Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Mloganzila zimefunga mashine nne (Muhimbili tatu, Mloganzila moja) za kujifukiza ambapo gharama ya kila mashine ni Sh7.5 milioni na kila moja ina uwezo wa kuhudumia watu sita kwa wakati mmoja wanaopaswa kukaa kati ya dakika tano hadi 10 wakivuta mvuke wenye mchanganyiko wa dawa asili.
Akizungumza katika uzinduzi wa mashine hizo zilizopewa jina la Bupiji Sauna leo Alhamisi Machi 4, 2021 mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema kuanzishwa kwa mashine hizo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya kujifukiza kwa watu wote wanaohitaji.
"Kujifukiza huku kunaenda sambamba na matumizi ya dawa za asili ambazo zimekuwa zikitumiwa na zimeonyesha kusaidia, mashine hii inatumia dawa ya Bupiji inayowekwa katika maji ya mvuke na mgonjwa au mtu anayetaka anaingia ndani atakaa dakika tano hadi 10," Profesa Museru
Profesa Museru amesema uwepo wa mashine hizo kutawawezesha madaktari kujua kama njia hiyo inasaidia kwa kiwango gani vita dhidi ya corona.
Ili mtu aweze kujifukiza katika mashine hizo anapaswa kulipia Sh5,000 na yeyote anaruhusiwa hata wapita njia.
Source