Wednesday, October 3, 2018

Dreamliner kupaa na mashabiki wa Stars

Dreamliner kupaa na mashabiki wa Stars
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka nchini TFF imetangaza kuwa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itasafiri na ndege maalumu kuelekea nchini Cape Verde kwaajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON.


Taifa Stars inatarajia kucheza  na Cape Verde mjini Praia, 12 Oktoba kabla ya mchezo wa marudio utakaopigwa Jumanne 16, Oktoba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari kuhusiana na uamuzi huo, Waziri Dkt.Harrison Mwakyembe amesema,

" Mechi hizi mbili ni muhimu kwa sisi kushinda ili kujiweka katika mazingira ya kuzufu mwakani nchini Cameroon, tumeona njia pekee ni kutumia silaha yetu ya mwisho ambayo ni Boeng 787 Dreamliner, Asante JPM. Hii ni ndege pekee kwanza isiyochosha kwa safari ndefu na inayoweza kuibeba Taifa Stars na mashabiki wake bila kutua shemu yoyote ", amesema Dkt.Mwakyembe.

" Kwa Taifa Stars kutua nchi kama ile tena kwa Dreamliner ikishuka na wachezaji kama Mbwana Samatta, tayari tumeshawapiga bao mbili kisaikolojia  ", ameongeza.

Pia Waziri Mwakyembe ametangaza bei kwa mashabiki wanaotaka kwenda kuisapoti timu yao, ambayo ni dola 1,500 ambazo ni sawa na Shilingi 3.5 millioni za Kitanzania kwa daraja la kawaida na dola 2,000 kwa daraja la kibiashara 'Business Class'.

Kwa upande wake, Rais wa TFF, Wallace Karia amewataka watanzania kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ya kuungana na timu yao katika ndege moja na wachezaji ili kwenda kuishangilia na kuhakikisha timu inarejea na matokeo mazuri.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...