Wednesday, August 19, 2020

Waziri Mkuu: Kuweni Wabunifu Muweze Kujiajiri

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wanaohitimu masomo nchini wasikae majumbani na badala yake watumie elimu yao kubuni namna ya kujiajiri.

"Lazima tubadilike ili wahitimu wasisubiri kazi za masomo. Ukimaliza masomo, tumia ujuzi wako kuona unaweza vipi kujiajiri," alisema.

Ametoa wito huo jana jioni (Jumatatu, Agosti 17, 2020) wakati akizungumza na wahitimu wa Seneti ya Dar es Salaam kwenye mahafali ya vyuo na vyuo vikuu vya jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee, jijini humo.

"Tunajaribu kuondoa dhana ya ajira ni ile kazi ya kushika kalamu na kukaa ofisini na kulipwa mshahara mwisho wa mwezi. Sasa kama wasomi wote tukitaraji kuajiriwa, hatutaweza. Lazima tukubali kuwa ajira ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato chake," alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani imefanya kazi ya kuboresha mazingira ya utoaji wa taaluma kwa kujenga na kukarabati miundombinu katika baadhi ya vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu nchini.

"Ili kuondoa adha ya malazi kwa wanafunzi kwa vyuo na taasisi za elimu ya juu zilizopo Dar es Salaam, Serikali imetoa nyumba za Serikali zilizoko Kigamboni na Kijichi, jijini Dar es Salaam."

Akizungumzia kuhusu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Waziri Mkuu alisema ujenzi wa maktaba ya kisasa inayochukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja uligharimu sh. bilioni 93. "Ujenzi wa mabweni 20 ya Dkt. John Pombe Magufuli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 na ukarabati wa hall 2 na 5, yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 788 uligharimu shilingi bilioni 15.48," alisema.

Kuhusu Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE), Waziri Mkuu alisema Serikali ilitumia sh. bilioni 1.5 kujenga miundombinu ya kufundishia na ofisi za wahadhiri Katika chou hicho na pia ilitumia sh. bilioni 4.9 kufanya ukarabati mkubwa wa majengo ya Hall 2 na Hall 5 chuoni hapo.

"Kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) tulitumia shilingi bilioni 11.5 kwa ajili ya ujenzi wa maabara yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,400 kwa wakati mmoja; ujenzi wa Kafeteria ya wanafunzi pamoja na kutengeneza shamba darasa kwa shilingi milioni 700; ukarabati wa karakana ya uhandisi kwa shilingi milioni 750 na ununuzi wa matrekta 10 aina ya URSUS pamoja na majembe nane na harrow mbili kwa thamani ya shilingi milioni 587.5 ili kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa vitendo."

Akielezea uboreshaji uliofanywa kwenye Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Waziri Mkuu alisema ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 716 uligharimu sh. bilioni 3.44 ilhali Chuo Kikuu cha Dododma (UDOM) kilinunuliwa vifaa vya maabara vya thamani ya sh. bilioni 3.0.

"Kwa upande wa Chuo cha Ardhi (ARU), tumeanza na awamu ya kwanza ya ujenzi wa bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 312 kwa gharama ya shilingi bilioni 2.61, Na kwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), tumejenga jengo la mihadhara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,200 kwa gharama ya shilingi bilioni 8.8. Pia tumejenga maabara kwa gharama ya shilingi bilioni 2.1," alisema.

Kuhusu Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU), Waziri Mkuu alisema ujenzi wa hosteli zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,024 uligharimu sh. bilioni 6.5 huku ujenzi wa jengo la mihadhara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 900 ulitumia sh. bilioni 3 katika kampasi ya Mzumbe-Mbeya.

Na kwa upande wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Waziri Mkuu alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa maktaba ya kisasa yenye uwezo wa kuwahudumia wanafunzi 2,500 umekamilika kwa gharama sh. bilioni 5.523.

"Kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila, ujenzi wa miundombinu ya hosteli zitakazochukua wanafunzi 1,370, ujenzi wa maktaba, kafeteria, madarasa na ukumbi wa mihadhara utagharimu shilingi bilioni 13.3," alisema Waziri Mkuu.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Tuesday, August 18, 2020

Ray Kigosi na Chuchu Hans Hapatoshi..Ray Aandika "Mwanamke Mjinga Huivunja Ndoa Yake Kwa Mikono Yake Mwenyewe" Wadau Wamshukia

Ray Kigosi na Chuchu Hans Hapatoshi..Ray Aandika "Mwanamke Mjinga Huivunja Ndoa Yake Kwa Mikono Yake Mwenyewe" Wadau Wamshukia Ray Kwenye Comments


Soma Baadhi ya Comments wadau walivyomkatalia:

Zamani wanawake wa jinga ndo wali kuaga na bomoa nyumba zao kwa mikono Yao wenyewe but kwa sasa imeshaa geuka' wanaume wajinga hu bomoa nyumba zao kwa ku chepuka kwao ' volume ina tosha? Na pita tu

Enyi wanaume ishini na wake zenu kwa akili, (basi aliyeshindwa kuishi na mkewe maana yake hana akili)


Kaka wew ni mwanaume mkuu mambo ya mipasho waachie wanawake,kama nyumba inawaka moto mwite huyo mjinga tafuta wazee wenye busara wajaribu kuwasuluhisha

embu toeni hiko kimovie chenu bwana mstusumbue sisi


Mjinga ni ww ambae huna hata haya mwanamke kakuzalia mtoto mzr bd unamsaliti mbwa ww ambae huna hata kiwanja unaishi kwenu

maandiko yanasema wanaume ishini na wanawake zenu kwa akili kwahyo yeye kashindwa kuishi na mkewe kwa akili basi hana akili #SautiInatosha

Monday, August 17, 2020

TFF YAMLIMA BARUA MWENYEKITI WA YANGA SC, DKT. MSHINDO MSOLLA




Harmonize,H Baba Wamfanyia Surpise Barnaba Classic


Wikiendi ilikuwa ndefu au busy sana kwenye upande wa burudani kutokana na yaliyotokea kuanzia Uwanja wa Uhuru ambapo zaidi ya wasanii 100 walifanya show kupitia chama ca Mapinduzi CCM pamoja na show aliyoifanya Barnaba.



Tuliangalie hili la Barnaba ambalo alitumia zaidi ya saa 3 stejini kufanya show ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao kama Harmonize, Gigy Money, Lulu Diva, H Baba, Country Boy, Linah, Aslay, Tunda , Whozu, Kusah, Beka Flavour , Chegge na Don Dada "Masha Love".

Kubwa ni suprise aliyofanyiwa Barnaba na wasanii wenzake ambao waliweza kumtunza pesa za kutosha wakati wa show hiyo, kwa harakaharaka unaweza kusema Barnaba amemwagiwa vibunda vya kutosha ambayo anaweza asifanye tena show mwaka huu na bado angebakiwa na pesa hizo.

Thursday, August 13, 2020

Mhadhiri UDOM kizimbani kwa rushwa ya ngono

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini  [TAKUKURU ]mkoa wa Dodoma  inatarajiwa kuwafikisha mahakamani watu 10 katika mahakama za Dodoma na Bahi na kuwafungulia mashauri yanayohusiana na Rushwa akiwemo Mhadhiri Msaidizi Chuo kikuu cha Dodoma akihusihwa na rushwa ya ngono..

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 13,2020 jijini Dodoma,Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapa Bw.Sosthenes Kibwengo amesema kwa kushirikiana na ofisi ya taifa ya mashtaka ,TAKUKURU mkoani Dodoma itamfikisha mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Bw.Jacob Paul Nyangusi [43]mhadhiri Msaidizi wa chuo kikuu cha Dodoma[UDOM]na kumfungulia shauri la uhujumu uchumi kwa kosa la kutaka rushwa ya ngono kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11 /2007 ikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza na vifungu vya 57[1]na 60[2] vya sheria ya uhujumu uchumi   sura ya 200 marejeo ya mwaka 2020.

