Kocha wa Yanga,Mwinyi Zahera amewatamkia mashabiki wa klabu hiyo, habari nzuri ya kufurahisha ambayo imetokana na kazi pevu anayoifanya kambini mkoani Morogoro.
Mechi kubwa ya Yanga inayofuata ni Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Algers ya nchini Algeria itakayofanyika Agosti 19 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kukamilisha ratiba kwani maji yameshazidi unga.
"Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya kujiandaa na ligi kuu lakini pia mechi yetu Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ambayo tutacheza hivi karibuni. "Hali ya kikosi changu kusema kweli ni nzuri na ninavutiwa zaidi na hali ya kujituma uwanjani inayoonyeshwa kila siku na wachezaji wangu," alisema Zahera ambaye ana uraia wa DR Congo na Ufaransa.
"Kuhusiana na kikosi cha kwanza kitakachokuwa kikianza katika michuano ya ligi kuu, tayari nimekipata lakini hakutakuwa na mchezaji ambaye atakuwa na uhakika wa namba kwa asilimia mia moja, mchezaji atakayekuwa akifanya vizuri mazoezini huyo ndiye atakayekuwa na nafasi kubwa ya kucheza," alisema Zahera.
Licha ya kutotaja wazi majina ya kikosi hicho, lakini kulingana na mazoezi ambayo wamefanya inaonekana wazi kuwa golini atakaa kipa Klaus Kindoki, atasaidiana na walinzi Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vicent 'Dante', Kelvin Yondani viungo ni Papy Kabamba Tshishimbi, Rafael Daud, Feisal Salum 'Fei Toto', Deus Kaseke na Mrisho Ngassa huku mbele akisimama mshambuliaji mmoja ambaye ni Heritier Makambo.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
