Friday, August 7, 2020

Kisa kamili mlipuko mkubwa Lebanon, kuteketea kwa bandari na Nahodha wa meli



Serikali ya Lebanon imesema kuwa mlipuko mkubwa ulioteteresha maeneo kadhaa ya mji wa Beirut umesababishwa na tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate iliyokuwa kwenye bandari ya mji huo.


MV Rhosus iliwasili bandari ya Beirut mwaka 3013 ikiwa imebeba tani 2,750 za kemikali ammonium nitrate


Watu wameonesha ghadhabu zao na kutoamini kuwa kiasi hicho kikubwa cha kemikali hatari iliwekwa kwenye ghala bila kuzingatia hatua zozote za usalama kwa zaidi ya miaka sita, kwenye eneo hilo ambalo liko karibu sana na eneo la katikati ya mji.


Serikali haijaeleza kemikali hiyo ilipotoka, lakini kiasi hicho hicho cha kemikali kiliwasili Beirut mwezi Novemba mwaka 2013 katika meli ya mizigo ya iliyokuwa na bendera ya Moldova, MV Rhosus.


Chombo hicho kinachomilikiwa na Urusi kilianza safari mwezi Septemba kutoka Batumi, Georgia kwenda Beira, Msumbiji.


Ilikuwa imebeba tani 2,750 za ammonium nitrate, ambayo huwa katika muundo wa madonge madogo madogo ambayo hutumika kutengeneza mbolea lakini pia inaweza kuchanganywa na mafuta kutengeneza vilipuzi kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini na katika sekta ya ujenzi.


Wakati ikisifiri kupitia mashariki mwa Mediterranea, MV Rhosus ilipata "tatizo la kiufundi" na ikalazimika kutia nanga bandari ya Beirut, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 iliyoandikwa na mwanasheria wa Lebanon aliyewawakilisha wafanyakazi wa meli hiyo.




Meli hiyo ilifanyiwa uchunguzi na maafisa wa bandari na "kuzuiwa kufanya safari", mawakili walisema. Sehemu kubwa ya wafanyakazi wake walirudishwa makwao, isipokuwa nahodha wa meli Mrusi, Boris Prokoshev, na wengine watatu walioripotiwa kuwa raia wa Ukraine.


Bwana Prokoshev aliliambia shirika la habari la Reuters siku ya Alhamisi kuwa meli hiyo ilikuwa inavuja, na kuwa ilipelekwa Beirut na mmiliki wake kwa ajiliya kubeba mzigo mwingine zaidi kwa sababu ya changamoto za kifedha.


Hatahivyo, wafanyakazi wa meli hiyo hawakuweza kubeba mzigo huo , na mmiliki aliposhindwa kulipa ada ya bandarini, mamlaka ya Lebanon iliizuia meli hiyo, alisema.


Muda mfupi baadae, MV Rhosus "ilitelekezwa na wamiliki wake.


Muda kidogo baadae, MV Rhosus "ilitelekezwa na wamiliki wake kuonesha wasiwasi kuwa hawahitaji tena mzigo", kulingana na wanasheria.


Wakati huo huo, bado wafanyakazi walikuwa wamezuiwa kwenye chombo hicho walikuwa wakikosa chakula na mahitaji mengine. Mawakili hao walisema waliomba kwa Jaji wa Masuala ya dharura huko Beirut atoe amri ya kuwaruhusu warudi nyumbani, wakisisitiza "hatari ambayo wafanyakazi walikuwa wakikabiliana nayo kwa kuzingatia" hatari "ya shehena ya mizigo" kwenye meli.Boris Prokoshev (Kulia), nahodha wa MV Rhosus, na raia wa Botswana Boris Musinchak wakiwa kando ya meli iliyobeba shehena ya kimikali ya ammonium nitrate


Hatimaye Jaji alikubali kuruhusu wafanyakazi wa meli hiyo kushuka na mwaka 2014 mamlaka ya bandari ilihamisha kemikali ya ammonium nitrate na kuiweka katika "ghala namba 12", karibu na ghala la nafaka.


Mawakili walisema mzigo huo ulikuwa "ukisubiri kupigwa mnada au kuharibiwa".


"Mzigo huo ulikuwa wenye uwezo wa kulipuka. Ndio maana ulibaki ndani ya meli tulipokuwa huko…," alisema bwana Prokoshev.


Aliongeza: "Nina masikitiko kwa watu (waliopoteza maisha au kujeruhiwa na mlipuko). Lakini mamlaka nchini humo zinapaswa kuadhibiwa. Hawakuujali mzigo huo kabisa."Transparent line


Mkurugenzi Mtendaji wa bandari, Hassan Koraytem, na Mkurugenzi wa mamlaka za mapato, Badri Daher, kwa pamoja walisema siku ya Jumatano kuwa wao na maafisa wengine walikuwa wakitahadharisha mahakama kuhusu hatari ya kuhifadhi kemikali ya ammonium nitrate na uhitaji wa kuiondoa.


Nyaraka zilizosambaa mtandaoni zilionesha barua za maafisa hao kwenda kwa jaji wa masuala ya dharura mjini Beirut wakitaka muongozo jinsi ya kuuza au kuharibu ombi ambalo lilipelekwa karibu mara sita tangu mwaka 2014 mpaka mwaka 2017.


Bwana Koraytem alikiambia chombo cha habari cha nchini humo OTV kuwa idara ya usalama pia ilituma barua za tahadhari.


Waziri wa ujenzi Michel Nijjar, ambaye ameingia madarakani mwanzoni mwa mwaka huu, aliiambia Al Jazeera kwamba alibaini uwepo wa kemikali ya ammonium nitrate mwishoni mwa mwezi Julai na kuwa alizungumza na bwana Koraytem kuhusu jambo hilo siku ya Jumatatu.


Mlipuko katika bandari ya Beirut uliua watu takribani 137 na kuwajeruhi watu karibu 5,000, wengine wakiwa hawajulikani walipo.Athari za mlipuko mjini Beirut


Rais Michel Aoun amesema kuwa kushindwa kushughulikia mzigo wa meli ya Rhosus "hakukubaliki" na kuahidi "kuwashughulikia waliohusika na katika kitendo cha kizembe cha kupuuza na kuwaadhibu vikali."


Serikali imeamuru maafisa waliohusika na kuhifadhi au kuongoza shughuli za kukamata mzigo wa shehena ya kemikali ya ammonium nitrate.




Source

Umuhimu wa kula ndizi katika kujitibu tatizo la nguvu za kiume

Ndizi ni kati ya matunda na vyakula vitamu sana vinavyopendwa  katika jamii ya kiafrika. Mbali na utamu wake ni kwamba ndizi husaidia kuongeza nguvu za kiume.

Vitamini B na Bromelaini ambazo hupatika kwenye ndizi huchangia kuongezeka kwa homoni fulani ya kufanya mapenzi kwa wanaume.

Pia ulaji wa ndizi zinakupa nguvu zaidi inayomstahimilisha mtu anapofanya mapenzi na kumfanya amtosheleze mpenzi wake kimapenzi.

Ukweli ni kuwa ndizi uchangia kwa kiasi kikubwa kusafisha mishipa ya damu, kusaidia kupitisha damu na pia hupatia moyo nguvu zaidi.

Hivyo basi, ndizi hazisaidii tu kuongeza nguvu za kiume, bali pia huponya wanaume wasio na nguvu za kufanya mapenzi, yaani impotent.

Makosa sita ambayo wanaume hufanya kabla ya kufanya mapenzi! Pia, ndizi husaidia kupunguza mrundiko wa mawazo(Stress) ambao huwa ndiyo tatizo kuu la wanaume linalowafanya kutosimamisha mkuki.

