Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Grace Janes Mushi (25) kwa tuhuma za kumchoma moto ndani ya nyumba aliyekua mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Khamis Abdallah (25).
Tukio hilo limetokea tarehe 16.07.2021 majira ya saa nane na nusu usiku huko maeneo ya Mbezi Makabe kwa Mzungu Wilaya ya Ubungo.
Mtuhumiwa Grace majira hayo ya saa nane usiku aliamka na kumfungia mlango kwa nje Khamis Abdallah kisha kumwagia mafuta ya petroli nyumba hiyo, kitendo kilichopelekea Khamisi kuungua na kufariki dunia akiwa ndani.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kimapenzi.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE