Monday, January 11, 2021
ZINGATIA ..Haya ni Mambo Matatu Ambayo Hupaswi ‘Kuya-Google’ Kamwe..!!!
Google imerahisisha njia za kufahamu mambo mengi ambayo binadamu angepaswa kutumia muda mwingi kuyatafuta au hata kulipia ili aweze kuyafahamu.
Kupitia Google unaweza kuwa na shule ya ziada ya ufahamu wa mambo mbalimbali yakiambatana na picha za aina unazotafuta. Ili mradi tu kuna mtu duniani aliwahi kuweka kwenye mtandao kwa ajili ya umma. Unachopaswa kuwa nacho ni kifaa cha mfumo wa 'computer' chenye mtandao.
Naweza kusema kuwa Google ni kama kioo cha ubongo wako, chochote unachotaka kukiangalia ndicho kitakachojitokeza kwenye kioo cha computer au simu yako yenye mtandao.
Wengi tumepata elimu kubwa sana na ufahamu wa mambo mengi makubwa na muhimu kupitia Google. Tunapata habari, burudani na mengine mengi.
Lakini nakumbuka mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia kuwa google ni msaada mkubwa kwa masomo yako, lakini ni chanzo kikubwa cha 'kukupumbaza' (google will make you stupid).
Kauli hiyo ndiyo iliyonifanya niweze kufikiria, ni mambo gani ambayo sipaswi kuya-google ili yasinifanye kuwa mpumbavu au yanayoweza kunidhuru kwa kuyaangalia?
Kwa bahati mbaya, wataalam wa Saikolojia wanaeleza kwamba akili ya binadamu hutamani sana kuangalia mambo yaliyozuiliwa kuangalia, kuliko mambo yaliyowekwa bayana.
Tukumbuke kuwa Google ni kama soko huria la mawazo ambalo karibu kila utakacho utapata, lakini huwezi kununua usichotaka. Kila aina ya usafi na uchafu hutupwa Google.
Mambo ambayo hupaswi kuya-google ni mambo yote ambayo, kwanza yatakubadili saikolojia yako na kufuata mambo ambayo kabla ya kuyagoogle ulijua kabisa hayafai katika jamii uliyopo.
Pili, ni mambo yote ambayo ni haramu kuyatamka au kuyazungumzia katika jamii yako, jiulize unataka kuyafahamu ili upate faida gani? Je, unahisi ukiyaona yatakusaidia kuendeleza zaidi maisha yako au yatakuondoa kwenye reli ya maadili na imani yako?
Tatu, mambo yote ambayo yanaweza kukuharibia siku kisaikolojia, unaweza kuona mateso, uchafu na mambo kama hayo ambayo yatakugharimu na kuichafua akili yako. Usijaribu ku-google vitu unavyovichukia au kukupa addiction mbaya kama picha za x au videos kisaikolojia vitakugharimu… hususan kama hakuna sababu muhimu na chanya zaidi ya kuviona.
Baki salama, usi-google kila kitu. Google isikufanye kuwa mpumbavu, google kwa malengo chanya na matokeo yatarajie kukujenga zaidi badala ya kukubomoa.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
