Monday, January 11, 2021

MANAWASA yaweka wazi jumla ya madeni ya bili za maji ambayo taasisi za serikali zinadaiwa

 


Na Hamisi Nasri, Masasi 

   MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) imeweka wazi jumla ya madeni ya bili za maji ambayo taasisi za serikali zinadaiwa kwa kipicha cha kuanzia Januari hadi Disemba kwa mwaka 2020 ni sh.339.078,242.5  fedha ambazo zinakwamisha utendaji kazi wa mamlaka hiyo.

  Hayo yalisemwa jana mjini Masasi na mkurugenzi wa mamlaka hiyo,Tuntufye Mwamsojo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya MANAWASA katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ya Masasi (DCC) 

   Alisema katika kipindi cha kuanzia Januari mpaka Disemba mwaka 2020 mamlaka hiyo inazidai taasisi za serikali madeni ya bili za maji jumla ya fedha sh 339.078, 242.5 na kwamba taasisi zote zinazodaiwa zimekuwa sugu katika kulipa bili za maji.

  Alisema ili mamlaka hiyo iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma ya maji kwa wateja wake inahitaji makusanyo mazuri mazuri ya fedha za bili za maji lakini inavyotokea baadhi ya wateja kushindwa kulipa bili mamlaka inakwama kujiendesha katika utendaji kazi wake.

  Mwamsojo alisema anaoziomba taasi hizo kulipa bili zao za maji ili taasisi hiyo iweze kupata fedha hizo ambazo zitasaidia utekelezaji wa malengo ya mamlaka hiyo kwani ili mamalaka iweze kujiendesha kwa ufanisi zaidi inategemea fedha za malipo ya bili hizo kutoka kwa wateja.

  "Madeni ya bili za maji kuanzia mwezi Januari hadi kufikia mwezi Disemba mwaka 2020 yamefikia jumla ya sh. 339.078,242.5 kwa namna moja au nyingine madeni haya yanaikosesha mapato yake mamlaka hivyo hata utendaji kazi wa mamlaka unakwamza lakini kama fedha hizi tungepata zingesaidia katika uendeshaji,"alisema Mwamsojo  

   Aidha, Mwamsojo alisema kuwa mamlaka imefanikiwa kuongeza mauzo ya maji na kusimamia makusanyo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi kufikia Disemba ambapo ongezeko hilo la mauzo la maji limeweza kufikia mita ujazo 1, 063,918  

  Alisema sambamba na ongezeko la mauzo hayo ya maji lakini pia katika kipindi hicho cha mwezi Januari hadi Disemba mamlaka uzalishaji wa maji kwa mji Masasi na Nachingwea ulikuwa ni kiasi cha mita za ujazo 1,341, 09

   Mwamsojo alisema pia mamlaka inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ile ya vitendea kazi kama vile vyombo vya usafiri katika kusimamia na kufuatilia miradi ya maji na hiyo inatokana na ukubwa wa eneo la huduma.

    Alisema changamoto nyingine inayoikabili MANAWASA ni bado kuna changamoto ya kutolipwa kwa madeni ya nyuma kutoka kwa taasisi za umma pia kuna changamoto ya ukosefu wa mitambo ya ujenzi katika wilaya ya za Masasi na Nachingwea kwa ajili ya matengenezo ya mabomba makubwa pindi hitilafu inapojitokeza.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...