Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema hatajiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa licha ya kushinikizwa na baadhi ya wanachama kuachia nafasi hiyo.
Chalamila alitoa msimamo huo jana alipokuwa anazungumza na viongozi wa dini na kueleza baadhi ya wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa wanamshinikiza ajiuzulu, ili kukidhi matakwa ya utaratibu mpya wa chama unaotaka mtu mmoja kuwa na cheo kimoja.
Alisema ataendelea kuwa mwenyekiti mpaka Rais Dk. John Magufuli ambaye ndiye aliyemteua, atakapotoa maelekezo mengine.
"Baada ya kuteuliwa kuna baadhi ya watu walinifuata wakinitaka nijiuzulu nafasi ya uenyekiti, sasa ninachokijua ni kwamba Rais aliniteua kuwa Mkuu wa Mkoa akiwa anajua kuwa mimi ni mwenyekiti, hivyo naendelea kushika nyadhifa zote mpaka nitakapopata maelekezo mengine," alisema Chalamila.
Katika hatua nyingine, Chalamila alisema kwa muda mrefu Jiji la Mbeya limekuwa halipati maendeleo kutokana na mwendelezo wa siasa chafu zinazoifanya serikali ishindwe kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo.
Aliwataka viongozi wa dini kuisaidia serikali katika kuhubiri amani na kuwaelimisha vijana kufanya kazi kwa bidii badala ya kuendekeza vijiwe vya siasa zisizokuwa na manufaa katika maisha yao ikiwamo kukashifu vyama wasivyoviunga mkono.
Alisema katikati ya Jiji la Mbeya barabara ilitakiwa iwe ya njia nne na barabara ya mchepuko kutoka Uyole mpaka Songwe kwa ajili ya magari makubwa ya mizigo ilitakiwa iwe imejengwa, lakini siasa zimekuwa zikikwamisha.
"Hili ni jiji, lakini siku zote huwa najiuliza kuwa ni kweli serikali imeshindwa kujenga barabara ya njia nne, ni kweli serikali imeshindwa kujenga kilomita 40 barabara ya mchepuko na je, serikali imeshindwa kuukamilisha uwanja wa ndege wa Songwe na kuupa hadhi yake ya kimataifa?" Alihoji Chalamila.
"Ninachokiona hapa ni kwamba siasa ndiyo 'zinatucost' (zinatugharimu), mtu anaamua kurudisha nyuma mikono na kuacha aone tunavyofanya, lakini kwa sasa naona hali imeanza kuwa tulivu, mimi na katibu tawala tutamwandikia rais atusaidie baadhi ya miundombinu hii muhimu iboreshwe haraka," alisisitiza.
Aliwaomba viongozi wa dini mkoani humo, kuendelea kuisaidia serikali kuwaelimisha vijana kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo na kuachana na siasa chafu ambazo hazina manufaa kwa sasa.
Aliwataka kuanzisha madarasa maalumu ya kuwafundisha vijana ujasiriamali kwenye maeneo yao ya kuabudia, ili wajikite kwenye shughuli hizo na kujiletea maendeleo.
Credit:Nipashe
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
