Friday, November 8, 2019
Zijue sifa za mwanaume ambaye hana malengo na wewe katika mahusiano ya kimapenzi
Mara nyingi unapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi basi mwanaume ambaye hana malengo na wewe katika mahusiano yenu basi utmajua kwa kuangalia mambo yafuatayo;
Anakwepa mazungumzo ya ndoa.
Haonyeshi kufurahi unapoanzisha mazungumzo kuhusu suala la kufunga ndoa na wala hapendi kuzungumzia hilo. Wakati mwingine hata kukutambulisha kwa ndugu zake au rafiki inakuwa shida.
Anagharamia anasa kuliko mambo muhimu.
Anakuwa ni mtu wa kukununulia mapambo ya gharama na vitu vyote vya anasa, lakini hana mawazo ya kuzungumzia maisha yenu ya baadaye wala kukununulia vitu ambavyo vitakuwa na manufaa katika maisha ya mbeleni. Haangalii masuala ya elimu wala kukutafutia mtaji au kazi.
Hajali machozi yako.
Unaweza kugundua ni jinsi gani hana mpango mzuri na maisha yako, kwani hata anapokuudhi anakuwa hajali wala haumizwi na machozi yako, ni busara kuwa makini kwa sababu huyo atakuwa ni mtu wa kukupa maumivu wakati wote.
Hajitokezi hadharani
Mwanaume ambaye malengo yake ni kukuchezea huwa hataki mapenzi yenu yajulikane hadharani atakuwa mtu wa kutaka mambo yaende kwa siri. Hajitambulishi kwa rafiki wala kwa ndugu zako. Hatoi nafasi ya wewe kumtembelea nyumbani kwake wala kuwajua wale wa karibu yake na familia yake.
Hana mpango na watu wako
Mwanamume anayekupenda atajishughulisha na mambo yanayohusiana na watu wako wa karibu, hususan ndugu, jamaa na marafiki zako. Utabaini kuwa mwanamume huyu haulizi swali lolote kuhusiana na familia yako au marafiki zako, basi tambua kuwa hana mpango wowote wa maana na wewe. Kumbuka mwanamume akikupenda hujaribu kuwafahamu na kuwapenda watu wako, maana amependa boga na sheria ni kwamba lazima upende na ua lake.
Hakumbuki lolote la maana
Ni wazi kuwa hujakaa sana na mwanamume huyu, lakini angalau kuna mambo muhimu umefanya naye ambayo anapaswa kuyakumbuka. Kama hawezi kukumbuka tarehe muhimu za uhusiano wenu, basi yamkini mwanamume huyu hana mpango wowote wa dhati wa kuendelea kuwa nawe.
Source
Kwanii Wanaume Waaminifu Kwenye Uhusiano Huachwa.....
Kuachwa na mpenzi kwa sababu umekuwa ni muaminifu sana yaonekane ni jambo lisiloingia akilini lakini linatokea.
Moja ya mambo ya ajabu unayoweza kuwa ushawahi kuyasikia ni kwamba mara nyingine uamuzi wako wa kuwa mwanaume mwema sana na unayejitahidi kufanya uhusiano wako wa kimapenzi uwe mzuri muda wote unaweza kukugharimu na kujikuta unaachwa kabisa.
Haitakiwi kuwa hivyo lakini mara nyingine inatokea, na inatokea kwa sababu wazo la mwenza wako kuhusu uhusiano wa kimapenzi laweza likawa tofauti na ulionao wewe. Wengine wana mawazo hasi kuhusu jinsi uhusiano/ndoa inavyotakiwa kuwa.
Hii ndio sababu hutakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu asiye na vipaumbele sawa na vya kwako au asiye na mtazamo mmoja wa kimaisha kama ulionao wewe.
