Monday, April 29, 2019

IGP Sirro atoa maagizo kwa RPC Iringa


Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amemuagiza kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire, kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa Jeshi hilo unakamilika ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

IGP Sirro amesema kuwa kukamilika kwa nyumba hizo zilizotokana na fedha zilizotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, zitasaidia kukabiliana na changamoto ya makazi.

Aidha, IGP Sirro, ameipongeza kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Iringa kwa kuendelea kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inazidi kuimarika katika mkoa huo huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi, ubakaji pamoja na kujihusisha na wizi wa kutumia pikipiki.

Hiki Hapa Kikosi cha Yanga Dhidi ya Azam Uwanja wa Uhuru Leo

KIKOSI cha Yanga kitakachoanza leo dhidi ya Azam FC uwanja wa Uhuru



kikosi cha kwanza

1. Klaus Kindoki
2. Paul Godfrey
3. Andrew Vincent
4.Gadiel Michael
5.Abdallah Shaibu
6.Feisal Salimu
7. Mrisho Ngasa
8. Mohamed Banka
9.Heritier Makambo
10.Ibrahim Ajibu
11.Raphael Daud

Kikosi cha akiba

1. Ramadhan Kabwili
2. Juma Abdul
3. Said Makapu
4. Jaffary Mohamed
5. Pappy Tshishimbi
6. Amiss Tambwe
7. Haruna Moshi
Source

Mwanamitindo adondoka jukwaani na kufariki akiwa kwenye onyesho (Video)

Mwanamitindo wa kiume, Tales Soares (26) amefariki dunia baada ya kuanguka jukwaani wakati akitembea kwa mwendo wa maringo (catwalk) alipokuwa akishiriki kwenye wiki ya mitindo mjini São Paulo, nchini Brazil. Soares alipoanguka, watazamaji walidhani ni sehemu ya onesho lake. Mwanamitindo huyo alipatiwa huduma ya kwanza na kufaliki muda mfupi baadae wakati akipelekwa hospitali. Kampuni ambayo …

The post Mwanamitindo adondoka jukwaani na kufariki akiwa kwenye onyesho (Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Maendeleo hayana chama, hata CHADEMA watapita - Rais Magufuli


Rais John Magufuli ameendelea kusistiza kuwa maendeleo ya nchi hayana chama ingawa anaamini maendeleo ya uhakika yanaletwa na kiongozi kutoka CCM.

Ameeeleza hayo akiwa katika ziara yake mkoani Mbeya ambapo leo anatarajiwa kufungua kuaweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Katumba – Mbambo – Tukuyu na ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Kikusya – Matema.

"Maendeleo haya chama, sisi wote tunahitaji maendeleo, lakini nina uhakika maendeleo ya kweli na kiongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi ambaye atawajibika kuwatumikia Watanzania wote, tumechelewa,

Ameendelea kwa kusema, "Tukitengeneza barabara hata CHADEMA watapita, nashangaa hapa hakuna hata kituo cha mabasi, yaani niwe mbunge wa hapa nishindwe kusema eneo hili liwe kituo cha mabasi watu wafanye biashara".

Serikali Kuendelea Kulinda Uhuru wa Kuabudu

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa Katiba huku akiwapongeza Watanzania namna wanavyotumia uhuru huo bila kuuvunja.

Pia ameahidi kuwa Serikali itandelea kushirikiana na dini pamoja na madhehebu yote kwa sababu ni taasisi nyeti na muhimu katika jamii kwa sababu zinasaidia kuwafanya wananchi kuwa raia wema.

Ameyasema hayo  jana Aprili 28, 2019 katika misa ya kumsimika Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa kanisa katoliki Jimbo Kuu la Mbeya iliyofanyika katika viwanja vya Sokoine na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Alisema amefurahi kuona katika misa ya kumsimika askofu Nyaisonga kuhudhuriwa na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali huku akiamini pia wahudhuriaji ni kutoka sehemu tofauti.



Source

Mwinyi Zahera Aitwa na Takukuru

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imewataka wadau wote wa michezo akiwemo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwasilisha malalamiko yao licha ya taasisi hiyo kuwatuma maofisa wake kufuatilia yanayoendelea kwenye Ligi Kuu Bara.



