Saturday, April 13, 2019
Hizi Ndio Sababu Zinazowafanya Wanaume Kufa Mapema Kabla ya Wanawake
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume wengi walioko kwenye ndoa wanakufa mapema na kuwaacha wake zao, ingawa swali linabaki kuwa ni kwanini?
Zifuatazo ni sababu 5 za wanaume wengi walioko kwenye ndoa kufa mapema na kuwaacha wake zao.
1. Ugumu katika kufunguka.
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia
mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza.
2. Ugumu katika kusamehe.
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote.
Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sana kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.
3. Tabia hatarishi.
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao
waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.
4. Ugumu katika kujali afya.
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo.
Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.
5. Msongo wa mawazo.
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo "stress" ingawa kwa nje wanajitahidi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa
moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.
Kuwa open, roho safi and less agressive.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