Usipozingatia hilo, utajikuta unaingia kwenye uhusiano na mtu ambaye hatakujali vya kutosha kwakuwa labda humfokei au kumpiga anapokukosea – au utajikuta ameshakupanda kichwani na kuanza kukudai mambo ambayo huwezi kuyatimiza lakini ukajikuta unajitutumua kumtimizia kwa sababu unataka kumfurahisha mpenzi wako na analijua jambo hilo.
Kwa sababu baadhi ya wanaume wanapenda kulinda siri na kuwaachia uhuru wapenzi wao, wanajikuta wakiwapa ruhusa wanawake zao kwenda popote wanapojisikia bila kuwafatilia wanachofanya.
Nini kinafata baada ya hapo? Mwanamke anatoka, anatafuta mchepuko na kukusaliti. Mwisho inakufanya wewe mwanaume uonekane mjinga mbele ya wengine.
Tatizo ni kwamba tabia hii inaibuka kutokana na mazoea ya watu kuingia kwenye uhusiano wakiwa wameficha tabia zao halisi na kuja kufungua makucha yao baada ya kuona ameshaishi na wewe kwa muda mrefu kiasi kwamba huwezi tena kumuacha.
Hii inasababisha wanaume walioathirika kutokana na tabia kama hizi kutoka kwa waliokuwa wapenzi wao wasiweze kuwaamini wanawake wengine tena kwa kuona kwamba wote ni sawa na wale waliowaumiza na kusababisha wasiweze kuwaonesha wenza wao wapya mapenzi kwa kiwango cha juu wakihofia kuumizwa tena.
Kuwa mpole, mkarimu na mwenye upendo wa hali ya juu kwa mpenzi wako ndio jambo linalotarajiwa kwenye uhusiano. Mtu hatakiwi kufanywa ajisikie vibaya kwa kumuonesha mapenzi ya kweli mwenza wake.
Kama wewe unakuwa muaminifu na mwema kwa mpenzi wako lakini umekuwa unadharauliwa au ukaachwa kutokana na tabia hiyo, kaa ukiwa na amani kabisa kwamba lawama za kuvunjika kwa uhusiano huo hazikuhusu wewe – lawama ni za mpenzi wako aliyeshindwa kujua wewe umekuwa mwema kiasi gani kwake.
CHADEMA WATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KWA MADAI YA KUFANYIWA RAFU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kujitoa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika November 24, mwaka huu. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza uamuzi huo leo kwa madai kuwa uchaguzi huo ni batili na wakishiriki watahalalisha ubatili huo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema sababu kubwa ni wagombea wa chama hicho kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.
Mbowe amesema mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho na wabunge, maazimio waliyokubaliana ni kugomea uchaguzi huo sababu majina ya wagombea wengi kukatatwa.
"Sisi kama chama tumeamua hatutashiriki zoezi hili na ninatoa amri kama Mwenyekiti wa viongozi na wagombea nchi nzima wasitishe kugombea na wasitishe kukata rufaa.
"Waachane na kuweka mapingamizi hatupo tayari kubariki ubatili." amesema Mbowe.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.
Wednesday, November 6, 2019
Dalili kuu 7 zinazoonyesha mtu ambaye atachelewa sana kufanikiwa
1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo lakini hana PESA za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.
2. Siku Zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia Movie, kusoma magazeti na Kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana MUDA wa Kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.
3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza Kwao.
4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.
5. Siku Zote Hujiona anajua Kuliko Mtu Yeyote Yule na hapendi Kujifunza kwa wengine. Huongea sana Kuliko Kusikiliza.
6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.
7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.
Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo? Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo .... NDOTO YAKO INAWEZEKANA, CHUKUA HATUA.

China, Ufaransa zasaini mikataba ya kibiashara
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa China Xi Jinping wametangaza leo kusaini mikataba mikuu ya kibiashara mjini Beijing ya kiasi cha thamani ya dola bilioni 15.
Mikataba iliyosainiwa ni ya sekta za usafiri wa angani, nishati na kilimo. Kampuni 20 za Ufaransa zilipewa idhini ya kuuza nyama ya kuku, ng'ombe na nguruwe nchini China.