Hivyo basi kwa njia hii ndizi yaweza boresha utamu wa mapenzi kitandani. Anza kula ndizi kwa wingi . Ukila aghalabu moja kwa siku itakufaa. Na kabla kwenda kukutana na mpenzio, kula ndizi moja au mbili kwa sababu pia harufu yake ni nzuri, mdomo hautanuka.

Thursday, August 6, 2020

Serikali Yahimiza Mabenki kutoa Mikopo Miradi Mikubwa ya Madini

Na Jonas Kamaleki
Serikali imezitaka benki na taasisi nyingine za fedha kukopesha miradi mikubwa ya uchimbaji wa madini nchini ili kukuza sekta hiyo ambayo imeanza kutoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa.

Akifungua mafunzo haya leo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema imekuwa ndoto yake ya muda mrefu ya Tume ya Madini kukutana na mabenki kwa ajili ya mustakhabali wa wachimbaji wa madini.

"Sekta ya madini kufungamanishwa na mabenki ni hatua kubwa katika kukuza sekta hiyo ambayo ina mchango mkubwa kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla", amesema Nyongo.

Waziri Nyongo amebainisha ukuaji wa haraka wa sekta ya madini nchini na kusema kuwa miaka michache iliyopita sekta ya madini ilikuwa ikichangia aslimia 3.8 kwenye pato la Taifa lakini kwa sasa inachangia zaidi ya asilimia 5.2, ameongeza kuwa sekta hiyo inakuwa kwa asilimia 17.7.

Amesisitiza elimu ya biashara ya madini kuendelea kutolewa kwa mabenki ili kuwajengea uwezo wakopeshaji ili kutambua fursa zilizopo kwenye sekta ya madini na kuwataka kuajiri wataalaam wa madini ambao wanaweza kuchambua michanganuo ya mikopo ya uchimbaji wa madini.

"Natoa wito kwa mabenki mengine kupitishwa kwenye mafunzo haya ili waweze kuwakopesha wachimbaji hasa wadogo na kwa kufanya hivyo kipato chao kitaongezeka, ajira zitaongezeka na mabenki yatafanya biashara kutokana na riba", alisema Nyongo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Katibu Mtendaji Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya amesema kuwa sekta ya madini ni sekta muhimu katika uchumi ambayo inahitaji mitaji mikubwa katika uwekezaji wake hivyo watoa mikopo ni muhimu kuwa na uelewa wa sheria na kanuni za madini.

"Sekta ya madini ni biashara kama biashara nyingine inahitaji mitaji mikubwa hivyo ninyi watu wa benki inabidi mjue vizuri leseni za madini, uhai wa leseni hizo na sheria na kanuni za madini", alisema Prof. Manya.

Aidha, Prof. Manya amesema mafunzo hayo yataondoa kusitasita kutoa mikopo kwa wachimbaji hasa wadogo baada ya kuwa na uelewa mpana kuhusu mnyororo wa madini unaohusu wachimbaji, wauuzaji, vifaa vya uchimbaji na uchakataji wa madini na watoa huduma wengine katika sekta hiyo.

Prof. Manya ameyaomba mabenki mengine kujengewa uwezo na kutoa mikopo kwa wachimbaji wa madini kwa kuzingatia vigezo vilivyopo ikiwemo uhai wa leseni ya mchimbaji.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo, Meneja wa Dawati Maalum la Wateja wakubwa Fredrick Mwamyalla amesema benki ya CRDB kwa kushirikiana na Tume ya Madini imeandaa mafunzo hayo kutokana na mageuzi yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ikiwemo kuanzisha masoko ya madini, kurekebisha Sheria ya Madini na kudhibiti mianya ya utoroshaji madini.

"Kupitia mafunzo haya tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kubuni bidhaa nzuri zinazohusu utoaji mikopo kwa sekta ya madini, hasa kwa wachimbaji wadogo, wakubwa na wa kati", alisisitiza Mwamyalla.

Mwamyalla ametoa wito kwa wachimbaji, wanunuzi na wauzaji wa madini kufika CRDB Benki ili kupata mikopo ya kuwawezesha kuwekeza katika sekta hiyo.

