Wednesday, March 6, 2019
Serikali yakasirishwa na tabia ya uongozi wa juu wa mgodi wa Acacia North Mara
Na Issa Mtuwa – Wizara ya Madini Tarime
Waziri wa madini Mhe. Doto Biteko ameonyesha kukerwa na tabia zinazofanywa na uongozi wa juu wa mgodi wa Acacia North Mara kwa serikali kwa kushindwa kuhudhuria vikao mbalimbali vinavyo andaliwa baina ya pande hizo mbili, licha ya baadhi ya vikao kuongozwa na Waziri wa Madini lakini viongozi wa juu wa mgodi ambao ndio wafanya maamuzi na watekelezaji wa maagizo ya serikali wamekuwa wakishindwa kuhudhuria .
Biteko amesema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara jana Machi 5, 2019 katika kijiji cha Nyamongo wilayani Tarime ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi kwenye migodi ya North Mara na Buhemba. Biteko amesema anakerwa na tabia za uongozi wa mgodi huo kwa kushindwa kuhudhuria mara kwa mara mikutano mbalimbali ya ndani na ile ya hadhara badala yake wamekuwa wakituma wawakilishi.
" Kuanzia leo, haki ya mungu, haki ya mungu, haki ya mungu, mimi Waziri wa Madini leo ni siku ya mwisho kukaa na hawa wawakilishi kwenye vikao, hasa kama hivi vinavyo husu hatima ya maisha ya watu alafu wafanya maamuzi hawahudhurii. Niwambie ukweli nasikitishwa sana na tabia hii. Hawa walipo sio saizi yangu, kama ni hawa hata mimi ningewaleta maafisa wa wizara tena wale wanaolingana na hawa.
Wanataka wawepo hadi afike Rais…!? nendeni mkawambie kwenye ngazi ya Wizara mimi ndio wamwisho katika kufanya maamuzi, kama mimi nipo kwa nini wao wasiwepoo…!? nyinyi mliokuja hapa nendeni mkawaambie hii ni mara ya mwisho wasifikiri serikali hii wanaweza kuiweka mfukoni, haikubaliki, hii tabia lazima ifike mwisho" alisema Biteko huku akisikitika sana.
Amesema kwa ujumla hafurahishwi na namna mambo yanavyokwenda mgodini hapo ukilinganisha na migodi mingine. Mgodi wa North Mara umezungukwa na matatizo mengi sana yakiwemo ya malipo yafidiaza wananchi, utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya wananchi.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
NA REBECA DUWE TANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Burian amewataka wananchi wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya ndoa na ardhi ...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
