Saturday, August 11, 2018

VAR yatumika rasmi Ufaransa, Payet akifanya yake


Kwa mara yakwanza ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 hapo jana imeanza kutumia mfumo wa VAR kwenye mchezo wa ufunguzi baina ya timu ya Marseille iliyopata ushindi wa mabao 4 – 0 dhidi ya Toulouse.
Mchezaji wazamani wa West Ham, Dimitri Payet amenufaika na VAR baada ya kupewa penati kupitia mfumo huo na kuandika bao lake lakwanza dakika ya 45 kabla hajafunga lapili dakika ya 62 wakati wachezaji wengine waliyotupia mabao ni Germain dakika ya 89 na Florent Thauvin akihitimisha karamu hiyo yamagoli dakika ya 90+2.
Payet ambaye alishindwa kucheza kombe la dunia kutokana na kusumbuliwa na majeraha amepata penati hiyo baada ya mwamuzi wa mchezo huo Ruddy Buquet kuamuru kona kabla ya VAR kumzawadia penati mchezaji huyo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...