Wednesday, August 1, 2018

Mkwasa akimbizwa hospitali India, msemaji wa Yanga amtakia kila la kheri

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesafiri kuelekea India kwa ajili ya matibabu. Taarifa zinaeleza kuwa, Mkwasa amesafirishwa kuelekea nchini huko kutokana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Huu ndiyo ugonjwa unaomsumbua Mkwasa Afisa habari wa klabu ya Yanga, …

The post Mkwasa akimbizwa hospitali India, msemaji wa Yanga amtakia kila la kheri appeared first on Bongo5.com.


Source

MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MAGHARIBI AWAPOKEA WAMAREKANI JIMBONI KWAKE

Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa, Elibariki Kingu, akihutubia katika hafla ya kuwapokea viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri kutoka Marekani waliotembelea Zahanati ya Kanisa hilo ya Kijiji cha Msungue iliyopo Kata ya Sepuka mkoani Singida jana. Zahanati hiyo inasimamiwa na kanisa hilo Dayosisi ya Kati. Dotto Mwaibale
Mkurugenzi anayesimamia Hospitali na Zahanati za Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, Mchungaji Manase Msengi, akimuonesha picha ya vitanda vya Hospitali vinavyo sambazwa na Bohari ya Dawa (MSD), Mkurugenzi wa Uhusiano Kati ya Sinodi ya Kusini Mashariki ya Minessota na makanisa ya nje ya Marekani, Callemia Chatelaine. Kushoto ni Mganga wa zahanati hiyo.
Mganga wa zahanati hiyo akiwaelekeza jambo wageni hao walipotembelea chumba cha maabara cha zahanati hiyo.
Mkurugenzi anayesimamia Hospitali na Zahanati za Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, Mchungaji Manase Msengi, akiwaelekeza jambo wageni hao eneo ilipofungwa mfumo wa maji katika zahanati hiyo.


Source

Trumpa Apiga Marufuku Kuingiza Marekani Nguo Kutoka Rwanda

Trumpa Apiga Marufuku Kuingiza  Marekani Nguo Kutoka Rwanda
Marekani imepiga marufuku uagizaji wa nguo kutoka Rwanda , baada ya taifa hilo la Afrika mashariki kupiga marufuku uingizaji wa mitumba na viatu nchini humo kutoka Marekani.

Rais Donald Trump ametoa agizo hilo akipiga marufuku uondoaji wa ushuru kwa nguo zote zinazotoka Rwanda kwa miezi sita baada ya kukutana na rais Paul Kagame na kumuita rafiki yake.

Kulingana na agizo hilo jipya ni wazi kwamba nguo za Rwanda hazitaingia tena katika soko la nchi hiyo bila kutozwa ushuru.

Ukweli wa mambo: Kwa nini baadhi ya nchi za Afrika hazitaki nguo za msaada

Serikali ya Marekani inasema kuwa Rwanda imeshindwa kuafikia masharti ya sheria ya AGOA iliopitishwa miaka 18 iliopita kuruhusu bidhaa zaidi za Afrika kuingia nchini Marekani.

Rwanda iliuza nguo zenye thamani ya dola milioni 1.5 nchini Marekani mwaka 2017 lakini hiyo ni asilimia 3 pekee ya bidha inazouza nchini Marekani.

Mwaka 2016, ,majirani wa Afrika mashariki Kenya, Tanzania na Rwanda zilikubaliana kupiga marufuku nguo zilizotumika pamoja na viatu kufikia 2019 ili kulinda viwanda vya nchini .

Kenya na Tanzania zilisalimu amri baada ya Marekani kutishia kupiga marufuku bidhaa zao zinazoelekea nchini humo lakini Rwanda imeendelea kuwekea ushuru mkubwa nguo hizo pamoja na viatu.

Rais Trump na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walijadili biashara walipokutana mnamo mwezi Januari nchini Switzerland lakini hakuna hata mmoja wao aliyezungumzia mzozo kuhusu nguo hizo.

Marekani inadai kwamba marufuku dhidi ya nguo zilizotumika barani Afrika itawanyima raia 40,000 kazi , lakini Rwanda imesema kwamba haitakubali kuwa 'jaa'.

Serikali Kumnyang’anya Mohammed Enterprises Mashamba.


Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula amesema serikali imekusudia kuchukua baadhi ya mashamba yanayomilikiwa na Kampuni ya Mohammed Enterprises na kuwapa wananchi kwa kuwa wameshindwa kutimiza masharti ya endelezaji wake.

Mhe. Mabulla amesema hayo baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mashamba katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambapo amegundua kampuni ya Mohammed Enterprises inamiliki maeneo makubwa sana kwa zaidi ya hekta 9,418 sawa na hekari 20,779 ambayo wamechukulia mkopo kwa ajili ya kupanda mkonge, kitu ambacho hakijafanyika kwa asilimia kubwa.

