Monday, October 1, 2018
Spika Ndugai amuandikia barua Mwenyekiti wa NEC kujiuzulu kwa Mbunge wa Chadema
Kufuatia kujiuzulu ubunge wa Jimbo la Serengeti mkoani Mara, Marwa Ryoba Chacha, Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ye Uchaguzi NEC, Jaji Semistacles Kaijage kumfahamisha kuwa jimbo hilo kwa sasa lipo wazi.
Spika Ndugai ameandika barua hiyo kwa mujibu wa kifungu 37(3) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi kinachoelekeza kwamba pale ambapo mbunge amejiuzulu, atafariki au ataacha kazi ya ubunge kwa sababu nyingine yoyote tofauti na zilizoainishwa katika kifungu cha 113 cha sheria hiyo, Spika atamjulisha Mwenyekiti wa NEC na kutangaza kwenye gazeti la Serikali kwamba kiti hicho kiko wazi.
Chacha alitangaza kujiuzulu Ubunge na nafasi zake zote za uongozi ndani ya Chadema huku akitangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi kwa kile alichoeleza kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...