Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh, Jokate Mwegelo amemsaidia mama aliyejifungua watoto mapacha waliyo ungana maini kupata bima ya afya na nyumba bora ya kuishi kutoka UBA United Bank for Africa hii inakuja mara baada ya mama huyo pamoja na watoto wake kupata ruksa ya kurejea nyumbani kwao Kisarawe.
Mama huyo wa watoto mapacha Gracious na Precious Michael Mkono wamepata ruksa rasmi katika Hospitali ya Muhimbili mara baada ya kufika hapo toka tarehe 21/07/2018 kupata matibabu baada ya kujifungulia nyumbani.
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imefanikiwa kufanya upasuaji huo wa kuwatenganisha mapacha hao walioungana wakiwa chini ya miaka mitatu, ambao wamezaliwa Kisarawe mkoani Pwani, Julai 12, mwaka huu. Jumatano ya Septemba 26, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Laurence Moselu, alisema upasuaji huo uliofanyika Septemba 23, kwa mafanikio makubwa ilienda vizuri.
Kwa mujibu wa Daktari bingwa wa upasuaji kwa watoto Dkt. Petronila Ngiloi amesema mapacha hao walizaliwa na mama yao aitwaye Esta (22) nyumbani kwao Kisarawe, alikozalishwa nyumbani baada ya kugundua watoto wameungana walipelekwa Kituo cha Afya cha Kibaha na baadaye kuhamishiwa Muhimbili wakiwa wamechoka sana.
Amesema watoto hao walipochunguzwa iligundulika wameungana sehemu kubwa ya ini na ikaonekana upasuaji huo unaweza kufanyika MNH ambapo walifanya kazi ili kuona mama huyo anapata huduma nzuri
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
NA REBECA DUWE TANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Burian amewataka wananchi wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya ndoa na ardhi ...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
