Tuesday, August 28, 2018

Birdman Ajishusha Amuomba Msamaha Lil Wayne Mbele ya Maelfu ya Mashabiki

 Birdman Ajishusha Amuomba Msamaha Lil Wayne Mbele ya Maelfu ya Mashabiki
UGOMVI wa kifamilia kati ya wasanii Birdman na Lil Wayne umemalizika Jumamosi iliyopita kwenye tamasha la  Lil Weezyana Fest lililofanyika huko New Orleans, Marekani, ambapo Birdman aliomba msamaha mbele ya maelfu ya mashabiki waliokusanyika katika dimba la  Champions Square.

Tukio hilo linafuatia watu hao wawili kumaliza bifu lao ambapo Wayne alimfungulia mashitaka Birdman kwa kumdai Dola mil. 51 (Sh. bil. 117) ili ajiondoe katika mkataba wake mwaka 2015.

Hilo lilimalizika kwa siri mnamo mwezi Juni mwaka huu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...