Bw.Kibwengo amefafanua kuwa,Majira ya saa 3 usiku   wa tarehe 3,Oktoba,2018 TAKUKURU ilimkamata Bw.Nyangusi nyumbani kwake  eneo la  Nyumba Mia tatu jijini Dodoma muda mfupi kabla hajatekeleza nia yake ovu ya kufanya ngono  na aliyekuwa mwanafunzi wake wa mwaka wa kwanza wa shahada ya sanaa katika jiografia na Mazingira.

Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoani Dodoma,ameendelea kufafanua kuwa ,awali TAKUKURU ilipokea taarifa kuwa mtuhumiwa alimtaka  mwanafunzi wake  huyo kingono kama sharti la kumsaidia ili aweze kufanya mitihani ya marudio na kumwezesha kufaulu katika somo lake ,na ndipo ikaweka mtego na kumkamata.

Aidha,Bw.Kibwengo amesema TAKUKURU Dodoma kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Mashtaka watafikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma watu watatu ambao ni Diwani Mstaafu kata ya Ntyuka jijini hapa Bw.Theobald Emmanuel Maina [44],Afisa Mtendaji Mstaafu kata ya Ntyuka Bw.Benedict Baraguyu Mazengo[60] na Mwenyekiti mstaafu mtaa wa Chimala jijini Dodoma Bw.Anderson Jonathan  Mwaluko[48] kwa makosa ya matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na kifungu cha 31 na ubadhirifu kinyume na kifungu cha 28[1]vyote vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa  Na.11/2007.

"Uchunguzi wetu  umeonesha kuwa ,April,2016 watuhumiwa kwa pamoja walitumia vibaya madaraka yao na hivyo kujipatia n kwa njia ya kughushi Tsh.Milioni mbili ambazo ni malipo ya minara ya simu iliyopo kwenye kata ya Ntyuka ,watuhumiwa walifuja frdha hizo badala ya kusimamia ili zitumike kwa ajili ya kununua vifaa vya ujenzi wa ofisi ya Mtaa wa Ntyuka"amesema Bw.Kibwengo.

Bw.Kibwengo amesema TAKUKURU,Dodoma itamfikisha mahakamani  afisa mtendaji Mstaafu kata ya Mnadani Bi.Ritha Protas [30] kwa kosa la kuomba rushwa Tsh.Laki nne kinyume na kifungu cha 15[1]cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa  Na.11/2007.

"Uchunguzi wetu umeonesha kuwa  Tarehe 17,Mei,2019 mtuhumiwa aliwashawishi wanakikundi cha Sabasaba Group ambao walikuwa wanafuatilia mikopo inayotolewa na halmashauri ya jiji  kwa ajili ya wajasiriamali  wampatie fedha hizo ili awasaidie kupata mikopo na baada ya wanakikundi hao kukosa mikopo kama walivyoahidiwa na mtuhumiwa waliamua kwenda  Ofisi za Halmashauri za jiji kutoa taarifa na walipotambua kuwa huo sio utaratibu wa  kupata mikopo,walitoa taarifa TAKUKURU na ndipo uchunguzi ukafanyika na kuthibitika alipokea kiasi hicho alichoshawishi"amesema.

Bw.Kibwengo pia amesema TAKUKURU itamfikisha mahakama ya Wilaya ya Bahi mtendaji wa  kijiji cha Chifutuka Bw.Alfred Ndukai Oleteya[58] na kumfungulia shauri la jinai la kuomba na kupokea rushwa ya Tsh.Laki mbili kinyume na kifungu cha 15[1]a cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa  Na.11/2007.

Hali kadhalika,TAKUKURU mkoani Dodoma inatarajia kuwafikisha katika mahakama ya wilaya ya Bahi watu wanne  ambao ni Afisa Misitu wa Bahi Bw.Said Msemo[56],Ramadhan Juma Said[35]Msaidizi wa  afisa misitu ,Bw.Michael Robert[34],na Bw.Molo Lucas Mwalise [40]Mgambo wa kijiji cha Lamaiti-Bahi kwa makosa ya kuomba rushwa ya Tsh.Laki tano na kupokea laki moja na elfu hamsini kutoka kwa mwananchi mmoja ili wamrejeshee pikipiki yake waliyoikamata awali.