Takukuru wametoa kauli hiyo kufuatia hivi sasa wadau wengi wa soka kulalamika juu ya uwepo wa rushwa michezoni katika kuzihujumu timu kwenye mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara. Zahera mara kwa mara amekuwa akilalamika juu ya baadhi ya timu kutumia vibaya fedha zao katika kuzihujumu timu nyingine.



Akizungumza na Championi Jumamosi, Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, alisema kuwa kwa upande wao tayari vijana wao wapo kazini kufuatilia kila kitu kinachotokea katika ligi kuu kupitia timu shiriki huku akiwataka wadau akiwemo Zahera kuwapelekea malalamiko yao ili waweze kuyafanyia kazi.



"Ni kweli hizo taarifa zimetufikia lakini kitu kinachotusikitisha sana kutoka kwa wananchi (wadau) ni kwamba mambo yanaongelewa na watu lakini wahusika wanaoguswa na hayo mambo hawaji kutupa taarifa kwa ufasaha yaani kutupa kamili, nini kimetokea, nani kafanya nini wakati gani na wapi.



"Sasa tuna taarifa lakini ni za kuungaunga mno, sisi tungependa hao watu wanaolalamika waje watueleze, nani kachukua rushwa, wakati gani na wapi, sisi tunaingia kazini yaani tupo tayari, tumepata habari nusunusu vijana wetu wemekwenda kufanya uchunguzi lakini inakuwa vyema kama tunapata taarifa ambazo zimejitosheleza kwa sababu inatusaidia kuanza na tatizo kuliko kusubiria," alisema Mbungo.

TUMESHUSHA BEI ZA TV, JIPATIE TV ORIGINAL KWA BEI POA. DAR USAFIRI BURE


Hii ni habari njema kwa wale wote wanaohitaji Tv Origianl kwa bei ya Punguzo. Bongo Deco tumewaletea ofa hii ya nguvu, tupigie 0658184797 na 0752 18 4797 tunapatikana kinondoni mwanamboka pembeni kabisa ya kituo cha mwendokasi mwanamboka. SHUKA HADI MWISHO WA POST HII KUONA BEI ZOTE ZA TV


Kwa wale watakaohitaji Tv na wapo mkoani basi tunaweza watumia hadi mkoani kwa gharama nafuu zaidi, ambapo mteja atalipia gharama ya usafirishaji au kama mteja ana ndugu Dar anaweza mtuma Dukani akaja.

OFA HI SIO KWA TV ZOTE NI BAADHI TU

Kwa Dar ukinunua tunakuletea na kukufungia ukutani BURE. Warranty ni mwaka 1. Piga 0658184797 au 0752184797. Tupo Kinondoni Mwanamboka pembeni ya kiituo cha mwendokas upande magari yanapotoka Moroco
 
STAR X LED
24inch 300,000 (OFA)
32inch 430,000 (OFA)
43inch 700,000 (OFA)
50inch 950,000
STAR X LED SMART TV
32inch 480,000 (OFA)
43inch 800,000 (OFA)
50inch 1,050,000
55 inch 4k  1,250,000
65inch 4k  2,100,000
PHILIPS 32
480,000
PINETECH
32 smart 480000 (OFA)
55  smart 1,250,000
TCL LED SMART TV
Tcl 32" - 500,000 (OFA)
Tcl 40" - 750,000 (OFA)
Tcl 43" - 850,000 (OFA)
Tcl 49" - 1,200,000 (OFA)
Tcl 55" - 1,550,000 (OFA)
Tcl 55" 4k - 1,600,000
Tcl. 65" - 3,000,000
LG LED TV's (Sio smart)
24"- 380,000
32" - 500,000 (OFA)
43" - 900,000 (OFA)

LG LED SMART TV
32 = 630,000 (OFA)
43  =1,000,000 (OFA)
43 4K  UHD =1,250,000 OFA
49 4k  UHD =1,650,000 OFA
55 UHD =2,250,000  OFA
55 = 1,700,000 OFA
65 UJ651V  UHD =3,600,000
SAMSUNG LED TV's
32 - 540,000 (OFA)
40 - 890,000 (OFA)
49 - 1,400,000
SAMSUNG SMART TV
40 - 1,150,000
43 4k - 1,350,000
49 4k - 1,750,000
55 4k – 2,350,000

