Tuesday, February 16, 2021

Polisi 7 wapoteza maisha Afganistan

 


Maafisa 7 wa polisi wamepoteza maisha katika shambulizi la bomu katika wilaya ya Almar mkoa wa Faryab kaskazini mwa Afghanistan.


Msemaji wa Idara ya Polisi ya Faryab Abdul Kerim Yurish alitangaza kuwa bomu lililotegwa kando ya barabara katikati mwa Almar lililipuliwa wakati gari la polisi lilipokuwa likipita katika eneo hilo.


Yurish amesema kuwa maafisa 7 wa polisi wamepoteza maisha katika shambulizi hilo.


Hakuna mtu aliyedai kuhusika na shambulizi hilo mpaka hivi sasa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...