Friday, September 14, 2018

Zijue faida za uaminifu katika mahusiano ya Ndoa


Suala la uaminifu katika mapenzi kwa karne hii limekuwa kikwazo kikubwa kwa watu wengi sana, wengi wemekuwa si waaminifu wakati mwingine kupelekea mahusiano hayo kufa.

Hivyo uaminifu ni muhimu sana katika mapenzi kwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuna faida nyingi kwa mwili na akili. Watu walio katika mahusiano bora ya mapenzi huishi maisha marefu na kufurahia afya njema kuliko wale wasiokuwa katika mahusiano ya aina hiyo.

Faida hii haina pingamizi
kwa sababu ya ukweli kwamba watu wanaokuwa katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu fulani ambayo huwasaidia kusaidiana na kujaliana wakati wa shida. Siyo tu kwamba watu walioko katika mahusiano ya aina hii wanaishi muda mrefu lakini pia ni kweli kwamba wanakuwa na furaha na wanaridhika na maisha kuliko wale wanaoshindwa kukaa katika mahusiano.

Pili, kuwa katika mahusiano mazuri ya mapenzi kunasaidia katika mambo mbalimbali ya kimahitaji. Kusaidiana katika mahitaji mbalimbali baina ya wapenzi ni njia nzuri ya kuwa na maendeleo. Watu wawili wanaoshirikiana pamoja mara nyingi watakuwa na maisha mazuri zaidi ya yule anayefanya peke yake.

Unapokuwa na mtu karibu wa kusaidiana naye katika mahitaji ni rahisi kupata mafanikio. Watu walio katika mahusiano mazuri wanapata msaada wa kijamii; kwa maana ya kuwa na mtu wa karibu ambaye anajali mahitaji yako ya msingi na hisia zako. Kuwa na msaada
wa aina hii kuna faida nyingi, mojawapo muhimu ni kuweza kufanya maamuzi ya busara bila kuwa na mtindio wa mawazo na hofu ama mashaka.

Kuwa na mwenza katika maisha hufanya maisha kuwa ya faraja zaidi.
Kuwa na mtu ambaye mnaweza kushirikiana mambo madogo madogo ya maisha kama kuangalia Tv, kutembea, kula pamoja ni muhimu; inaboresha mahusiano na mara nyingi watu walio katika mahusiano ya aina hii wamekuwa na maisha bora zaidi.

Mahusiano ni muhimu kwa sababu wapenzi wana kawaida ya kuangaliana tabia zao hasa zile ambazo ni haribifu, na wamekuwa na kawaida ya kuonyana ama kushauriana kuacha kufanya mambo mabaya na tabia mbaya.

Kwa mfano watu walio katika mahusiano ya karibu wamekuwa na tabia ya kujaribu kuwashauri wapenzi wao kuacha kuvuta sigara, kupunguza pombe, kuacha kutumia madawa ya kulevya
nk.
Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...