SAMSUNG CURVE SMART TV 
49inch 4K   - 1,700,000
55inch 4K UHD  -2,350,000 (OFA)
65inch 4K UHD ) - 3,700,000 (OFA)

BOSS TV
Boss 32" @400,000 (OFA)
Boss 40" @680,000 (OFA)
BOSS SMART TV
43" @800,000(OFA)
49" @950,000 (OFA)
55 @ 1,200,000 (ofa)
HISENSE LED Tv
32"  580,000
39"  900,000
43"  1,200,000
50"  1,450,000
55"  1,950,000
58"  2,120,000
HISENSE FULL HD SMART TV
32'' 800,000
43'' 1,400,000
49'' 1,600,000
50'' 1,990,000  
 
HISENSE TV SMART 4K ULTRA
50" 2,050,000
55" 2,350,000
58" 3,000,000
65" 3,750,000
HISENSE CURVED TV
55 Curved TV 3,950,000
SONY 32 INCH => 650,000
EVVOLI LED TV 
32" EV300S Smart @ 485,000
43" EV100 @ 720,000 0FA
43" EV300S Smart @ 790,000 OFA
49" EV600US 4K Smart @ 1,350,000
55" EV800US 4K Smart @ 1,790,000
65" EV600US 4K Smart'  @ 2,700,000
 








 
 

Ratiba ya leo Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL)


Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) inatarajiwa kutimua vumbi tena leo ambapo Azam FC itavaana na Yanga SC. Chini ni ratiba ya michezo ya leo iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


Source

Kufanya Mapenzi Mara kwa Mara Kunaboresha Afya yako



Kufanya mapenzi ni mojawapo ya vitu vichache ambavyo watafiti wanasema vinamfanya mtu aburudike huku mwili wake ukifaidika kutokana na tendo hilo.

Utafiti umeonyesha kwamba kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kunatibu mafua, kuepusha magonjwa ya moyo, kunazuia kansa na hata kuongeza urefu wa maisha.

Watafiti katika chuo kikuu cha Nottingham University nchini Uingereza wamegundua kwamba wanaume wenye umri zaidi ya miaka 50 wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara wana uwezekano mdogo sana wa kupata kansa ya kibofu.

Watafiti hao walikanusha madai kwamba kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara 20 kwa mwezi kunaongeza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo.

Madaktari wamekubaliana kwamba mapenzi ni kama shughuli zingine za kawaida na ni mazoezi bora kwa afya.

"Kwa kulinganisha na mazoezi, kufanya mapenzi ni sawa na kutembea zaidi ya kilomita moja au kupanda na kushuka ngazi za majengo mawili marefu" alisema Dr Graham Jackson wa hospitali ya St Thomas.

Utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Queens University cha Belfast umesema kwamba kufanya mapenzi zaidi ya mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.

Tendo la ndoa pia linasaidia kulinda mifupa. Dr Sarah Brewer alisema: "kiwango cha Testosterone kimeonekana kuongezeka wakati tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa".

Utafiti huo ulibainisha kwamba kwa wanaume na wanawake ili waweze kupata faida za tendo la ndoa inawabidi wafanye tendo hilo mara kwa mara.

"Itumie au ipoteze" ndiyo ushauri uliokuwa ukitolewa kwa wazee na wanasayansi toka nchini Finland.

Pamoja na faida za tendo la ndoa ,tendo hilo pia lina hasara zake kama vile kupata magonjwa ya zinaa iwapo kinga haitatumika.

Tangia kugunduliwa kwa viagra miaka 10 iliyopita idadi ya watu wenye umri zaidi ya miaka 45 walioambukizwa magonjwa ya zinaa imeongezeka maradufu.