"Hii kampuni ya Mohammed Enterprises imetupa taarifa ambazo si za kweli kwamba wameendeleza maeneo yao wanayoyamiliki kwa asilimia 83, mimi nimefika katika mashamba yote 14 wanayoyamiliki na nimeona ni eneo kubwa sana ambalo limebaki pori na halijapandwa mkonge tangu wakabidhiwe mwaka 2000 takribani miaka 17 sasa wakati wananchi wa Korogwe wanakosa maeneo ya kulima, kuishi na kufugia" amesema Mhe. Mabula.

"Kwa sasa Wizara yangu imejiridhisha kwamba kuna haja ya kugawa maeneo yanayomilikiwa na Mohammed Enterprises ambayo hayajendelezwa kwa kupandwa mkonge ili wapewe wananchi wa Korogwe ambao wana uhaba wa ardhi kwa muda mrefu kutokana na maeneo makubwa kumilikiwa na watu wachache". Mhe. Mabula ameongeza.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla amefanya ziara ya ukaguzi wa mashamba yote 14 yanayomilikiwa na Kampuni ya Mohammed Enterprises na kugundua kuwa amepanda mkonge eneo dogo sana na sehemu kubwa ni mapori tofauti na taarifa aliyopewa na kampuni hiyo.

Waziri pia amesema mashamba hayo yametumika kuchukua mikopo benki lakini mikopo hiyo haijatumika kuendeleza mashamba hayo kitu ambacho kinafanya wananchi wayahitaji maeneo hayo lakini wanashindwa kuyatumia kwa kuwa yanamilikiwa na kampuni ya Mohammed Enterprises.

Akijatetea mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi Meneja anayesimamia Mashamba yote ya mkonge ya kampuni ya Mohammed Enterprises ndugu Newalo Nyari mesema kwamba si kweli kwamba hawajaendeleza maeneo hayo bali wameendeleza na wamepanda mkonge baadhi ya maeneo na mengine wameyaacha mapori ili kuhifadhi misitu na mengine wanawaachia wananchi waweze kupanda mazao yao ikiwa ni ushirikiano wa kijirani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni aliyekuwa akikaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Godwine Gondwe ambaye ameonesha kukasirishwa na maneno ya meneja huyo kwamba wameendeleza mashamba hayo wakati yeye mwenyewe ameshuhudia kwa macho yake mashamba yote 14 na kuona hali halisi ya mapori ambayo hayaendelezwa.

Baadhi ya wananchi wa Korogwe wameonesha kufurahishwa na hatua hiyo ya Serikali ya kuipunguzia umiliki wa baadhi ya maeneo yanayomilikiwa na kampuni ya Mohammed Enterprises ambayo watapewa wananchi hao ili waweze kufanya shughuli zao za maendeleo.

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya ubatilishaji umiliki wa mashamba ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mwenye dhamana ya kumyanga'anya mmiliki wa ardhi au mashamba baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Ardhi.

Babu Tale atoboa siri ya maisha yake ndani ya WCB ‘Sijaenda shule lakini sijawahi kujutia’ (+video)

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale ameamua kuweka wazi kuwa yeye hajaenda shule kabisa kupata ujuzi na hajutii kwa hilo katika maisha yake ya sasa.
Babu Tale akifunguka kwenye kamera za Bongo5 amesema kuwa licha ya kukosa elimu ya darasani lakini katika familia yao amelelewa katika misingi ya dini na ndiyo maana pengine amefika hadi hapo alipo kwa sasa.
Akizungumzia kazi yake kubwa ndani ya WCB amesema kuwa yeye ni HR (Human Resource) na ana-play role kubwa pia kwenye kutoa ushauri na mawazo ndani ya WCB kwani hapendi maneno maneno.
The post Babu Tale atoboa siri ya maisha yake ndani ya WCB ‘Sijaenda shule lakini sijawahi kujutia’ (+video) appeared first on Bongo5.com.

Source

Lugola Amtaka Zitto Kabwe Ajisalimishe Polisi Haraka Sana


Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amemtaka mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kujisalimisha kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi kwa maelezo kuwa ametoa kauli za uchochezi.


Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 31, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.


Amesema Zitto ametoa kauli za uchochezi na kuwatukana viongozi wa Serikali wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Kilwa Kusini.


Katika mkutano huo Zitto alialikwa na mbunge wa jimbo hilo, Seleman Bungara maarufu Bwege.


"Kosa jingine la Zitto ni kwenda kufanya mkutano eneo ambalo sio la kwake kwa mujibu wa taratibu. Nampa siku mbili ajisalimishe kwa RPC (Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi)," amesema Lugola.


"Akikaidi nitamuagiza IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini-Simon Sirro) amkamate popote alipo. Nilishasema na nitaendelea kusema katika uchaguzi huu na zijazo watu wanaotukana  viongozi hawatabaki salama."

Katika hatua nyingine, Waziri Lugola amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mkuu wa Polisi Wilayani Kilwa(OCD) kutokana na kumruhusu Zitto kuendelea kufanya mkutano katika jimbo lisilo lake.

" Na pia namulekeza IGP achukue hatua kwa mkuu wa polisi wa wilaya ya kilwa ocd, ya kwa nini hakuchukua hatua dhidi ya zitto kwa kuendelea kufanya yale tuliyoyakataza," amesema.

