Wednesday, February 20, 2019
Mbinu za kuongeza mauzo katika Biashara
Yapo mambo ya msingi ambayo mfanyabiashara yeyote yule ili aweze kukua katika biashara yake ni lazima ayafahamu, na mambo hayo si mengine bali ni jinsi gani anatakiwa kuongeza kiwango chake cha mauzo.
Na si kuongeza kiwango cha mauzo pekee, bali kuhakikisha anapata faida kubwa kwa kile anachokifanya. Wapo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa hawalizingatii hili na kupelekea bidhaa au huduma wanazozitoa kutofanya vizuri sokoni.
Kwa minajili hiyo nikaona ni vyema ili kuweza kuwasadia wafanyabiashara hao ili wapone ni vyema niandike makala haya ili ikusaidie kuweza kuongeza kiwango chako cha mauzo katika biashara unayoifanya.
Kwanza kabisa ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara ambayo unaifanya unatakiwa kuachana na mfumo wa zamani ambao ulikuwa unatumia katika kufanya biashara yako, kama inashindikana kuachana na mfumo huo wa zamani basi unachotakiwa kufanya ni kuboresha mfumo huo wa zamani ili uweze kufanikiwa kibiashara.
Jambo jingine ambalo ni muhimu kabisa ambalo unatakiwa kulikumbatia katika biashara yako ni, kuelewa mbinu za kufanya biashara ya yako kwa kutumia mitandao ya kijamii. Kwa wenzetu wazungu mfumo huu huitwa affiliate marketing, ambapo kwa kibantu tunaweza tukasema ifike mahala utengeneze mifumo thabiti, mfumo huu utakusadia kutenggeza pesa ukiwa umekaa tu nyumbani.
Wakati mwingine unaweza ukasema labda njia hii haiwezekani kuleta matokeo chanya, lakini ninachotaka kusema hakuna lisilo wezekana chini ya jua hii ni kwa sababu dunia ya sasa imekuwa kiganjani mwa wadamu, kila kitu ambacho unakitaka utakipata kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kifupi dunia ya sasa inakwenda kasi sana tofauti na ilivyokuwa nyuma.
Na ili uweze kwenda sawa na kasi hiyo ni lazima jifunze mbinu mbalimbali zitakazokusaidia kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia mitandao ya kijamii, kwani kwa sasa wanaitumia njia hiyo ndiyo ambao wanafaidi matunda ya kutumia mbinu hizo.
Jambo jingine ambalo litaweza kukusaidia kuweza kuongeza mauzo ya katika biashara unayoifanya ni kuhakikisha unakuwa mtalamu katika biashara husika. Hii mbinu muhimu sana katika kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara kwa sababu pindi utakapokuwa mtalamu au m-bobezi wa jambo hilo itakusaidia sana kuweza kuizungumzia vizuri bidhaa au huduma unayoitoa kwa mteja wako, kufanya hivyo kutamfanya mteja huyo ainunue bidhaa hiyo.
Hivyo ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara yako jifunze kuwa mtalamu katika eneo husika unalolifanya.
Jambo la mwisho ambalo ni muhimu sana litakalo kusaidia kuweza kufanya biashara yenye tija ni kuhakikisha unaimarisha vizuri upande wa huduma kwa mteja, kwa sababu ule usemi wa kwamba mfalme ni mteja hakuwepo tu, bali msemo huo upo kumanisha kweli, mteja ni mfalme pindi awapo na asipokuwapo katika eneo lako la kibiashara pia.
Ufike pahala neno mteja liwe lina maana kubwa sana katika biashara yako, yaani mfanye mteja kuwa ni sehemu ya biashara ya yako. Mfanye mteja ajisikie huru katika suala zima la kibiashara.
Mwisho nimalize kwa kusema biashara yenye tija hujengwa na vitu vitatu vya msingi ambavyo ni bidhaa au huduma nzuri+ masoko mazuri= wateja wengi.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
