Monday, January 11, 2021

Rais wa Zambia amfuta kazi waziri wa afya, Sababu zaelezwa



Rais wa Zambia Edgar Lungu amemfuta kazi waziri wa afya nchini humo Bw Chitalu Chilufya, ambaye alikamatwa mwezi Juni kwa ufisadi lakini akaachiliwa baadae.


Bw Chilufya alishitakiwa makosa manne ya kumiliki mali ambazo alishukiwa kuzipata kwa njia ya uhalifu. Aliachiliwa huru kutokana na ukosefu wa ushahidi dhidi yake na kurejea kazini.

Jumapili Rais Lungu hakutoa sababu za kumfuta kazi, lakini akasema kuwa uamuzi huo unatekelzwa mara moja.

Social embed from twitter
twitter

RipotiReport this social embed, make a complaint

Mwandishi wa BBC Kennedy Gondwe ameripoti kuwa wizara ya afya imekuwa ikigubikwa na madai ya ufisadi, abapo madai ya hivi karibuni yalihusisha usambazaji wa mipira ya kondomu yenye kasoro ya thamini ya dola milioni 17 (£12m) pamoja na glovu zinazotumika katika shughuli ya upasuaji.

Kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema amesema kuwa "kumfuta kazi Dkt Chitalu Chilufya haitoshi na ni hatua ndogo sanailiyochelewa kuchukuliwa"


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...