Vilevile Bw.Kibwengo amesema Mahakama ya Kondoa imetoa uamuzi wa shauri la uhujumu uchumi  Na.3/2018  na kumtia hatiani hukumu ya Mwaka mmoja jela au faini ya Tsh.       Mil. Moja  pamoja na  kurejesha Tsh. Mil.7 .25 Bi.Bunana Dioniz Msafiri  afisa mifugo mstaafu halmashauri ya mji wa Kondoa  ambapo Agosti 2018 TAKUKURU ilimfikisha Mahakamani kwa matumizi mabaya ya mamlaka   aliyosababisha hasara  ya  Tsh.Mil.7.25 za ushuru wa machinjio  alizokusanya bila kuwasilisha halmashauri.

Sanjari na hayo,TAKUKURU mkoani Dodoma  Mwezi Julai 2020 imefanikiwa kuokoa  mbao 106 zilizokuwa zimevunwa na kuhifadhiwa kinyume na taratibu  katika nyumba ya mwananchi mmoja kijiji cha Lamaiti Wilayani Bahi .

MWISHO.


Wednesday, August 12, 2020

Ufaransa yatolea wito Lebanon kunda serikali mpya

Ufaransa imetolea wito Lebanon kuunda serikali mpya  haraka iwezekanayvo baada ya waziri mkuu wa tiafa hilo kujizulu siku chache baada  ya mlipuko uliopelekea vifo vya watu  zaidi ya  150 kufariki na wengine zaidi ya  6000 kujeruhiwa mjini  Beyrut.


Waziri mkuu wa Lebanon  Hasan Diab  alitangaza kujiuzulu kufuatia   mlipuko huo ambao umesababisha maafa makubwa nchini Lebanon.


Wito huo umetolewa na Ufaransa muda mchache baada ya waziri Hasan Diab kutangaza kujiuzulu kwake katika wadhifa wake wa waziri mkuu wa Lebanon.


Kwa mujibu wa Ufaransa , hali iliopo nchini Lebanon inastahili  inatakiwa kupatia ufumbuzi  kwa ajili ya kukidhid matkwa ya raia ambao wanahitaji  kusikilizwa na kuhudumiwa katika kipindi hiki kigumu.


Rais wa Ufaransa alifanya ziara nchini Lebanon baada ya  janga mablo limekumba taifa hilo.


Viongozi tofauti akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Uturuki walikwenda nchini na baade kufuatia msaada wa vifaa vya matibabu na madaktari ambao wanawahudumia majeruhiwa wa mlipuko uliotokea mjini Beyruth.


 

Tuesday, August 11, 2020

Shamsa Ford Awavaa Kinadada wa Mjini "Huwa Mnatutisha Mnaonekana Mna Mishape Kumbe Edit"



"Wadada wa mjini waongo nyie dah.Huwa mnatutisha mnaonekana mna mishape kumbe Edit 🙉.Na mm leo nimeeditiwa na Chris Yaani hiyo shape sina kabisaa nina mtumbo balaa na sina makali niko flat screen😆😆.kaka zangu hawa wadada wasiwatishe na mipicture yao kabisaaa yaani Instagram wanaonekana nyama rost kumbe tembele😆😆" - amesema Shamsa

EXCLUSIVE: Noorah awa muuza duka, afunguka mazito “kila shabiki namdai elfu 10, wanaabudu ngono” (+video)



Haji Noorah maarufu 'Noorah baba Stylz' ni miongoni mwa majina makubwa kwenye muziki wa bongofleva, sasa hivi ni zaidi ya miaka ya miaka 10 hajasikika kwenye muziki, pamoja na kwamba Noorah alipitia matatizo kadhaa ikiwepo ajali mwaka 2005 lakini pia mke wake wa kwanza kufariki 2015 lakini kuna sababu anazo za kwanini sasahivi hayupo tena kwenye muziki.

AyoTV na millardayo.com tumemtembelea ofisini kwake Shinyanga Mjini maeneo ya Kambarage ambapo biashara yake ya sasa ni kuuza spea za magari.