Profesa Lipumba Afanya Uteuzi wa Viongozi Mbalimbali CUF

Chama Cha Wananchi (CUF) kimewateuwa wanachama 13 kushika nafasi mbalimbali za uongozi ili kusaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, aliwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa, wameteua wanachama ambao miongoni mwao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

Wanachama walioteuliwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Zainab Mndolwa na naibu wake, Omar Mohammed Omar, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge na Sera, Mohammed Habibu Mnyaa na naibu wake, Mohammed Ngulangwa.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke Jafar na naibu wake, Mohammed Vuai Makame, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma, Abdul Kambaya na naibu wake, Mbarouk Seif Salim.

Wengine ni Haroub Mohammed Shamis aliyeteuliwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria, naibu wake Salvatory Magafu wakati Thinney Juma Mohammed akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mafunzo na Uhamasishaji na naibu wake, Masoud Omary Mhina.
 

Profesa Lipumba alisema Kamati ya Uongozi imemteua Yusuph Mohammed Mbugiro kuwa Ofisa Tawala wa ofisi kuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo wa CUF pia amefanya uteuzi wa viongozi wa jumuiya za chama huku akisema viongozi hao watakaimu nafasi zao mpaka pale watakapochaguliwa kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali ameteuliwa kuwa kaimu mwenyekiti Jumuiya ya Vijana wa CUF (Juvicuf), makamu wake Faki Suleiman Khatib na kaimu Katibu Mtendaji, Yusuph Kaiza Makame na naibu wake, Mbaraka Chilumba.

Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (Jukecuf) ni Dhifaa Mohammed Bakar na makamu wake ni Kiza Mayeye, kaimu Katibu Mtendaji ni Anna Ryoba na naibu wake ni Leila Jabir Haji.

Kwa upande wa Jumuiya ya Wazee wa Cuf (Juzecuf), kaimu mwenyekiti ni Mzee Chunga na makamu wake ni Hamida Abdallah, kaimu katibu mtendaji ni Hamis Makapa na naibu wake ni Said Ali Salim.


Iran: Marekani lazima iombe idhini kwa jeshi la Iran la SEPAH kuweza kupita Hormuz

Mkuu wa Majeshi ya Iran amesema kuwa meli za Marekani haziwezi kupita katika Lango Bahari la Hormuz bila ya kuomba idhini kwanza kutoka kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Meja Jenerali Mohammad Baqeri amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea hadi hivi sasa kuhusu meli za kivita, za kibiashara na za mafuta na vyombo vyote vya majini vya Marekani vinavyopita kwenye Lango Bahari la Hormuz. 

Wakati wowote vinapoamua kufanya hivyo lazima viombe idhini kwanza kutoka kwa jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ndipo vinaweza kupita baada ya kuruhusiwa na jeshi hilo.
 
Amesema Iran inataka lango hilo libakie wazi na salama na kuonya kuwa Tehran haitoruhusu mtu yeyote kuhatarisha usalama wa eneo hilo. 

Itakumbukuwa kuwa karibu thuluthi nzima ya mafuta yanayotumika maeneo mbalimbali duniani yanapitia katika Lango Bahari la Hormuz la nchini Iran. 

Jukumu la kulinda usalama wa eneo hilo muhimu mno kiistratijia ni la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ambalo hivi karibuni rais wa Marekani Donald Trump alidai kuwa  jeshi hilo ni taasisi ya kigaidi.

Mkuu huyo wa vikosi vya ulinzi vya Iran ameongeza kuwa, madhali meli za nchi nyingine zinatumia lango hilo kusafirisha mafuta, Iran nayo ni haki yake kabisa kutumia eneo lake hilo kusafirishia mafuta. 

Hata hivyo amesema hii haina maana kwamba Iran inakusudia kulifunga lango hilo. 

Amesema: "Hatuna nia ya kulifunga Lango Bahari la Horumuz isipokuwa kama adui atatulazimisha kufanya hivyo. Na tukiamua kulifunga, basi tunao uwezo wa kufanya hivyo muda wowote ule."

Credit: Parstoday


Rais Magufuli kuzindua kiwanda cha maparachichi leo


Rais John Magufuli leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya ambapo atafungua kiwanda cha maparachichi wilayani Rungwe, mkoani humo.

Pia ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Katumba – Mbambo – Tukuyu na ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Kikusya – Matema.

Hapo jana akiwa mkoani humo, Rais John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli walishhiriki ibada ya kusimikwa kwa Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Mkoa wa Mbeya.

