Friday, April 10, 2026
AMANI NI SILAHA YA KUTIMIZA NDOTO NA MAONO YETU- MSIGWA
Thursday, April 9, 2026
SAMAMBA ATOA WITO GST KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI, KUIMARISHA USHIRIKIANO

Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Wednesday, April 8, 2026
TRA TANGA YAVUKA MALENGO KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO NDANI YA MIEZI TISA KUANZIA JULAI 2025 HADI MACH 2026.
MAMLAKA ya mapato (TRA)mkoani Tanga imeweka rekodi mpya ya ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya jumla ya Shilingi Bilioni 406.17 katika kipindi cha miezi tisa (Julai 2025 – Machi 2026), ikiwa ni ongezeko la asilimia 137 ya lengo lililowekwa.
Katika kipindi hicho, Mkoa ulikadiriwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 296.3, ambapo ufanisi huo mkubwa uliovuka lengo kwa takriban Shilingi Bilioni 110, umetajwa kuwa ni matokeo ya ushirikiano wa karibu kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), walipakodi, na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Castro John, amewashukuru walipakodi wa Tanga kwa kulipa kodi kwa hiari na kushirikiana na taasisi mbalimbali kama Chama cha Wafanyabiashara (JWT) na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA).
"Huu ni ufanisi mkubwa ambao haujawahi kutokea. Tunamshukuru Mkuu wa Mkoa na vyombo vya usalama kwa kuhakikisha mazingira ya ukusanyaji kodi yanakuwa salama. Sifa hizi ni za walipakodi wa Tanga ambao wamekuwa wasikivu na wazalendo kwa nchi yao," alisema John.
Licha ya mafanikio hayo, John ametoa onyo dhidi ya wafanyabiashara wanaotumia njia zisizo rasmi (njia za panya) kuingiza bidhaa nchini. Alibainisha kuwa bidhaa za magendo siyo tu zinaikosesha serikali mapato, bali ni hatari kwa afya ya mlaji kwani hazijapita katika taasisi za udhibiti wa ubora.
Aliongeza kuwa operesheni dhidi ya magendo zinaendelea na wafanyabiashara kadhaa wameshakamatwa na kutozwa faini kubwa (Penalties), huku akisisitiza kuwa chombo chochote kitakachokutwa kimebeba bidhaa za magendo kitataifishwa kulingana na sheria. Aidha, aliwataka wananchi kudai risiti za EFD na wafanyabiashara kutoa risiti halali katika kila manunuzi.
Meneja huyo, amewahimiza wafanyabiashara kutumia Bandari ya Tanga ambayo sasa inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kutoa mizigo kwa wakati, jambo linalochochea ukuaji wa biashara mkoani hapa.
Kuhusu wafanyabiashara wenye madeni makubwa, TRA imewataka kufika ofisini kwa ajili ya majadiliano (Negotiations) ili kuwekewa utaratibu wa kulipa kwa awamu. Mamlaka hiyo imebainisha kuwa imeweka "Dawati la Wafanyabiashara" kwa ajili ya kutoa elimu na kusaidia kukuza biashara ndogo ziweze kufikia hatua ya kuwa walipakodi wakubwa.
Meneja huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza kukadiriwa mapato yao ili kuepuka changamoto wakati wa zoezi la ukaguzi barabarani.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...