Maafisa Waandamizi wa Benki ya CRDB wamepewa mafunzo kuhusu sekta ya madini ili kujengewa uwezo katika sekta hiyo ili kurahisiha utoaji mikopo kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa ikiwemo watoa huduma.

Mafunzo hayo ambayo yameanza leo (Agosti 6, 2020) jijini Dodoma yanatolewa na wataalaam toka Tume ya Madini.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa. Baadhi ya mada ni Sheria na Kanuni za Madini, Jiolojia na Madini yanayopatikana nchini na Leseni za Madini. Mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuyajengea uwezo mabenki kwani yalianza kutolewa kwa benki ya NMB.


Tuesday, August 4, 2020

Fatma Karume Amlipua Msajili wa Vyama Vya Siasa



Aliyekuwa Rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) Fatma Karume amemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi kutaja kifungu cha sheria kilichovunjwa na wanachama wa chama CHADEMA.

Fatma amesema hayo kupitia ujumbe wake alituma kwenye ukurasa wake twitter na kutaka kutoa ufafanuzi ili wanachama wa chama hicho kujua kosa lao.

"Francis ni mwanasheria angeanza kwa kutaja ibara ya Katiba iliyovunjwa na kipengele cha sheria kilichovunjwa ili wananchi waelewa" Ameandika Karume.

Mapema leo Agosti 4, 2020 msajili huyo wa vyama vya siasa alituma onyo kwa chama cha CHADEMA juu ya kitendo chao cha kuongeza beti kwenye wimbo wa Taifa.

Amnesty yaishutumu polisi ya Marekani

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeishutumu polisi nchini Marekani kwa uvunjaji wa haki za binadamu za waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.

Katika ripoti yake iliyochapishwa hii leo, shirika hilo linasema polisi ilitumia vurugu za kimwili mara kwa mara, kemikali kama vile gesi ya kutoa machozi na pilipili, pamoja na vitupo vingine visivyo na madhara makubwa kama risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji wa amani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, matukio ya hivi karibuni yamezusha wasiwasi kuhusiana na haki za kuishi, usalama wa mtu, ulinzi sawa wa sheria, uhuru wa kutobaguliwa na uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani.

Shirika hilo la haki za binadamu limeorodhesha matukio huru 125 ya matumizi ya nguvu isivyo laazima katika majimbo 40 pamoja na mji mkuu Washington.

Monday, August 3, 2020

BIGAMBO AKERWA KAULI ZA "WAJUMBE SIYO WATU WAZURI"

Mtia nia kugombea Ubunge Jimbo la Busanda  Simon Bigambo Chozaile 

Katika hali inayoonesha kuchukizwa na kauli zinazoendelea kutolewa dhidi ya Wajumbe wa CCM katika Uchaguzi wa kura za maoni kwenye mchakato wa kupata wagombea Ubunge na udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi, Kada wa CCM Simon Bigambo Chozaile ambaye naye alijitosa katika mchakato wa kuomba chama chake kimchague kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Usanda ameandika waraka ufuatao:

WAJUMBE KUTUKANWA, KUSEMWA VIBAYA NA KUONDOLEWA UTU WAO

Tangu tarehe 20/7/2020 na 21/7/2020 pamekuwepo kauli tofauti tofauti kutoka kwa Wagombea wengi wa Chama chetu Cha Mapinduzi (CCM) hasa wale ambao kura zao hazikutosha wakionesha kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo sio watu wazuri kwa sababu hawakuwapigia kura.

Ninaomba kutumia fursa hii kusema mambo machache kuhusu hili;
Kwanza wagombea hawa wameshindwa kujua kikao hiki kina uzito gani na kwamba kugombea kwao hakungebadili maoni ya wajumbe wa mkutano wa Jimbo.

Wanatakiwa watambue kuwa Wajumbe wanayo haki kikatiba kuchagua kiongozi ambaye wanampenda na wangependa awaongoze.

Wajumbe ni watu wazima na kwamba wanayo maamuzi yao na maamuzi yao ni Siri yao kwa hiyo hata wakicheka na wewe bado wanayo maamuzi ya ama kukuchagua au kutokukuchagua.

Hivyo naomba wagombea wenzangu ambao kura zetu hazikutosha tuwaheshimu viongozi wetu wa Chama yaani Mwenyekiti wa CCM wilaya, Wenyeviti wa CCM kata zote zilizounda Jimbo ulilogombea, makatibu wa CCM na makatibu waenezi wa kata zote.

Viongozi wa Jumuiya zote ngazi za kata yaani Wazazi, UWT na UVCCM ngazi za kata na matawi. Hawa ni viongozi bwa CCM katika ngazi zao wa wanastahili heshima.

 USHAURI WANGU KWA WAGOMBEA
Kwanza kutambua mkutano wa Jimbo ni mkutano ambao unatoa maoni ya muhimu kabisa katika hatua za upembuzi wa nani apeperushe bendera ya CCM katika Jimbo husika.

Wagombea wawaheshimu wajumbe (viongozi wa CCM ngazi ya Jimbo) kwani kushindwa kwao kusiondoe utu wa viongozi wetu.

Ndugu zangu wagombea ni lazima mkubali kuwa hata kama tungekuwa wawili bado mshindi alitakiwa mmoja. 

Hivyo kauli zenu zinaingilia vikao vya juu zaidi katika kufanya maamuzi yake.

Naamini wote wanaotumia kauli hii wengi sio wazalendo na walikwenda na majibu ya Uchaguzi mifukoni.

Pili wengi ni wasanii, wahuni na wasiojua mipaka na kanuni za chama chetu pamoja na utendaji wake.

Mwisho ninawaomba wasiendelee kutumia lugha chafu, lugha za kejeli na matusi na zenye kuondoa utu wa viongozi hawa wa Chama katika ngazi husika.Hawa ni viongozi wa Chama na maoni yao yaheshimiwe na matarajio ya kugombea kwetu yasiondoe utu wao. Naomba tuwe na kiasi na nidhamu kwa viongozi wetu.

Imetolewa na Simon Bigambo Chozaile (0674101933)
 Mgombea Ubunge CCM Jimbo la BUSANDA


Simon Bigambo Chozaile akichukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Busanda mwezi Julai 2020




Aubameyang kujiunga na Chelsea, mashabiki washtushwa na taarifa hizo


Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ameshangaza watu baada ya kuibuka kwa taarifa za kuwa anafikiria kuhamia Chelsea mwezi Januari.

Aubameyang mwenye umri wa miaka 31, ameonyesha nia hiyo ya kuhamia The Blues siku moja kabla ya mchezo wao wa Fainali kombe la FA Cup.

Hata hivyo hadhima yake ya kuhamia Chelsea imeonekana kugonga mwamba baada ya Chelsea kutokuwa na kiasi kikubwa cha fedha cha kumlipa Aubameyang.

Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao, Aubamayeng amesajiliwa Arsenal akitokea Borussia Dortmund kwa dau la paundi milioni 56 mwaka 2018.


Kocha wa Chelsea, Frank Lampard kwa sasa anatafuta mchezaji wa safu ya ushambuliaji lakini hana msuli wa kumlipa nyota huyo raia wa Gabon na kama atahitaji kuitumia The Blues lazima Aubamayeng ashushe dau lake la mshahara.

Aubameyang amefunga jumla ya magoli 27 msimu huku Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta akifanya kila jitihada kuhakikisha anambakiza nyota huyo ambaye pia anawindwa na Barcelona na AC Milan.


Saturday, August 1, 2020

Picha zamfikisha tena Nandy BASATA



Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza  amesema sababu ya kumwita msanii Nandy ofisini kwao jana Julao 30, ni kutokana na picha alizopost kwenye mtandao wa Instagram ambapo kwa mujibu wa Basata wamesema sio picha nzuri. 


Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Godfrey Mngereza amesema kuwa wamemwita kuzungumzia kuhusu utaratibu wa picha alizopost Instagram ambazo hazikuwa nzuri. 