VIDEO:

Msichana mwenye sifa hizi huwa hakiwii kuolewa

Kuolewa ni heshima kwa mwanamke. Heshima hiyo inaenda mbali zaidi hadi kuwagusa wazazi wa binti ambaye ataolewa. Wazazi wanatembea kifua mbele pindi binti yao anapoolewa, tena wanafurahia zaidi binti huyo anapoolewa akiwa angali bado hajazaa.

Wanamshukuru Mungu kwa binti yao kujitunza. Wanamshukuru binti kwa kuwapa heshima katika familia yao na ndiyo maana siku ya sherehe ya kuagwa (send off) wazazi wanafurahi sana kuagana na binti yao kwa heshima.
Hali hiyo huwa inaleta shauku kubwa kwa warembo wengi kutamani kuingia kwenye ndoa. Wengi wanaguswa na rekodi za wanawake wenzao ambao wamejitunza na hatimaye kuwaletea heshima wazazi wao.

Kinyume chake, wengi wamejikuta wakijilaumu kwa kushindwa kuleta heshima katika familia zao. Binti umri unaenda, anatamani kuingia kwenye ndoa lakini hapati wa kumuoa. Au mwingine inatokea, anatamani kuolewa lakini anaishia kupigwa mimba na kuachwa.

Badala ya kuleta heshima, analeta aibu katika familia yake kutokana na mila na desturi zetu kumtaka binti azae pale tu atakapokuwa ameolewa. Azae pale atakapokuwa kwa mumewe na si vinginevyo. Inapotokea bahati mbaya basi ni mara moja na si kuzaa na kuzaa watoto kibao.

Pamoja na kuwa ndoa ni mpango wa Mungu lakini hivi umeshawahi kujiuliza wanaolewa wanakuwa na sifa gani? Kwa nini wanaume wanavutiwa nao? Wanakuwa na kitu gani cha ziada ambacho wanawake wengine hawana? Leo nitakuambia!

Jamani, sifa ya kwanza ambayo mwanamke anapaswa kuwa nayo ni ile hulka ya kuwa mke. Wanaume wengi huwa wanapenda kuishi na mwanamke ambaye ana ile sifa ya kuwa mke. Ninaposema sifa ya kuwa mke naamisha mwanamke ambaye atakuwa tayari kumlea mume na hata watoto.

Mwanamke ambaye atakuwa msaada kwa mwanaume wake pindi atakapokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo za maisha pamoja na maradhi. Mwanamke ambaye atajua thamani ya mume, ambaye atajua nini maana ya heshima kwa mumewe.

Mwanamke ambaye atamudu misukosuko ya maisha ikiwemo kufilisika, kuachishwa kazi na mengine magumu yanayofanana na hayo. Mwanamke ataka-yevaa sifa ya kuwa mke kwa maana ya kumhudumia mumewe pindi atakaporudi amechoka kutoka kazini.

Wanaoolewa ni wale pia ambao wanajua kushuka pindi wanapoona kumetokea kutoelewana. Wanawake wale ambao wanajua kumtoa uchovu wa maisha mwanaume. Mwanamke ambaye hasababishi makelele ya mara kwa mara kwenye ngoma za masikio ya mwanaume.

Mwanamke ambaye hana gubu. Mwanamke atakayeelewa kwamba muunganiko wa ndoa una pande mbili hivyo kuwajali ndugu wa pande zote mbili, ndugu zake na ndugu wa upande wa mumewe. Mwanamke ambaye atakuwa na muonekano wa mke kwa maana ya mavazi na hata mazungumzo.

Wanaoolewa jamani wanakuwa na sifa ya uvumilivu. Wanakuwa na hofu ya Mungu. Mwanamke mwenye hofu ya Mungu, anamuomba yeye ampatie mwanaume mcha Mungu na kweli inatokea. Kuna siri kubwa sana katika kumuomba Mungu ambayo wengi wetu hatuijui lakini ni vyema kumtanguliza yeye katika kila jambo.

Ukiwa na sifa hizo, hata kama hautakuwa na muonekano wa kimisi au kuwa na shepu bomba kama wanavyosema vijana wa kisasa, utaolewa tu na hizo ndizo sifa za mwanamke anayetaka kuolewa!
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...