Waislamu mjini Xinjiang nchini China walilazimishwa kula nyama ya nguruwe na kutumia vileo kwenye sherehe za mwaka mpya wa jadi wa China.
Kwa ushuhuda uliotolewa na wakazi wa Ili Kazakh mjini Xinjiang, wamesema kuwa siku ya kilele cha siku hiyo, walialikwa kama desturi ya Wachina wanaposherehekea na kuamliwa kula kitimoto na kunywa pombe.
Kwa mujibu wa kituo cha Radio Free Asia, kimeripoti kuwa mamlaka za mji huo unaokaliwa na takribani waislamu milioni 10, ziliwataka waislamu kusherehekea kwa nguvu sherehe hizo, ambazo zinapingana na imani ya dini ya Kiislamu .
Kituo hicho cha Radio, kimeripoti kuwa Mamlaka zilipitia kila nyumba na kuwataka washerehekee kwa kula na kunywa pombe, la sivyo watachukuliwa hatua kali ikiwemo kutupwa jela.
Pombe na nyama ya kitimoto ni vitu ambavyo haviruhusiwi kutumiwa na Waislamu, na ndio maana ya Waislamu nchini China wanapinga kusherehekea sikukuu hiyo, ambayo ni kubwa na ni maarufu zaidi nchini humo kama ilivyokuwa sikukuu ya Kristmasi kwa Wakristo.
"Watu wa Khazan, hawajawahi kula kitimoto, hata mwaka jana tulitishiwa na baadhi yetu walichukuliwa na polisi kwa kugoma kusherehekea sikukuu ya mwaka wa China. Sisi hapa tunajua sikukuu zetu ni Eid al-Fitr na Eid al-Adha hizo nyingine hatuwezi kusherehekea hata kwa nguvu,"amesema mkazi wa Khazan mjini Xinjiang .
Serikali ya China katika Jimbo hilo, imekuwa ikitoa masharti magumu kwa waislamu wanaoishi jimbo hilo.
Mwaka 2017, Serikali ilipiga marufuku wanaume Waislamu kufuga ndevu ndefu na wanawake kuvaa hijab mjini Xinjiang linalokaliwa na Waislamu milioni 10.
Mwaka 2015, China ilizuia Waislamu wa Xinjiang kutofunga mwezi wa Ramadhan kwa kuhofia nguvu kazi ya taifa kupungua.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