RAIS MAGUFULI: NILITAMANI KUWA ASKOFU, SIJUI NINI KILITOKEA NIKASHINDWA KUWA HATA KATEKISTA


Rais  Magufuli amesema alipokuwa mdogo alitamani kuwa Askofu lakini hajui ni nini kilitokea akashindwa kuingia katika njia hiyo.

Akizungumza katika ibada ya kuzindua Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Mbeya na kumsimika Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga, Rais Magufuli amesema anashanga hadi sasa pamoja na matamanio yake hayo ameshindwa kuwa hata Katekista au Mwenyekiti wa jumuiya.

"Nilitamani sana kuwa Askofu lakini sijui ni nini kilitokea nikashindwa kuwa hata Katekista lakini au hata mwenyekiti wa Jumuiya.

"Leo nimefurahi na ninawaonea wivu Maaskofu, nilitamani niwe huko lakini niko huku, mlioko huko msitoke ni pazuri, sasa hivi niko huku na bado natamani kuja huko," amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia aliwakumbusha Maaskofu kuhusu wito wa kazi ya uaskofu kupitia Kitabu cha Biblia cha 1Timotheo 3:1 unaosema "Ni neno la kuaminiwa mtu akitaka kazi ya Askofu atamani kazi njema."

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Polycarp Kadinali Pengo, amelitaka Kanisa kutimiza wajibu wake wa kuwasimamia waumini kiroho bila kusahau kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuweka mazinga mazuri ya kiutawala.

"Tunahitaji uwepo wa roho mtakatifu katika kuboresha mazingira ya waumini ambao wanatambua vyema wajibu wao katika kuwaongoza vyema waumini, serikali ndiyo inayoweza kulifanya hili katika upeo mpana wa kiutawala, ili roho mtakatifu aweze kutenda kazi tunahitaji kuwa na kanisa linaloshirikiana vyema na serikali," amesema Kadinali Pengo.


Sunday, April 28, 2019

Ushauri: Nina Naumbile Madogo ya Uume (Kibamia), Naogopa Kutembea na Wasichana



Amakweli mungu hakunyimi vyoote na haupi vyoote pia. Mimi ni kijana wa miaka 21, mwembamba kiasi nina body naturaly,maji ya kunde, mrefu wastani sio handsam sana but mtanashati najiheshimu, mstaarabu kutokana na sifa nilizo kuwa nazo imepelejea kupendwa sana na wanawake.
Wengine hupigana na kupelekana hadi polisi kwajili yangu pasipo mimi kuwa na mahusiano nao yani ni wivu tu na nimetongozwa na wanawake tangu nikiwa na miaka 15 na wengine ni wakubwa kwangu na wengine wanakuja hadi mbele ya mama na kueleza hisia zao kwangu ila mimi sina mpango nao kabisa yani.

Hii inapelekea hadi mama yangu kupoteza imani na mimi kwa kuhisi huenda mwanae ni shoga ama sifanyi kazi kama dume.Ila mimi sio kama siwatamani au siwataki ila nina tatizo moja linalonifanya mpaka nishindwe kujielewa wakati mwingine najipiga ukutani kwa hasira, but nashindwa nifanye nini.
Ninawaza sijui nimwambie mama yangu au baba yangu ila nawaza nitaanza je kuwaambia tatizo langu ikiwa baba ni mkali sana na mda mwingine hataki hata salamu na katika familia walio nitangulia kuzaliwa ni wanawake wote daaaah.! inaumasana ninapo muona mamayangu akitoa chozi pindi akiwa na waschana Wanaokuja mbele yake kwaajili yangu.

Pia hii imenifanya nishindwe hata kutembea mtaani kwa kuhisiwa mimi ni shoga ila tatizo langu sio kabisa yani daah..! Nawaza nitafanya vipi mapenzi na msichana ikiwa mimi nina UUME MDOGO saana nilipo upima kwa rula ni wa nchi 4 so hivi msichana yeyote anaweza kuhisi uume huu kweli daaah..
Why mimi waungwana naombeni msaada ni nini nifanye nimwambie mama akamueleze baba labda atanisaidia kupata dawa au kama kuna dawa ni wapi napata na ni ipi coz naona ninakoelekea sio kabisa.

