Friday, April 26, 2019

JE WAJUA KWANINI VIMBUNGA HUPEWA MAJINA?? ..MFANO KIMBUNGA KENETH...SOMA HAPA

Umewahi kusikia vimbunga vikiwa na majina ya kushangaza, kilichoitwa Idai kilichosababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe mwezi uliopita Machi katika kile ambacho Umoja wa mataifa unasema huenda ni janga baya zaidi la hali ya hewa kuwahi kushuhudiwa kusini mwa Afrika.

Matthew ambacho kilikumba maeneo ya Haiti, Jamaica, Jamhuri ya Dominika, Bahamas na baadhi ya majimbo ya Marekani mwezi Oktoba mwaka 2016.

Mwezi uliotangulia kulikuwa na kimbunga kingine kilichojulikana kama Hermine ambacho kilisababisha uharibifu mkubwa jimbo la Florida.

Lakini kinachokumbukwa sana ni kile kwa jina Katrina ambacho kiliathiri sana majimbo ya Louisiana, Mississippi na Alabama nchini Marekani.

Je, vimbunga hivi hupewa vipi majina?

Vimbunga katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico hupewa majina ya Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambalo lina makao yake makuu nchini Uswizi.

Zamani, ni majina ya kike pekee yaliyotumiwa lakini kuanzia 1979, majina ya kiume yalianza kutumiwa.

Huwa kuna makundi sita ya majina ambayo hutumiwa kwa mzunguko.

Hii ina maana kwamba majina yaliyotumiwa kwenye vimbunga mwaka hu hayatatumiwa tena hadi 2022.

Majina kwenye orodha hii yanaweza kubadilishwa na WMO.

Orodha hii ilianza kutumiwa mwaka 1979. Kabla ya hapo, jina la kimbunga Fern lilibadilishwa mwaka 1966 na badala yake kukatumiwa Frieda. Hakuna sababu iliyotolewa.
Majina yanavyoacha kutumiwa

Baadhi ya majina huacha kutumiwa, sana kunapotokea uharibifu mkubwa au hasara kubwa hivi kwamba kutumia tena jina hilo kutafufua kumbukumbu zenye uchungu.

Mfano ni kimbunga Katrina kilichoua watu 2,000 mwaka 2005 na kusababisha uharibifu mkubwa Marekani.

Kimbunga hicho kiliwaacha watu milioni moja bila makao. Mji wa New Orleans, Louisiana uliathirika sana.

Katika WMO kuna kundi la wataalamu liitwalo Kamati ya Vimbunga vya Tropiki ambalo hukutana kila mwaka.

Kundi hilo ndilo huamua ni majina yapi yatatumika tena na ni yapi yataacha kutumiwa.

Majina yaliyoachwa kutumiwa

Kando na Katrina, kuna majina mengine ambayo yameacha kutumiwa. Mitch, kutokana na kimbunga cha mwaka 1998 kilichoua watu 11,000 Honduras na Nicaragua, halitumiwi tena. Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kukumba maeneo ya Magharibi mwa dunia katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Kimbunga Sandy cha mwaka 2012 na Kimbunga Irene 2011 pia vilisababisha uharibifu mkubwa. Majina hayo hayatumiwi tena.

Kimbunga hatari zaidi kuwahi kukumba Marekani kilitokea 1780, ambapo kiliua watu 22,000 maeneo yaMartinique, Barbados na St Eustatius.

Wakati huo majina hayakuwa yameanza kutumiwa kurejelea vimbunga.

Majina yaliyoacha kutumiwa tangu 1954.
Majina maeneo mengine duniani

Katika maeneo mengine duniani, huwa kuna utaratibu tofauti wa kuvipa majina vimbunga.

Lakini majina yote hupitia kwa WMO.

Kwa mfano, maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Pasifiki na Bahari ya China Kusini, kuna jedwali la majina ambalo kila taifa linaloathirika huchangia.

Baada ya kimbunga kutokea, kimbunga kinachofuata hupewa jina linalofuata.

Kwa mfano, kimbunga cha kwanza huitwa Damrey (kimbunga cha kwanza Cambondia) na kitakachofuata kinafaa kuitwa Kaikui (jina la kwanza China).

Kimbunga cha sasa maeneo hayo ni Chaba (jina la nafasi ya nne Thailand).

Kilichotokea majuzi kiliitwa Megi na ambacho kiliathiri maeneo ya China na Taiwan. Jina hilo ni la nafasi ya nne chini ya majina ya Korea Kusini.
Majina ya vimbunga na tufani yalianza kutumiwa Uingereza na Ireland, kwa majaribio.

Kuna jina kwa kila alfabeti, isipokuwa Q, U, X, Y na Z, ambao ndio utaratibu unaotumiwa kuvipa majina vimbunga Atlantiki Kaskazini.
CHANZO - BBC
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...