Monday, November 5, 2018

WABUNGE WA CHADEMA KUAPISHWA CCM BUNGENI DODOMA


Baadhi ya wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kesho wanatarajiwa kushuhudia baadhi ya waliokuwa wabunge wake wakiapishwa kuwa wabunge wapya kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa 13 wa bunge utakaoanza kesho mjini Dodoma.

Mbunge mteule Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, na Mbunge mteule jimbo la Monduli Julius Kalanga.

Miongoni mwa wabunge watakaopishwa kesho ni aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga, ambao wote walikuwa wabunge kupitia Chama hicho na baadaye kuhamia CCM kwa nia ya kumuunga mkono Rais Magufuli.

Mbali na wabunge hao, wabunge wengine watakaoapishwa kesho kupitia mkutano huo wa 13 wa bunge ni Mbunge wa Korogwe vijijini, pamoja na Mbunge wa Liwale Zubei Kuchauka.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Spika Job Ndugai amesema mbali na kuapishwa kwao pia bunge hilo ni maalum kwa ajili ya kujadili miswada.

"Katika mkutano wa 13, pia kutakuwa na mswali na majibu ambapo kutakuwa na maswali 125 ya kawaida, madhumuni makubwa ya mkutano huo ni mawasilisho ya mpango wa nchi, ambapo waziri wa fedha atawasilisha mpango wa serikali unaokusudiwa kutekelezwa 2019/2020" amesema Spika Ndugai

Bunge linatarajiwa kuanza rasmi novemba 6 mwaka huu na kumalizika novemba 16 mwaka huu.
Chanzo - EATV
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...