Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Iringa kimesema mbunge wa chama hicho Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amezuiwa na polisi kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Iringa, Jackson Mnyawami amesema mkutano huo ulikuwa ufanyike leo, kwamba wamepokea barua ya polisi ikiwataka wasiendelee na mkutano huo.
Barua ya Novemba 21, 2018 iliyotolewa na mkuu wa polisi Wilaya ya Iringa kwenda kwa mbunge huyo inaeleza kuwa mkutano huo umezuiwa kutokana na taarifa za kiintelejensia.
"Polisi Iringa tunazo taarifa kuna kikundi cha watu wanaojiandaa kufanya fujo katika mkutano huo. Hali hiyo inaweza kuleta uvunjifu mkubwa wa amani," inaeleza sehemu ya barua hiyo.
"Hakuna askari wa kutosha kwa ajili ya kusimamia mkutano huo kwani nguvu kazi kubwa imeelekezwa katika shughuli maalum za kitaifa ya usimamizi wa mitihani ya kidato cha nne, cha pili na darasa la nne."
Mnyawani amesema wameipokea barua hiyo ya polisi ikiwa na sababu mbalimbali.
"Sababu tulizoelezwa ni za kiintelejensia kwamba kuna watu watafanya vurugu lakini pia wamesema kuwa kuna shughuli za kitaifa, ikiwa ni pamoja na mitihani inayoendelea kufanywa na wanafunzi wa kidato cha nne," amesema.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
