Tuesday, June 4, 2019
Akimbizwa Hospitali Baada ya Kukaa ‘Airport’ Siku 10 Akimsubiri Mpenzi Aliyempata Mtandaoni..!!!
Mwanaume mmoja raia wa Uholanzi amejikuta akilazwa hospitalini baada ya kukaa katika Uwanja wa Ndege kwa siku 10 nchini China alipoenda kwa lengo la kukutana na mrembo aliyekuwa akiwasiliana naye mtandaoni, ambaye hakutokea.
Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Alexander Peter Cirk mwenye umri wa miaka 41, alisafiri kutoka Uholanzi na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changsha Huanghua kukutana na mrembo aliyemfahamu kwa jina la Zhang.
Hunan TV imeripoti kuwa Cirk alikataa kuondoka katika uwanja huo wa ndege, lakini hali yake ya afya ilizorota kwa kukosa maji ya kutosha na chakula, hivyo maafisa walilazimika kumkimbiza hospitalini.
Baada ya tukio hilo kuripotiwa kwenye vyombo vya habari, mrembo huyo alijitokeza na kufanya mahojiano na Hunan TV wakati mwanaume huyo alikuwa tayari amesharushwa nchini kwao.
Mrembo huyo alieleza kuwa alidhani mwanaume huyo anatania pale alipomwambia anaenda nchini China kwa ajili yake. Aliongeza kuwa wakati wote huo yeye alienda kufanya upasuaji (plastic surgery), hivyo simu yake ilikuwa imezima.
"Siku moja alinitumia picha ya tiketi za ndege ghafla na nilidhani alikuwa anatania. Hakuwahi kuwasiliana na mimi tena baadae," alisema mrembo huyo.
Hata hivyo, mwanaume huyo alipoulizwa wakati anarudishwa Uholanzi baada ya kutibiwa, alieleza kuwa anaamini atakaporudi nchini kwao wataendelea na uhusiano wao wa mapenzi mtandaoni.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...