Sunday, February 9, 2025

Kanye West Amtetea P Diddy, Ashirikiana Naye Kibiashara

Kanye West Amtetea P Diddy, Ashirikiana Naye Kibiashara


Licha ya kuwa rumande akisubiri kesi dhidi yake kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu wa kingono, Sean "Diddy" Combs, 55, ameshirikiana na rapa Kanye West (Ye), 47, kuzindua mradi mpya wa mavazi.


Wawili hao wametangaza kuwa wameanzisha ushirikiano kati ya chapa za Yeezy na Sean John, na tayari wamezindua fulana tatu mpya.


Kanye West alitangaza ushirikiano huo kupitia Instagram yake, akiandika:


"YEEZY SEAN JOHN COLLAB AVAILABLE @ YEEZY.COM ME AND PUFF SPLITTING THIS 50/50 LIKE WE DISCUSSED BEFORE THEY LOCKED HIM UP."


Diddy naye alithibitisha taarifa hiyo kwa kuweka picha ya ushirikiano huo kwenye X (zamani Twitter), akiandika:

"Thank you to my brother @Ye YEEZY.COM."


Mbali na ushirikiano wa kibiashara, Kanye West ametumia mitandao ya kijamii kumtetea Diddy na kuitaka serikali imuachie huru. Kupitia X, Kanye alidai kuwa Diddy anadhulumiwa kwa makusudi ili kuwa funzo kwa wengine.


Aliandika:


"WANATAKA KUTOA MFANO KUPITIA PUFF, NA NYOTE MNALIJUA HILO. HUYU NI SHUJAA WANGU, HUYU NI IDOL WANGU."


Katika chapisho lingine, Kanye alidai kuwa Diddy haruhusiwi kupata pesa akiwa gerezani. Akaahidi kumtumia sehemu ya mapato yake kupitia mtoto wake Justin Combs.


Kanye pia alidai akaunti yake ya Instagram imefungwa, akimwomba Elon Musk msaada wa kutumia X kama mbadala.

Diddy kwa sasa anashikiliwa katika Metropolitan Detention Center huko Brooklyn, New York, gereza ambalo liliwahi kuwa na wasanii maarufu kama R. Kelly na 6ix9ine.


Hivi karibuni, alihamishwa kutoka gerezani na kupelekwa hospitalini baada ya kulalamikia maumivu makali ya goti kutokana na jeraha la awali. Kwa mujibu wa ripoti ya New York Post, alifanyiwa uchunguzi wa MRI scan, lakini hakulazwa hospitalini.


Licha ya changamoto hizi, ushirikiano wa Diddy na Kanye West unaonekana kuendelea, huku mashabiki wao wakisubiri kuona iwapo mradi huu wa mavazi utafanikiwa wakati Diddy akiendelea kusubiri hatma yake mahakamani.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...