![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOEbHi-xbmoKuu5g2h-cJKxv5J3NXpIi14RRAJl2r-e0cEiDHz-n_PGjL_Siq860IZoqTIyLP-wlpDUjPGMWRgJ9b4MYQnNJ4XsSP-uPCC90OlB2WYGXu9sTbZE7xbrSSpaX1S-uDARiMMc23r_F-1ZMo-dIQr40eqwNkfyiU-X23y-LFWM7wAXdoGww/w640-h366/vyandarua.png)
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amezindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya, ambapo vyandarua zaidi ya milioni 1.5 vitagawiwa kwa wananchi katika halmashauri sita za mkoa huo.
Halmashauri hizo ni Manispaa ya Kahama, Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Msalala, Ushetu, na Kishapu.
Akizungumza leo Jumamosi Februari 8,2025 wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika katika Kata ya Old Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Macha amewahimiza wananchi kutumia vyandarua vyenye dawa ili kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Amesema Mkoa wa Shinyanga una kiwango cha maambukizi cha asilimia 16, ikiwa ni juu ya kiwango cha maambukizi cha kitaifa ambacho ni asilimia 8.
Mhe. Macha amesisitiza kuwa usambazaji wa vyandarua utafanyika kwa usawa, na hakutakuwa na kizuizi kwa wananchi wa maeneo ya vijijini, ambao nao watafikiwa.
Amewataka wananchi kuachana na imani potofu zinazozungumzia matumizi ya vyandarua, akisema kuwa madai ya vyandarua kupunguza nguvu za kiume au kuleta kunguni si ya kweli.
Vyandarua vitagawiwa kwa wananchi wa Shinyanga kupitia Wizara ya Afya, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), OR-TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD), na wadau wa afya, kama sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupambana na malaria.
Kila kaya itapokea vyandarua kulingana na idadi ya watu katika kaya hiyo, ambapo chandarua kimoja kitagawiwa kwa watu wawili.
Usambazaji huu utafanyika kwa wananchi walioshiriki katika zoezi la uandikishaji kaya, ambao walipokea kadi maalum za usajili. Kwa wale waliopoteza kadi zao, watapata vyandarua kwa kwenda katika vituo maalum vilivyohifadhi taarifa za kaya zao.
Zoezi hili ni sehemu ya juhudi za serikali na wadau wake katika kupambana na malaria, ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu hatari katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya leo Februari 8,2025 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya

Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji Bohari ya Dawa (MSD), Victor Sungusia akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Peter Gitanya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Afisa kutoka OR- TAMISEM Best Yoram akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (kulia), akigawa vyandarua vinne kwa mwakilishi wa moja ya kaya yenye watu nane katika kata ya Old Shinyanga wakati wa uzinduzi rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (kulia), akigawa vyandarua vinane kwa mwakilishi wa moja ya kaya yenye watu 16 katika kata ya Old Shinyanga wakati wa uzinduzi rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya

Magari yakiwa tayari kusambaza vyandarua kwa wananchi katika halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga ambazo Manispaa ya Kahama, Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Msalala, Ushetu na Kishapu.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZSQhVI6Il-DFmUvRw95b3mpjRv5xvyaaXjgQkAxiro9IXW93ZZ4FSqu1qc5AjRx-pKilJq9D8U0e0OWkN_vvLrRL8xN1ydHMCa28nyrVGMRihILibZT5khHsTRPG32FpfyMusSDRsTPgFKN8krzPJ_j5TbizpOj5VnPtuF7uq8X1yoAJ2cXp6U-d2PQ/s600/2B9A6420.jpg)
Magari yakiwa tayari kusambaza vyandarua kwa wananchi katika halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga ambazo Manispaa ya Kahama, Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Msalala, Ushetu na Kishapu.
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, (kulia) wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhUH5iF1H6W7z9JqQljrDjh_Xly84z6_1PNdQo8KSqWEPOecnWqPxlJU2SDp1giwpq18ubs4kZ-oW8st3La0fOHZS5oIh6vSEI4MrycEgvAUW-Tahs57SyI8-1YF0qWjS2b5EU0V3ezr_U22jaHWmTTnLj2ariq0N-2u76OxgrRMoRIsDzbsv2zHDJT2g/s600/2B9A6438.jpg)
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Saidi Kitinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anold Makombe akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akiagana na wananchi wa Old Shinyanga baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akiwa amembeba mtoto katika kata ya Old Shinyanga baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akiwa akifurahia na mtoto katika kata ya Old Shinyanga baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akiwa ampatia zawadi mtoto katika kata ya Old Shinyanga baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog