Saturday, July 17, 2021
MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUTUMIKA KUJAZA FOMU ZA UHIARI WA KUPATA HUDUMA ZA CHANJO DHIDI YA CORONA
Na WAMJW – DOM.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema kuwa Serikali imejiapanga kuwa na mifumo miwili ya kujaza fomu ya uhiari wa kupata huduma ya Chanjo ya Corona ikiwemo kupitia njia ya Kielektroniki na njia ya karatasi.
Dkt. Subi amesema hilo wakati akiongea katika Taarifa ya Habari iliyorushwa na TBC (ARIDHIO) ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya mlipuko wa tatu wa ugonjwa wa Corona na umuhimu wa Chanjo ili kupambana dhidi ya ugonjwa huo.
"Utaratibu ambao Serikali imeweza kuuweka ni kwamba, tutakuwa na mifumo ya aina mbili moja itakuwa ni mifumo ya kielektroniki ambapo mtu anaweza akatoa uhiari wake kwa kujaza mwenyewe kwamba anahitaji kwenda katika kituo Fulani kupata chanjo za ugonjwa wa COVID-19" Dkt. Subi.
Aliendelea kusema kuwa, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikiendelea kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya huduma mbali mbali za tiba ana kinga, hivyo kusisitiza kuwa baada ya utoaji wa Elimu, mwananchi anakuwa na uhiari wa kupata huduma au kutopata.
"Sisi kama Wizara ya afya tumekuwa tukiwapatia Wananchi elimu ya kutosha juu ya huduma fulani, sasa ukishampatia elimu ya kutosha , mwananchi anakuwa na uhiari wa kupata huduma au kutoipata, sawa sawa na mgonjwa anapoenda kufanyiwa huduma za upasuaji, tumekuwa tukimpatia huduma ya fomu ya uhiari" Dkt. Subi
Aidha, Dkt. Subi amesema kuwa, hiari inaweza kuwa kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi, hivyo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona Serikali ikaona ni vizuri kwa Watanzania kuendelea kutoa hiari yao katika kupata huduma hizi za Chanjo ya Corona.
Mbali na hayo Dkt. Subi aliwatoa hofu wananchi kwa kusema kuwa, Chanjo za ugonjwa wa Corona ni bora, salama, zina ufanisi wa kutosha na zimeorodheshwa na Shirika la Afya Duniani kwaajili ya matumizi ya dharura ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
"Chanjo hizi ni salama na zina ufanisi wa kutosha lakini pia ni bora, tunaposema Chanjo hizi zimeweza kuorodheshwa na Shirika la Afya Duniani kwaajili ya matumizi ya dharura hususan katika kipindi hiki ambacho Dunia imekubwa na wimbi kubwa la ugonjwa wa COVID – 19" alisema Dkt. Subi
Alisisitiza kuwa, Serikali imedhamiria kwa dhati kuutokomeza ugonjwa wa Corona, na ndio maana inatumia afua zote za kupambana dhidi ya maambukizi ikiwemo uvaaji sahihi wa Barakoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji safi tiririka, kuepuka misongamano isiyo ya lazima, kutumia vipukusi, kufanya mazoezi na matumizi ya Chanjo ya ugonjwa wa Corona.
Hata hivyo, Dkt. Subi amewatoa hofu Watanzania na kuwataka waendelee kuiamini Serikali na kufuata maelekezo yote kutoka kwa Wataalamu wa Afya katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa Corona, huku akisisitiza kuwa Sayansi haiwezi kupindishwa na maneno ya mitandao ya kijamii.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
