Thursday, August 16, 2018

Lulu Diva- Siwezi Kuachana na Mavoko Kisa Kuondoka WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kudai hawezi Kuvunja Bongo Penzi lake na msanii wa Bongo fleva Richard Mavoko kisa tu amejitoa WCB. Lulu Diva ambaye amekuwa Kwenye Mahusiano ya muda mrefu na Rich Mavoko ameongea juu suala hili kutokana na sakata linaloendelea hivi sasa kati ya Mavoko na uongozi wake WCB. Kwenye na Global Publishers, Lulu Diva amesema kuwa amekutana na maswali ya wengi ambayo yame-fanya afahamu kwamba wanahofu na penzi lao kwamba linaweza kuwa ni mwisho kwa sababu uhusiano wao ulianza wote wakiwa wapo kwenye lebo hiyo, lakini wafahamu kwamba penzi lao haliwezi kukatishwa na WCB. Watu wanahofia kwamba nitaachana na Mavoko kwa sababu ya kutoka WCB, hilo ni jambo lisilowezekana kwani tunapendana kweli na penzi letu halishikiliwi na lebo". Lulu diva pia alikataa kuongelea tetesi ambazo zimekuwa zikienea kuwania hivi sasa ana ujauzito wa Mavoko.

The post Lulu Diva- Siwezi Kuachana na Mavoko Kisa Kuondoka WCB appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...