BALOZI MPYA WA KENYA AKARIBISHWA NCHINI TANZANIA




Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akitoa hotuba yake kwa wageni mbalimbali waliohudhulia dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018. Kulia ni Mke wa Balozi Kazungu, Bi. Mapenzi Kazungu.
Kiongozi wa Mabalozi nchini na Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura akizungumza jambo kwa niaba ya Mabalozi wengine, wakati wakimkaribisha Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu, katika dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018. 
Kaimu Balozi wa Kenya nchini, Boniface Muhia akizungumza katika dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini Balozi mpya wa Kenya, Dan Kazungu, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018. 
Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu (kushoto) akiwa katika mazungumzo yenye furaha na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Kenya hapa nchini, wakati hafla fupi ya kumkaribisha Balozi huyo, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018.


Source

Maimartha Aongelea Kumuita Jokate Mama wa Taifa.

Mtangazaji na mc maarufu nchini Maimartha amefunguka na kuongelea  video iliyo-trend sana katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ikimuonyesha akiwa katika  hafla ya Zamaradi  akimuita jokate mama wa taifa swala lililozua sana mtafaruku katika mitandao. Maimarha anasema kuwa swala la yeye kumuita Jokate hivyo ni kwa sababu Jokate amekuwa mwanamke wa kuigwa na wanawake wengine kutokana na kujitoa kwake katika jamii hasa baada ya kuwa akifanya mambo mengi ya kunufaisha jamii. Jokate ni mwanamke, oate ni mfano wa kuigwa,nadhani nilichokisema hata mh magufuli kakiona  hicho kitu na kama mwanamke unapokuwa unajulikana tumia hiyo nafasi kuelimiesha wengine , hata kama unasema kiasi gani,haijalishi kwenye mahusiano yako uumekutana na changamoto gani.haijalishi umedondoka au umeanguka mara ngapi.she is a mom, ni mama na kuna ambao wameunganisha , Unaweza ukaiunganisha lakini  naomba wasinitafutie shida..

The post Maimartha Aongelea Kumuita Jokate Mama wa Taifa. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

UJUMBE WA WATAALAMU WA AFYA KUTOKA BRAZIL WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR.

Na Ramadhani Ali – Maelezo

Ujumbe wa watu nane wa Wataalamu wa afya kutoka Serikali ya Brazil upo Zanzibar kutekeleza ombi la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein kuitaka nchi hiyo kuzidisha ushirikiano katika sekta ya Elimu, Afya na Utalii.

Ujumbe huo ukiongozwa na Mratibu Mkuu wa Kanda ya Afrika, Asia, nchi za Oceanic na Mashariki ya mbali Fabio Webber umefanya mazungumzo na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed kujifunza changamoto zinazowakabili mama wajawazito na watoto wachanga.

Webber alisema Rais wa Zanzibar alipofanya mazungumzo na Balozi wa Brazil aliomba nchi hiyo kufungua ubalozi mdogo Zanzibar, kusaidia kuimarisha masuala ya afya na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta hiyo.Balozi wa Heshma wa Brazil hapa Zanzibar Abdulsamad Abdulrahim alisema baada ya Serikali ya Brazil kufungua Ubalozi mdogo Zanzibar, wanaelekeza nguvu zao juu ya afya ya mama mzazi na mtoto pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kitengo hicho.

Alisema ujumbe huo utafanya ziara katika vituo mbali mbali vya afya Unguja na Pemba kuangalia changamoto zinazowakabili mama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga na hatiamae kuzitafutia ufumbuzi.Waziri wa Afya aliueleza ujumbe huo kuwa Serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya ya msingi vijijini ili vituo vya afya vya huko viwe na uwezo na vifaa vya kutosha na wananchi waviamini na wavitumia.

Alisema hivi sasa kumekuwa na msongamano mkubwa wa wazazi katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja huku vituo vya afya vijijini vyenye uwezo wa kutoa huduma za kuzalisha vinakosa wazazi kutokana na dhana kuwa huduma ni ndogo.Alisema kuimarika kwa vituo vya afya vya vijijini vinavyotoa huduma ya mama na mtoto kutaipunguzia hospitali hiyo msongomano wa wazazi na kumudu kutoa huduma zilizo bora zaidi.

Ujumbe huo umeanza kazi ya kutembelea vituo vya afya vinavyotoa huduma ya kuzalisha kuona hali halisi na kujua changamoto zinazovikabili vituo hivyo na baadae kufanya uchambuzi wa kujua masuala yanayopaswa kutekelezwa kuongeza mashirikiano .
BALOZI wa Heshima wa Brazil hapa Zanzibar, Abdulsamad Abdulrahim (suti buluu) akiwa na Ujumbe wa wataalamu wa Afya kutoka Brazil wakitembelea Kituo cha Afya Fuoni.
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashoid Mohamed akizungumza na Ujumbe wa Wataalam wa Afya kutoka Nchi ya Brazil Afisini kwake Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
UJUMBE wa wataalamu wa Afya kutoka Brazil wakiangalia takwimu za mama wajawazito wanaofika kupata huduma ya kujifungua Kituoni hapo

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...