Macron na Xi wametangaza mikataba hiyo katika kikao cha wanahabari kama sehemu ya ziara ya kiongozi huyo wa Ufaransa nchini China.
Habari hizo zimekuja wakati kukiwa na ongezeko la mivutano ya kiuchumi kati ya China na Marekani.
Xi amesema katika taarifa kuwa viongozi hao wawili wametuma ujumbe thabiti kwa ulimwengu kuhusu umuhimu wa kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na biashara huru pamoja na kushirikiana katika kujenga demokrasia za wazi.
Aidha, Viongozi hao wawili walitoa taarifa ya pamoja wakielezea kuunga mkono Mkataba wa Paris kuhusu Mazingira uliotiwa saini 2015 wakiutaja kuwa usioweza kubatilishwa.
Marekani ilianza rasmi mchakato wa kujitoa rasmi wiki hii.

Naombeni Msinilaumu kwa Uamuzi Huu Niliouchukua kwa Mume Wangu
Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha. nikamsamehe
Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe
wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu
kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..
nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wkt tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena..
nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.
Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo
1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa lolote..
2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje
3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona km nazidiwa mawazo vile

Tuesday, November 5, 2019
ZANTEL YAZINDUA SIMU JANJA IJULIKANAYO KAMA SMARTA YENYE UWEZO WA 4G NA GHARAMA NAFUU
Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Jamila Muga (Julia),akionyesha simu janja na ya gharama nafuu ya SMARTA iliyozinduliwa na Zantel mjini Zanzibar. Simu hii inayonunuliwa ikiwa na GB 12 intaneti inayowezesha matumizi ya mwaka mzima inapatikana kwa shilingi 39,999/- nchini pote. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Zantel
**
Katika jitihada zake za kuongeza wigo wa watumiaji wa simu janja nchini Tanzania, Zantel imezindua simu janja yenye uwezo wa 4G na gharama nafuu sana sokoni ijulikanayo kama SMARTA.
Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Jamillah Muga, alisema simu iliyozinduliwa imetengenezwa kwa teknojia zinazowezesha matumizi ya programu za simu janja zinazowezesha kupata programu za kuelimisha na kuburudisha kama vile, WhatsApp, Facebook, YouTube, Google na inapatikana kwa bei nafuu ya shilingi 39,999/-.
Alisema simu ya SMARTA ni aina mpya ya simu katika soko la Tanzania inayowezesha kuongeza idadi ya watumiaji wa simu janja nchini kote na kuleta mabadiliko ya kidigitali kwenye jamii.
"Tumezindua simu aina ya SMARTA katika soko kuwezesha wananchi wengi kumudu kumiliki simu janja sambamba na kuwapatia fursa ya kufurahia maisha ya kidigitali kupitia mtandao wa 4G+ wa Zantel". Alisema Muga.
Muga, alisema kuanzia sasa simu janja zijulikazo kama SMARTA zinapatikana katika maduka yote ya Zantel yaliyopo Pemba, Unguja, na Tanzania bara na zinanunuliwa zikiwa tayari zimeunganishwa na intaneti ya bure yenye GB 12 itakayowezesha mteja kuitumia kwa kipindi cha miezi 12.
Mkuu wa Zantel Zanzibar,Mohammed Mussa Buacha, alisema kuzinduliwa kwa simu mpya za SMARTA ni moja ya mkakati wa Zantel kuleta mapinduzi ya kidigitali na kuwezesha kupatikana teknolojia za kisasa kwa gharama nafuu nchini kote. Alisema Zantel inaamini kuwepo kwa bidhaa za kisasa kwa matumizi ya huduma za kidigitali kunabadilisha maisha ya wananchi kuwa bora.
''Kupitia mapinduzi ya kidigitali yanawezesha kupata elimu, taarifa za afya, burudani, huduma za kifedha na kwenye intaneti inawezesha kujua mambo mbalimbali yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku. Dira ya Zantel ni kuwezesha upatikanaji wa huduma za kidigitali kwa manufaa ya wateja wetu wapya na wa zamani". alisisitiza Mussa.
