Unapenda wimbo gani kutoka kwa mwanamziki Miriam Makeba? Binafsi huwa napenda nyimbo mbili kutoka kwa kwake ambazo ni malaika na hapo zamani japo mwanamziki huyu anazo nyimbo nyingi nyingi kama vile samba, pata pata na nyinginezo nyingi.
Mwanamziki Miriam Makeba alizaliwa tarehe 4 Machi 1932 katika jiji la Johannesburg huko Afrika Kusini. Mama yake alikuwa wa kabila la Swazi sangoma na baba yake wa kabila la Xhosa. Baba alifariki wakati Miriam akiwa na umri wa miaka sita.
Miriam alikuwa mwanamuziki pekee wakati huo aliyeweza kufanikiwa kuzieneza nyimbo zenye asili ya Kiafrika. Pia alikuwa miongoni mwa wanamuziki waasisi wa kuchanganya mitindo tofauti ya muziki na kutengeneza muziki wa kuvutia kama Kwaito.
Alianza kazi ya muziki mwanzoni mwa mwaka 1950 akiwa na kundi la The Skylarks, baadaye alijiunga na kundi la Manhattan Brothers. Makundi hayo yalikuwa yakipiga muziki wa Jazz wenye vionjo vya Kiafrika kusini.
Mwaka 1959, Miriam alifanya onyesho kubwa pamoja na Hugh Masekela maybe alikuja kuwa mume. Maonyesho aliyofanya pamoja na albamu nzuri alizorekodi havikumpatia faida, lakini baadaye alifanya matamasha katika nchi za Ulaya na Amerika.
Ulipoanza mkakati wa kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendelea Afrika ya kusini, Miriam aliamua kurudi nyumbani kupigania uhuru. Baadaye alialikwa Italia katika tamasha la filamu la Venice.
Kati ya nyimbo za Miriam zilizo maarufu ni Patapata (kwa lugha ya KiXhosa ni "Qongaqothwan"). Wimbo maarufu wa Malaika uliotungwa na Fadhili William Miriam aliuimba akishirikiana na Harry Belafonte.
Miriam alirudi tena nyumbani mwaka 1990, na mwaka 1992 alicheza filamu ya Sarafina.
Mwaka 2001 alitunukiwa tuzo ya dhahabu iliyoitwa Otto Hahn Peace Medal, pia alishika nafasi ya 38 kati ya wanamuziki bora kati ya 100 waliopewa tuzo nchini Afrika ya Kusini.
Mwaka wa 2005, Miriam alifanya ziara ya kimuziki kwa ajili ya kuwaaga marafiki wake wote duniani iliyomchukua miezi kumi na minne; alifanya maonyesho katika nchi zote alizotembelea wakati alipokuwa akifanya kazi ya muziki.
Aliaga dunia kwa shtuko la moyo alfajiri ya tarehe 10 Novemba 2008, nchini Italia baada ya kutoa onyesho la muziki.
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...