Naombeni msaada naombeni

Naibu Waziri wa Maji AWESO kuelekea Aweso Cup: Ukizingua nakuzingua (Video)

Naibu Waziri wa Maji Jumaa AWESO amedai mashindano ya Aweso Cup ambayo yatafanyika siku ya kesho Mkoani Tanga, yataenda sambamba na kauli mbiu ya kuwataka makandarasi wa maji kufanya kazi bila kuisababishia serikali hasara.

The post Naibu Waziri wa Maji AWESO kuelekea Aweso Cup: Ukizingua nakuzingua (Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Saturday, April 27, 2019

Familia ya Ruge Mutahaba yafanya misa ya shukrani


Siku ya leo familia ya RugeMutahaba ilikuwa na misa ya shukrani katika kanisa la St. Martha, Mikocheni ambapo ndugu, jamaa na marafiki waliweza kuhudhuria katika misa hiyo.

Ruge Mutahaba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group (CMG) alifariki Februari mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo.


Source

Baba Mzazi Wa Emiliano Sala Afariki Dunia

Baba Mzazi Wa Emiliano Sala Afariki Dunia
Majonzi yameikumba tena familia ya mchezaji Emiliano Sala aliyefariki miezi mitatu iliyopita baada ya baba mzazi wa mchezaji huyo Horacio Sala kufariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 58 katika mji wa Progreso nchini Argentina.

Baba huyo mzazi wa Emiliano amekuwa kwenye matibabu ya moyo kwa kuwa hakuwahi kuamini kama mwanaye amefariki japo alikuwa ni sehemu ya maziko ya kijana wake aliyefariki akiwa na miaka 28.

Emiliano Sala aliyekuwa akiitumikia Nantes FC alifariki kwa ajali ya ndege alipokuwa akitoka Ufaransa kwenda England kujiunga na timu yake mpya Cardif City.

Friday, April 26, 2019

Fahamu kuhusu kilimo cha Mihogo

 
Utangulizi
Leo nimekuandalia makala hii ya kilimo cha mihogo. Kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame kipindi hiki ni muafaka kabisa kwa maandalizi na upembuzi juu ya kilimo cha mihogo kwa msimu ujao wa mvua za vuli. Natumai katika makala hii utajifunza mambo yote muhimu unayohitaji kujua kuhusu muhogo. Karibu…
Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania, zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya mihogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k.
Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini mihogo ni chakula kikuu ambacho kinachuku asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kwa siku za karibuni, muhogo unaongoza kwa kuongezeka katika umaarufu kuliko mazao yote ya chakula nchini. Watalaam wanazungumzia umaarufu wa muhogo kuwa ni (pamoja na mambo mengine) uwezo wake wa kustahamili hali ya hewambaya kama ukame na mvua zisizoaminika, kutoa mazao mengi kwa eneo na kustahamili mashambulizi ya magonjwa na wadudu.
Hata hivyo uzalishaji wa mihogo kwa eneo bado ni wa viwango vya chini mno. Zipo sababu nyingi zinazo sababisha kuwepo kwa hali hii kama vile:
  • Ukosefu wa mbegu bora za mihogo za kutosha 
  • Wakulima kuendelea kungangania mbegu zao za asili kuliko mbegu bora licha ya uzalishaji mdogo na kushambuliwa na magonjwa na wadudu.
  • Ukosefu wa masoko ya kuaminika ambayo yangeshawishi wakulima kulima mbegu za kisasa ambazo zimeandaliwa kibiashara. 
  • Wakulima wengi kutotumia teknolojia sahihi za usindikaji ambazo ni mbinu mbadala za hifadhi za asili. 
Kwa muda mrefu tatizo kubwa la zao la muhogo ni ukosefu wa teknolojia ambazo zina uwezo wa kuongeza thamani wa muhogo kama chakula chenye ubora kwa familia za mijini na vijijini.
Vikundi mbalimbali vya uzalishaji na usindikaji vimeundwa na muhogo umeanza kuthaminwa kwani unga wake unatumika kutengenezea vyakula kama maandazi, chapati, chichili, keki na vingenevyo vingi.
Ugali wa muhogo umeongezeka thamani kutokana na ubora wa unga uliosindikwa kwa kwa teknolojia ya kisasa.
Madhumuni ya Mogriculture Tz kutoa makala hii ni kutoa maelekezo juu kilimo bora cha zao la muhogo ili kusaidia wakulima kuinua viwango vya ubora na wingi wa mazao hivyo kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea kipato.


