Mnakubaliana nami kuwa kupenda mtu ni tofauti na kuishi kwa upendo. Kumpenda mtu ni rahisi lakini kwa kuishi huo upendo, yaweza kuwa ngumu kidogo. Ian Isherwood anasema kuwa kurudiarudia huu mshororo wenye maneno matatu tu, "I Love You" Mara kwa mara haitoshi kuweka mapenzi ya uhusiano wenu kunoga zaidi milele. Kuna Sentensi sita muhimu sana ukimwambia mpenzio mara kwa mara napenzi yenu yafikia upeo.
Kila mtu ana njia yake ya kumwonyesha mpenzi wake kuwa anampenda na kumjali. Haijalishi ni maneno yepi hutumia. La maana ni kwamba uhusiano wake na mpenziwe unadumu kwa raha tele.
Ukitumia maneno mazuri kwa mpenzi wako unampa furaha na kumwonyesha kuwa yeye ndiye mtu wa kipekee kwako duniani. Kama unaye mpenzi, anza kutumia , maneno haya sita na uhusiano wako utakuwa wenye raha;
1. Nimebahatika kuwa nawe
Kumwelezea mpenzio vile unajisikia kubahatika kuwa naye katika maisha yako ina uzito zaidi kuliko " Love You".
Wakati unampenda mtu sana unajiona duni kwamba hata kuona amekufanyia fadhila ({Favour) kuwa nawe. Yaani ni kama huna cha kumrudishia kama shukrani kwa upendo wake kwako. Ukisema haya wamfanya kujiskia amependwa na kwamba unafurahia anayokufanyia.
2. Pole/ Samahani
Kusema Pole baada ya kukoseana au majibizano madogo huongeza mapenzi katika ndoa yenu. Kusema "pole" haitamaanishe eti wewe ni hafifu sana kumliko mwenzio. Kila ndoa huwa na majibizano, wivu na kutoelewana. Lakini baada ya hayo yote, sema "pole" na kwa ukweli yatapoa!
3. Nimekusamehe
Ni vigumu kwa mtu kuomba msamaha lakini ni vigumu zaidi kusamehe mtu. Msamaha ni jambo muhimu sana katika uhusiano.
Ni ngumu sana kuifanya mara kwa mara lakini ndiyo huongoza na kupeana mwelekeo wa ndoa. Haina haja kushikilia mabaya ili kuharibu ndoa yako. Msamehe tu!
4. Nipo hapa kwa ajili yako
Ukimpenda mtu, mkubali kwa jiinsi alivyo kwa uzuri au ubaya. Hakuna aliyekamilika. Wakati mwenzako anapitia magumu, hakuna maneno yanayompa nguvu kuliko " Nipo hapa kwa ajili yako" kutoka kwa ampendaye. Maneno haya humhakikishia mwenzio kuwa una yeye katika hali zote za kimaisha.
5. Nakuamini
Bila kuaminiana ndoa haiwezi dumu. Ndoa hupata majaribu hata ikiwa ya miaka hamsini! Lakini la muhimu sana ili kudumisha mapenzi katika ndoa ni uaminifu.
Ukimwambia mwenzako unamuamini, basi umeondoa hisia za mbaya kumhusu kama wivu ambao ni hatari sana kwa ndoa.
6. Nijitolea kwako kikamilifu
Kujitolea kwa hakika kwa mpenzio huonyesha kuwa ulimchagua yeye pekee, kawa mwaminifu na kampeda kwa dhati. Kila mtu hutaka kuhakikishiwa kuwa ni yeye tu katika uhusiano. Usione ni kawaida kuwa na mpenzio.
Watu wengine hutumia maneno haya kwa nia mbaya. Kama kukushawishi mshiriki mapenzi ama kujinufaisha kifedha. Usidanganyike! angalia pia matendo yao kama yanaambatana na maneno yao.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
