Tuesday, August 14, 2018
BREAKING: CCM yawarudisha tena Waitara, Kalanga kwa wananchi
Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo imekutana na kufanya kikao chake ambacho kimepitisha majina ya wagombea wa ubunge watatu katika majimbo matatu ya Ukonga, Korogwe Vijijini na Monduli.
Majimbo hayo yalitangazwa kuwa wazi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya mbunge wa Ukonga kujiondoa Chadema na kujiunga na CCM na mbunge wa Monduli naye kujiondoa Chadema na kujiunga na CCM na kwa upande wa Korogwe Vijijini mbunge wake alifariki dunia.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt. John Magufuli ambaye aliongoza kikao hicho katika ofisi ndogo za CCM zilizoko Lumumba Jijini Dar es Salaam ametaja majina ya wagombea waliopitishwa kuwa ni Julius Kalanga Laizer jimbo la Monduli, Mwita Mikwabe Waitara jimbo la Ukonga na Timotheo Paul Mzava jimbo la Korogwe Vijijini.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Magufuli amewashukuru na kuwapongeza Watanzania kwa kuipatia CCM ushindi wa asilimia 100 katika uchaguzi mdogo uliomalizika kwa kuiwezesha kutwaa jimbo la Buyungu Kigoma na kata zote 77.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
