Tuesday, September 18, 2018

Kiongozi wa Mbio za Mwenge atembelea maduka kuhakiki bei ya mabati baada ya Kuhisi Udanganyifu

KIONGOZI wa mbio za Mwenge Kitaifa, Charles Kabeho amelazimika kuacha kuzindua ujenzi wa madarasa manne ya shule ya Sekondari Arusha kwa muda na kisha kuacha mwenge wa uhuru shuleni hapo na  kwenda kwenye maduka ili kujirithisha kama kweli bei ya bati aliyoambiwa ni sahihi na bei ya dukani. 
Kabeho alilazimika kufungua madarasa hayo yaliyojengwa kwa gharama ya sh, milioni 78,309,200 ambapo awali alisomewa taarifa zilizokinzana za bei ya bati na gharama halisi ya mradi kwa ujumla. 
Awali Kabeho alibaini ramani iliyotumika kujenga jengo hilo si ya Mkoa wa Arusha bali ni ya mkoa wa Kilimanjaro na hata bei halisi ya bati na kampuni ya mabati hayo haikujulikana. 
Baada ya kusomewa taarifa kutoka kwa Mwalimu Mkuu, Christopher Malamsha iliyodai kuwa jengo hilo la madarasa manne yamejengwa ili kuondoa changamoto ya wanafunzi wanaodahiliwa shuleni hapo. 
Malamsha alisema jengo hilo limegharimu sh, milioni 78. 309 na kusema kuwa watapunguza msongamano wa ongezeko la idadi ya wanafunzi. 
Baada ya kukabidhiwa taarifa ya Mwalimu Mkuu huyo, Kabeho aliiita timu ya wakimbiza mwenge kitaifa na kujifungia ndani ya jengo hilo kisha kupitia taarifa yote kisha kutoka nje na kuanza kuhoji gharama za mabati, viti vya kulalia wanafunzi (madawati) kisha kuhoji geji moja ya bati saizi 28 inauzwa kiasi gani. 
Na ndipo Injinia wa Jiji la Arusha, Mshuza alisema geji moja ya bati inauzwa kwa sh 17,000  hadi 24, 000 kutokana na bei ya soko baada ya majibu hayo alihoji tofauti ya bei ya sh, milioni 210 ambayo ndio gharama halisi ya bati hizo. 
"Bei halisi ya ujenzi wa madarasa hayo ni Sh, milioni 77ambayo ipo katika ripoti lakini kunafedha ambayo imebaki kwanini hamjasema kama kunafedha imebaki"
Watanzania wanatakiwa kujua gharama halisi ya mradi huu sababu ndio wanyonge halafu wewe nakuuliza bati hili ni la kampuni gani unashindwa kusema na wewe Injinia Samwel Mshuza unashindwa kujua bati ni la kampuni gani "
Sasa sifungui madarasa haya kwa muda wacha niende mtani nikajiridhishe mimi mwenyewe nyie kaeni hapa mnisubiri niende nikirudi nakuja na jibu. 
Na ndipo Kabeho aliondoka timu ya Viongozi alioambatana nayo kitaifa na kwenda madukani kwaajili ya kuuliza bei za bati ambapo baada ya muda alirudi na kisha aliporudi akasema amebaini bei  ya bati hizo ni halali ya bati moja sh, 25,000 ya kampuni ya kiboko, simba na nk kisha akazindua ujenzi wa madarasa hayo. 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...