Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Ibrahim Hassan (7) amefariki Dunia baada ya kukanyagwa na mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Taifa jana Jumapili kwenye mchezo kati ya Taifa Stars na Uganda.
Akidhibitisha taarifa hizo, Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Temeke, Rolester Kinunda amesema kuwa jana walipokea watu 18 waliopata majeraha kwenye vurugu zilizotokea Uwanja wa Taifa na miongoni mwa majeruhi hao alikuwa ni huyo mtoto Ibrahim Hassan.
"Majeruhi wote ukiachilia aliyefariki, walipata michubuko na wengine walikuwa wakilalamika kupata maumivu ya kifua, walipimwa na kuonekana hawajaumia ndani, hivyo walipatiwa dawa za maumivu na kuruhusiwa,"amesema Kinunda.
Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke kusubiria taratibu za mazishi.
Jana kwenye mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Uganda, kulizuka vurugu ambazo zilipelekea geti la kuingilia kuvunjwa na mamia ya watu kukanyagana.
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...