Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa na albamu yake ya 'Gold' amewajia juu watu ambao wamekuwa wakitumia vibaya mitandao ya kijamii. Serikali imekuwa ikikemea vikali matumizi mabovu ya mitandao ya kijamii kwani Kumekuwa na watu wanaofanya uharibifu na mitandao hiyo ikiwemo kutoa kugha chafu za matusi na hata kuikashifu Serikali. Mwezi uliopita Serikali Kupitia TCRA walitangaza kuwateua wasanii kama Barnaba, Hamisa Mobetto na wengineo kuwa mabalozi wa kuhakikisha kunakuwa na matumizi bora ya mitandao ya kijamii. Kwenye interview na Ayo Tv, Barnaba Boy Classic ametoa Kauli yake kuhusu harakati zake lakini kubwa zaidi ni kauli yake kwa watanzania ambao wanatumia vibaya mitandao ya kijamii na yeye akiwa kama balozi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA ). Vijana wajitambue katika nafasi zao na sisi kama Serikali tupo macho na hatutamchekea yeyote anayetumia vibaya mitandao ya kijamii, hii hatuwaambii kwa kuwatisha ila tutawashughulikia".
The post Barnaba Awashukia Wanatumia Mitandao Ya Kijamii Vibaya appeared first on Ghafla!Tanzania.
Source