Alisema kupatikana kwa simu za gharama nafuu za SMARTA, ni suluhisho la kuwezesha watanzania wengi kuweza kumudu kumiliki simu janja nchini na kuwezesha kuendeleza matumizi ya huduma za kidigitali Zanzibar "Kuanzia sasa Watanzania hawana sababu ya kuwa na vikwazo wanapotaka kununua simu janja".
Zantel imekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika ubunifu kwendana na ongezeko la watumiaji wa huduma za data na kuunganishwa kwenye intaneti yenye kasi kubwa ambapo ili wengi wafurahie huduma hizo kunatakiwa kuwepo simu janja za gharama nafuu.
Monday, November 4, 2019
Rais Magufuli " Usijifanye Muhimili, Kaliheshimu Bunge"
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere, leo Novemba 4 Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumpa maagizo katika kazi yake mpya.
Moja ya maagizo aliyompa ni kuhakikisha anasuka upya uongozi ndani ya taasisi hiyo ili kuhakikisha kuwa inafanya kazi kulingana na sheria na maagizo ya mihimili inayoongoza nchi.
Maagizo mengine aliyopewa ni, "CAG nenda kafanye kazi huko, usije ukajifanya na wewe ni muhimili mwingine, mihimili ni mitatu na umeshaiona hapa. Nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Serikali, kafanye kazi zako vizuri bila ya kuonea watu.
"Unapopewa kazi na mihimili mingine kama Bunge au Mahakama kaitekeleze usibishane nao wewe ni mtumishi. Kasimamie hiyo ofisi kuna baadhi ya watendaji wako wanapokwenda kukagua kwenye balozi wanaomba fedha, sasa nenda kawachambue." Amesema Rais Magufuli.
Aidha, amesema Rais ana mamlaka ya kumtoa CAG kulingana na Katiba na Sheria akieleza kuwa upo uwezekano wa mtumishi wa nafasi hiyo kutolewa muda wowote hata chini ya miaka mitano.
"Unaweza kumaliza miaka yako mitano au ukaishia mmoja. katika maisha ya duniani huwezi ukapewa mamlaka ya kuteua halafu usiwe na mamlaka ya kutengua, sikutishi lakini wewe nenda kafanye kazi zako"
Kuhusu suala la rushwa, Rais Magufuli amesema, "lakini pia kasimamie hiyo ofisi kuna baadhi ya watendaji wako wanapotumwa kwenda kukagua kwenye balozi wanalipwa pesa hapa na wakifika huko nako wanaomba pesa, ofisi ya CAG sio safi kama mnavyofikiri".
Kijana Aliyemtishia Mwenzake Kwa Bastola Afikishwa Mahakamani
Kijana Shaban Hamisi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na kosa la kumtishia silaha Dereva wa lori la mchanga Venance John ikiwa ni siku chache baada ya kusambaa mitandaoni video ya tukio.
Amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga mbele ya Hakimu Mfawidhi, Frenk Moshi, ambapo inadaiwa tukio hilo amelitenda Oktoba 30, 2019 maeneo ya Mbezi Mabwepande.
Inadaiwa alikutwa na Pistol aina ya Berreta yenye namba za usajili 102969 ambapo kwa makusudi alimtishia Venance John huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, baada ya kusomewa shtaka alikana ambapo pia upande wa mashitaka umesema hauna pingamizi na dhamana.
Baada ya kueleza hayo, Hamisi ambae pia ni Mume wa Mtangazaji Zamaradi Mketema ameachiwa kwa dhamana ya Wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho vya Taifa na wamesaini Bondi ya Sh.Mil 2 kwa kila mmoja, kesi imeahirishwa hadi November 13, 2019, mshitakiwa yupo nje kwa dhamana.

Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...