Wednesday, September 12, 2018
Chadema yawataka wanaohama chama kumuiga Nyalandu
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo, CHADEMA, Dk. Vincent Mashinji, amesema, Wabunge na Madiwani wanaojiuzulu na kuhama chama, waondoke tu kwa wema wala hakuna haja ya kusuguana na kusumbuana kila kukicha.
Dk. Mashinji ameweka wazi hilo leo kwenye mkutano wake na wanahabari jijini Dar es salaam, ambapo amesisitiza kuwa, mtu kuhama chama ni kutekeleza haki yake ya msingi ya Kikatiba na sio jambo la kusubiri usiku wa saa 6:00 ndio utangaze.
''Kati ya Wabunge 73 tuliopata kwenye uchaguzi mkuu 2015, watatu ndio wamehama, lakini wanatangaza usiku wakati hakuna haja ya kufanya hivyo maana Mwenyekiti alishawaambia waondoke tu kwa wema na chama hakitahangaika nao'', amesema, Dk. Mashinji.
Aidha, Dk. Mashinji ameongeza kuwa wanaohama wangeiga mfano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia (CCM), Lazaro Nyalandu, ambaye alijiuzulu nafasi yake kwa kufuata utaratibu ikiwemo kumwandikia barua Katibu wa chama chake pamoja na Spika wa Bunge.
Aidha, CHADEMA imewahakikishia wanachama wake kuwa, imejipanga vyema na ina uungwaji mkono mzuri katika majimbo mawili yanayofanya uchaguzi mdogo wa Wabunge ya Monduli na Ukonga na wanategemea kuibuka na ushindi.
Wabunge wa CHADEMA waliojiuzulu ni Godwin Mollel, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro, Mwita Mwikwabe Waitara aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Monduli Julius Kalanga.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...