"Mara nyingi tumekuwa na utaratibu wa kuzungumza na wasanii, kuna picha kadhaa ambazo alikuwa amezirusha kwenye mtandao wa Instagram yake ambazo hazikuwa nzuri, kwa hiyo mahali alipofikia yeye si vizuri kupost picha kama zile,  vilevile kuwa makini na suala la mitandao hivyo ndiyo vitu tulivyomkumbusha tena kwa njia chanya kabisa, sisi kama Basata tuna wajibu wa kuwakumbusha wasanii kabla hatujaenda kwenye upande wa adhabu" Katibu Mtendaji Basata Godfrey Mngereza



Source

Yajue mahitaji makuu ya mafanikio kwa msaka mafanikio

Mahitaji makuu ya mwandamu katika kuishi vyema hapa duniani anahitaji chakula, mavazi na maradhi, hii ni kwa mujibu ya mwalimu wangu ambaye aliwahi nifundisha miaka ya nyuma kidogo. Lakini tukiachana na mahitaji hayo, Itakuwa ni vigumu sana kama unataka kufikia ndoto yako kama hautakuwa na vitu vifuatavyo.

1. Lengo kuu.
Lengo kuu hutokana na malengo mengine madogo madogo. Kama ilivyo, ili iitwe bahari ni lazima bahari hiyo iweze kupokea maji kutoka vyanzo vingine vya maji kama vile vijito, mito, mabwawa na mengineyo ndipo itatokea bahari. Kwa kuona mfano huo tunaweza tuangalie mfano mwingine ambao itatusaidia kufukia lengo kuu,

kama unahitaji kuwa mfanyabiashara mkubwa unahitaji kuwa na malengo mengine madogo madogo ambayo ndiyo yatakufanya kukamilika kwa lengo hilo kuu. Hivyo kila wakati ikumbukwe ya kwamba ni lazima uweze kuyapapalilia vyema malengo yako madogomadogo kwani ndiyo chanzo kikubwa cha kufikia mafanikio yako.

Hivyo ili uweze kuwa mwenye mafanikio makubwa kwa upande wako unahitaji kuwa na lengo kuu ambalo litakufanya uwezo kutimiza ndoto yako.

2. Sababu
Hakuna mafanikio bila ya kuwa na sababu ya kufanya kitu hicho. Kila kitu inachokiona katika dunia hii kumbuka ya kwamba mwanzilishi wa kitu au jambo hilo alilianzisha kwa sababu maluumu. Huwezi kusema unataka kufanya jambo fulani kama huna sababu, kwani mafanikio ya aina hiyo utawasikia kwa majirani tu.

Hivyo kila wakati kwa kila jambo ambalo unalitaka kulifanya, kabla ya kufanya jambo hilo kumbuka ya kwamba ni lazima utafute sababu ya kufanya jambo hilo. Kama hautapata majibu ya kufanya jambo hilo ni vyema akaliacha kulifanya, kwani kama utaamua kulifanya jambo bila ya kuwa sababu, jambo hilo litakufa tu baada ya siku chache. Hivyo kumbuka kila kitu ambacho unakifanya au unataka kukifanya ni lazima kuwe na sababu maalumu.

3. Msukumo wa kiutendaji.
Mafanikio hayajatokea kama ajali kama hakutakuwa na msukumo wa kiutendaji juu ya jambo hilo. Msukumo humfanya Mtendaji wa jambo hilo kuweza kutendeka kwa ufasaha kila wakati. Hivyo kila wakati usifanye kitu kwa sababu mtu fulani amesema ufanye, kwani kama atafanya hivyo utakosa hamasa ya msukumo juu ya utendaji wa jambo fulani.

Hivyo kuwepo kwa lengo kuu, sababu ya kutenda jambo na msukumo wa kiutendaji hiyo ndiyo siri kubwa iliyojificha katika kufikia ndoto ambayo unayo.

Na. Benson Chonya

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...