Wednesday, August 15, 2018

“Nina Kipaji na Ninaweza” Ali Kiba Afunguka Kucheza Soka La Kulipwa

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuongelea kitendo chake cha kujiingiza katika soka la kulipwa ambapo hivi sasa ni mchezaji rasmi wa Coastal Union. Wiki chache zilizopita Ali kiba alitangazwa rasmi kama mchezaji wa timu ya Coastal Union yenye makazi yake mkoani Tanga. Kwenye mahojiano na Azam Tv, Ali Kiba anafunguka juu ya njia mpya aliyochukua na kueleza kuwa ana kipaji cha kucheza mpira na uwezo pia anaamini kuwa anao: Mimi kwa kipaji changu binafsi nimeona kwamba ninaweza na ndio maana nikajiunga na Coastal Union sababu ya kipaji nilichokuwa nacho". Lakini pia ALi Kiba amefunguka kuhusu uwezo wa timu yake hiyo mpya na malengi waliyokuwa nayo: Coastal Union wanajutahidi na ni wapambanaji na tunatafuta title msimu huu japokuwa kuna timu kongwe lakini mpira wanasemaga unadunda kwaiyo ni kupambana tu tutafika". Ali Kiba pia ameweka wazi kuwa kinywaji chake cha Mo Faya ndiyo kitaidhamini timu hiyo.

The post "Nina Kipaji na Ninaweza" Ali Kiba Afunguka Kucheza Soka La Kulipwa appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...