Umuhimu na Matumizi ya Muhogo
  • Muhogo ama (kitaalam) Manihot esculentum, ni muhimu sana kwa Tanzania kutokana na sifa zake za kuvumilia ukame, kustawi kwenye maeneo yenye rutuba kidogo hivyo kuhitaji gharama ndogo za uzalishaji. Kwa hali hiyo, zao hili hulimwa sana na wakulima wadogo walio wengi wenye kipato kidogo.
  • Kwa wakazi wa vijijini, muhogo huvunwa, kutolewa ganda la juu na kuanikwa hadi kukauka maarufu kama makopa. Kwa kawaida makopa hutwangwa kwenye kinu na kupata unga ambao hutumika kama uji au ugali. Makopa mara nyingi hutunwa ama kuhifadhiwa kwenye dari ya nyumba ambako hufukiziwa moshi wa moto ili yasipukuswe. 
  • Kutokana na hali hiyo, wakulima wengi hulima muhogo mchungu ambao haupukuswi kwa urahisi. Kwa vile muhogo mchungu una sumu nyingi aina ya cyanide, hufanya kiasi kidogo cha muhogo kiliwe kwa kutafuna ukiwa mbichi ama kupikwa kama futari. 
  • Kwa wakazi wa mijini, sehemu kubwa ya mihogo hutumika kama futari au kitafunwa kwa chai ama humenywa na kukaangwa kama chips maarufu kama chips dume. 
  • Kutokana na kuongezeka kwa teknolojia za usindikaji, unga wa muhogo hutumika kutengenezea biskuti, chapati,maandazi,chichili,keki na vyakula vingine vingi vinavyotengenezwa kwa kutumia unga wa ngano.
chipsi za muhogo

Mazingira na Aina za Mihogo
Mazingira yanayofaa
Muhogo ni zao la jamii ya mizizi. Hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye mwinuko wa mita 0 hadi 1500 toka usawa wa bahari. Zao hili hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa milimita 750 mpaka milimita 1200 kwa mwaka.
Muhogo hupendelea udongo wa kichanga usiotuamisha maji. Udongo wa kichanga husaidia mizizi kupenya kwa urahisi na kupevuka. Vile vile muhogo una sifa ya kuvumilia hali ya ukame wa muda mrefu.
Aina za Mihogo
Kuna zaidi ya aina 45 za mihogo zinajulikana nchini Tanzania. Zaidi ya asilimia 80 ya mihogo ni ya asili. Hivyo ni kusema wakulima wengi hawatumii mbegu bora.
Wakulima wengi pia hupendelea kulima mihogo michungu kwa sababu haishambuliwi sana na wadudu ama magonjwa shambani na makopa yake yanahifadhika kwa urahisi. Hata hivyo zaidi ya asilimia 70 ya mihogo yote inayolimwa Tanzania ni mihogo baridi.

Kuandaa shamba la Muhogo
Inashauriwa kuandaa shamba mapema kabla ya msimu wa mvua haujaanza. Zifuatazo ni hatua za msingi katika kuandaa shamba:
  • Kufyeka msitu au vichaka 
  • Kung'oa na kuchoma moto visiki 
  • kulima na kutengeneza matuta. 

Uchaguzi wa mbegu bora za mihogo
Mpaka sasa hivi kuna aina nyingi sana za mbegu bora za mihogo ambazo zimethibitishwa na tayari zinatumiwa na wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
Katika kuchagua mbegu inayofaa, pamoja na mambo mengine, zingatia yafuatayo:
  • Mbegu itokane na shina lililokomaa vizuri 
  • Isitokane na shina la muhogo ulioshambuliwa na magonjwa. 
  • Macho yake yasiwe yamekaribiana sana au kuachana sana

Upandaji wa Mihogo
Muda wa kupanda Mihogo
  • Kanda ya ziwa: December mpaka January mwishoni
  • Nyanda za juu Kusini: November mwanzoni na Kanda ya Mashariki: kuanzia October mpaka December
Urefu wa kipande cha shina cha muhogo
Baada ya kuchagua mbegu hatua inayofuata ni kukata shina lako la muhogo katika pingili ndogo ndogo tayari kwa kupanda. Inapendekezwa pingili ziwe na urefu wa sentimita 30.
Hata hivyo, urefu wa pingili utategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande. Inapendekezwa kipande kimoja kiwe na macho manne hadi sita.
Nafasi ya kupanda Muhogo
Nafasi ya kupanda kwa shamba linalokusudiwa liwe na muhogo mtupu ni mita moja toka shina hadi shina na mita moja kati ya mistari. Kwa shamba ambalo mkulima anakusudia kuchanganya mazao, inashauriwa nafasi ya kupanda iwe mita 2 hadi mita 4 (kwa kutegemea aina ya mazao yanayochanganywa) kati ya mistari na mita moja toka shina hadi shina.
Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
  • Kulaza ardhini (Horizontal)
  • Kusimamisha wima (Vertical) na
  • Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Kudhibiti Magugu
Katika miezi minne ya mwanzo muhogo unahitaji kupata chakula cha kutosha na mahitaji mengine ya msingi ili uweze kukua na kujenga mizizi mikubwa na imara.  Hivyo inashauriwa kufanya palizi la kwanza mapema, angalau mwezi mmoja baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua za mwanzo kunyesha.
Kwa kawaida palizi hufanywa kwa kutumia jembe la mkono au dawa ya kuulia magugu. Njia nyingine ya kudhibiti magugu ni kupanda mimea yenye majani yanayotanda juu ya udongo.
Palizi kwa kawaida hufanywa kila inapoonekana kwamba magugu yameota kiasi cha kuathiri ustawi wa muhogo, hivyo unaweza kupalilia mara 3 au 4 zaidi baada ya palizi ya kwanza hadi muhogo kukomaa.

Kuchanganya mazao kwenye shamba la mihogo
Utafiti unaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 80 ya mashamba ya muhogo Tanzania yanachanganywa na mazao mengine. Sababu kubwa zinazotolewa kuhusiana na hali ni kwamba wakulima wanafaidika kwa kupata mavuno ya ziada kama kunde, karanga, mahindi, maharage, korosho ama njugu.
Kwa kuchanganya mazao, mkulima, licha ya kuimarisha uhakika na usalama wa chakula, anaweza kuuza mazao mchanganyiko na kujiongezea kipato. Vile vile mazao ya jamii ya mikunde yanasaidia kuongeza rutuba ya udongo.
Hata hivyo, mazao mchanganyiko ni budi yasilete ushindani na muhogo katika kujipatia chakula, hewa, mwanga, unyevu na mahitaji mengine ya mmea yanayoweza kuathiri ustawi wa muhogo.
Inashauriwa pia kuzingatia muda wa kupanda, yaani muhogo upandwe mvua za kwanza ili mazao mchanganyiko yasiweze kuzidi na kuutawala muhogo.

Jinsi ya kudhibiti Wadudu na Magonjwa

Uvunaji wa Muhogo
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua. Mihogo hutoa mavuno ya tani 19 hadi 30 kwa hekta kutegemeana na aina ya mbegu (variety) iliyopandwa.
Uvunaji wa muhogo
Uvunaji wa Muhogo

Usindikaji bora wa Muhogo
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu tatu:
  • Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji 
  • Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo 
  • Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe. 
Njia bora za usindikaji Muhogo
  • Kwa kutumia mashine aina ya Grater 
Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho "presser" ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
  • Kwa kutumia mashine aina ya chipper 
Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.
Matumizi ya Muhogo
  • Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga 
  • Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k. 
  • Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga. 
Ni matumaini yangu kuwa umejifunza mambo mengi mazuri kuhusu kilimo cha muhogo, sasa tumia angalau dakika mbili tu kutupatia mrejesho kwa kuandika comment yako hapa chini.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...