Thursday, June 24, 2021
Tatizo la umeme Njombe kumalizwa baada ya siku 28
Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dkt. Medard Kalemani amesema changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara mkoani Njombe itakwisha baada ya siku 28.
Dkt. Kalemani ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe (CCM), Deo Mwanyika.
Mwanyika amehoji ni lini tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara mkoani Njombe litatatuliwa.
Akijibu swali hilo, Dkt. Kalemani amekiri suala hilo na kubainisha kuwa unakatika kwa sababu kuna matengenezo yanaendelea ambayo yatachukua siku 28.
Amesema katika maeneo ya Njombe na Ludewa kuna laini ya umeme ambayo inaongezwa na kwamba ujenzi huo umetengewa Sh270 milioni.
Amebainisha kuwa pia wametenga Sh Milioni 100 katika Mkoa huo kwa ajili ya ukarabati wa mitambo na kuimarisha umeme Makambako, Njombe na Ludewa.
"Niwahakikishie ndani ya muda nilioutaja hali ya umeme itaimarika kwa kiasi kikubwa," Kalemani
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
