Friday, March 5, 2021

MWALIMU ALIYEMKATA PANGA MWALIMU MWENZAKE MZOZO WA PENZI LA MWANAFUNZI WA FIELD AFIKISHWA MAHAKAMANI



Mwalimu wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Karoti katika Kaunti Ndogo ya Mwea Mashariki nchini Kenya Timothy Musembi (34) ambaye alimshambulia na kumjeruhi mwenzake aitwaye Alphonce Orina (26) wakizozania penzi ameshtakiwa kwa jaribio la mauaji.

Inasemekana Orina alikuwa ofisini wakati mwenzake aliingia akiwa amejihami kwa panga na kuanza kumshambulia akimzomea kwa kumnyemelea mwalimu wa kike ambaye yuko kwenye mazoezi ya kufundisha shuleni hapo. 

Alimkata mara mbili kichwani na kumlaazimu Orina kujitetea kwa vita naye.

 Timothy Musembi, 34, alifikishwa Alhamisi, Machi 4,2021 mahakamani huko Wang'uru chini ya ulinzi mkali ambapo alitakiwa kujibu kosa la jinai.

Alidaiwa kuwa mnamo Machi 2,2021 katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Karoti katika Kaunti Ndogo ya Mwea Mashariki, alijaribu kumuua Alphonce Orina, 26, kwa kumkatakata kichwani na mikononi. 

Mahakama iliarifiwa kuwa wakati wa shambulio lililotokea afisini, mwathirwa alipata majeraha mabaya na ilibidi alazwe hospitalini kwa matibabu maalum. 

Alipofika mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Monica Kivuti, Bw Musembi alikanusha shtaka hilo na kuomba aachiliwe kwa dhamana.

Alisema kuwa mashtaka anayokabiliwa nayo yana dhamana na aliomba aachiliwe ili aweze kuhudhuria vikao vya mahakama akitoka nyumbani.

Hakimu Musembi aliamuru aachiliwe kwa dhamana ya KSh100,000 hadi Machi 17 kesi hiyo itakapotajwa. 

Hata hivyo, mshtakiwa alitupwa kizuizini kwani alishindwa kulipa hela hizo.

Inasemekana Orina alikuwa ofisini wakati mwenzake aliingia akiwa amejihami kwa panga na kuanza kumshambulia akimzomea kwa kumnyemelea mwalimu wa kike ambaye yuko kwenye mazoezi ya kufundisha shuleni humo. 

Mhasiriwa alijeruhiwa vibaya mikononi wakati alipkuwa akijaribu kujizuia dhidi ya makali ya panga ya mwenzake.

 Katika patashika hiyo, mwathiriwa alizidiwa na kuanguka chini ambapo walimu wengine walilazimika kuingilia kati na kumkimbiza hospititalini kwani alipoteza fahamu.

 Kisa hicho kiliwaacha walimu na wanafunzi wakiwa na hofu.

 Baadaye mshukiwa alijisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Wang'uru ambapo alizuiliwa kabla ya kufikishwa mahakamani Alhamisi.
 
Via Tuko News

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...