofauti na kile walichokuwa wanafikiria kabla ya kuingia. Na mara nyingi matumaini haya hufa kutokana na soko la biashara kutokuwa la uhakika.
Kama wewe upo kwenye biashara, au una mpango wa kuingia kwenye biashara, hapa kuna maswali muhimu sana ya kujiuliza kuhusu soko la biashara yako. Kumbuka kwamba bila ya mteja wewe huna biashara, hivyo unavyojua zaidi kuhusu wateja wako ndivyo unavyoijua zaidi biashara yako.
Yafutayo ndiyo maswali ya kujiuliza wakati wa kuingia kufanya biashara:
Je biashara ninayotaka kufanya ina wateja?
Hili ni swali ambalo huwezi kuliruka. Ni lazima ujiridhishe kwamba kuna wateja wa biashara yako ili uweze kuendesha biashara husika.
Utajuaje kama kuna wateja wa biashara yako?
Angalia watu wenye shida ambayo biashara yako inaweza kutatua
Angalia mahitaji ya watu ambayo wanayakosa kwenye biashara zilizopo sasa.
Sikiliza malalamiko ya watu kwenye aina ya biashara unayofanya. Kama jibu ni ndio kuna wateja ndio unaweza kuendelea mbele. Kama jibu ni hapana, rudi kwenye meza na boresha wazo lako la biashara.
Je soko lina ukubwa wa kutosha?
Baada ya kujua kwamba kuna wateja wa biashara yako, pia unahitaji kujua kama wateja hawa ni wengi kiasi cha wewe kuweza kuendesha biashara yako vizuri. Unaweza kuwa na wazo zuri sana la biashara na kweli kukawa na wateja ila wateja wenyewe ni wachache kwa wewe kuweza kuendesha biashara yenye faida.
Hakikisha una soko la kukutosha ili uweze kufidia gharama zako za kuendesha biashara na kuweza kupata faida pia.
Je soko linafikika kwa urahisi?
Unaweza kuwa na biashara ambayo ina wateja na wateja ni wengi ila kuwafikia wateja wako ikawa changamoto kubwa sana. Kama wateja wamesambaa sehemu mbalimbali na biashara yako ni ya kuhitaji uwe sehemu moja inaweza kuwa changamoto kubwa kwako. Unahitaji kuwa na biashara ambayo itakuwa rahisi kwako kuwafikia wateja wako ili kuweza kufanya nao biashara.
Angalau kwa kipindi hiki imekuwa rahisi sana kufanya biashara kwa maeneo mbalimbali ila bado kuna maeneo ambayo yana changamoto kubwa.
Usiingie kwenye biashara kabla hujajiuliza maswali hayo matatu. Na kama tayari upo kwenye biashara, jiulize maswali hayo matatu na uone ni jinsi gani unavyoweza kuiboresha biashara yako zaidi ili uweze kuikuza na kupata faida zaidi.
Source
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...