Sunday, February 3, 2019
NDOA Yangu Imekuwa Chungu..Ndugu wa Mume Wamezidi, Nishauri Nifanyeje?
Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi Nyanda za juu kusini. Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa, yaani ndio star kwao.
Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza.
Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo. Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimo na hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe.
Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisa.
Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii. Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasa na ninaomba ushauri wenu ndugu ; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home.
Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hivi ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani.
Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu.
Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!
Msaada jamani!
Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress
By Sisame
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...