Friday, August 24, 2018

Mobetto- Sina Ubaya na Wanawake Wanaomtaka Diamond

Mwanamitindo na msanii wa Bongo movie Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa hana ubaya na wanawake ambao wanamtaka Baba mtoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz. Hamisa na Diamond wamefanikiwa kuzaa pamoja mtoto mmoja wa mwaka mmoja anayeitwa Dylan wakat Diamond ana watoto wengine wawili na mwanamama Zarinah Hassan. Kwenye mahojiano na Global Publishers Hamisa amefunguka wakati alipoulizwa kuhusu Msanii wa Bongo fleva Pretty Kind ambaye aliwahi kuweka wazi mapenzi yake kwa Diamond na baadaye kulalamika Hamisa kachukia hadi kamblock: Hamisa amekana kumblock Pretty Kind na kudai yeye hana ubaya na mwanamke yoyote anayemtaka Diamond ambaye anasemekana kuwa ni mpenzi wake: Kwanza kabisa nilikuwa simjui na hata kumsahau huyo mtu mwenyewe halafu sijamblock kwa sababu ya Diamond kwa sababu kuna wanawake kama milioni tano wote wanamtamani huyo huyo mtu mmoja sasa sasa kama ndio hivyo nitawablock watu wangapi Jamani? Pretty Kind kuna Maneno machafu na mabaya aliyaongea kuhusu mimi alinichafua sana halafu mimi ni brand simjui nikaona huyu naye katokea wapi? Nikamblock Maisha Yangu yaendelee kwa amani wa Nini mtu anayenipa kero". Pretty Kind alifunguka kuwa kama akitaka kutoka kimapenzi na Diamond anaweza akampata kwa sababu yeye ni mzuri na ana vigezo vyote vya kutokataliwa na Diamond.

The post Mobetto- Sina Ubaya na Wanawake Wanaomtaka Diamond appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...